TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 15, 2016

SMZ KUZUIA LESENI KWA WAFANYABIASHARA WATAKAOBAINIKA KUPANDISHA BEI ZA BIDHAA KWA MISINGI YA KISIASA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itawazuilia leseni wafanyabiashara watakaobainika kuwanyima huduma ama kuwapandishia bei baadhi ya wananchi kutokana na misingi ya kisiasa.

Akijibu suali la Mwakilishi wa viti maalum Viwe Khamisi Abdallah, katika Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar alietaka kujua iwapo Serikali inafahamu suala la hilo, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali alisema Serikali inalifahamu suala hilo na tayari linafanyiwa kazi na wakuu wa wilaya.

Balozi Amina alisema katika kisiwa cha Pemba kumekuwa na uchafuzi wa kisiasa na baadhi ya wanasiasa wanatumia nafasi hiyo kuwapandishia bei wananchi hususan wanachama wa CCM.

Alisema wamekuwa wakichukua hatua ya kuwafungia kwa muda mfupi wafanyabiashara wenye tabia hiyo lakini hivi sasa watawazuilia leseni kwa muda wa mwaka mmoja kama adhabu na onyo.

Mapema akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni Yussuf Hassan Iddi, Balozi Amina alisema Seriksali inafanya juhudi kubwa za kusimamia bei za bidhaa muhimu ikiwemo,mchele,Unga wa ngano,na sukari ili kuhakikisha hakuna upandaji wa bei kiholela.

Alikiri kuwa baadhi ya bidhaa hizo zimepanda bei kidogo kutokana na kupanda mara kwa mara kwa thamani ya Dola na kuongezeka kwa gharama nyengine za biashara zikiwemo kuchelewa kushusha mizigo bandarini.

Alisema Serikali imefanya juhudi kubwa kupunguza tatizo la upandaji wa bidhaa, ikiwemo kufanya mazungumzo na Shirika la Bandari pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima (ZNCCIA) ili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo. 

No comments:

Post a Comment