TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, June 16, 2016

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAKULIMA (AFP) AZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI JUU YA HUJUMA ALIYOFANYIWA

 

Baadhi ya wandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Saidi Sudi hayo pichani katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.


Na Mwandishi wetu –Habari Maelezo Zanzibar Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima ( A.F.P ) Said Suod Said amemshauri Msajili ya vyama vya siasa nchini kwenda kisiwani Pemba kufuatilia hujuma zinazoendea kufanyika kisiwani huko ili kuweza kuzipatia ufumbuzi . Hayo ameyasema huko katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kufanyiwa hujuma katika shamba lakeliliopo Mgelema Wilaya ya Chakechake. Alisema kwamba kuna baadhi ya watu wanafanya vitendo vya hujuma vinanyopelekea vinaashiria uvunjifu wa amani na wananchi kuogopa kuendelea kutoa huduma kisiwani humo. Alieleza kuwa baadhi ya hujuma hizo ni pamoja na kuchomewa moto kwa baadhi ya nyumba na kuharibu mashamba ya wananchi kukatiwa vipando ikiwemo mikarafuu, minazi na mashina ya muhogo hali ambayo inarejesha nyuma maendeleo na kutokukuwa uchumi wa nchi.“Vitendo hivyo vimekithiri watu kisiwani Pemba wamezidi siasa wanaifanya ushindani, watu wanashindana kwa kura sasa wao wanafanya hujuma mimi shamba langu wamenikatia mikarafuu 151 ikiwemo 14 tayari kuzaa, minazi 16 pamoja na mashina 250 yenye thamani ya sh. Milioni 200 inaniuma sana.” Alieleza Mwenyekiti huo. Alifahamisha kuwa siasa sio ugomvi kilichobakia ni kuleta maendelo ya nchi kwani uchaguzi umemalizika serikali tayari ipo madarakani hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kudumisha amani na kukuza uchumi wa nchi. Aidha amemuomba Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuzidisha ulinzi kisiwani Pemba kutokana na hujuma zinaendela kufanyika siku hadi siku kisiwani humo ili amani isije ikatoweka nchini. Amewataka Wazanzibar kuendelea kuwa wastahamilivu kutokana na hujuma zinaendelea kufanywa kisiwani huko kwani nchi inafuata sheria hivyo serikali inawajali wananchi wake na waendelee kudumisha amani.



Mhariri Mkuu Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhan Ali akimkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) ambae pia ni Waziri wa SMZ asie na Wizara Maalum Saidi Sudi azungumze na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Saidi Sudi akizungumza na waandishi wa Habari hawapo (pichani) kuhusiana na kadhia ya kukatwa mikarafuu, minazi na mihogo katika shamba lake lenye urefu wa eka moja na nusu huko Pemba.

No comments:

Post a Comment