TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, June 16, 2016

KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD YASHINDA TENA TUZO YA UBORA


Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja katika maonyesho ya wiki ya Maziwa
Meneja uzalishaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Bw Lipita Mtimila akionyesha cheti cha ushindi wa jumla ambacho kampuni hiyo ilikabidhiwa
Bw Mtimila akionyesha vyeti vya ushindi wa uzalishaji wa bidhaa bora


Vyeti vya ushindi




KAMPUNI ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa kwa mara ya nne mfululizo imeendelea kushika nafasi ya kwanza kitaifa uzalishaji wa maziwa nchini . Kampuni hiyo imeshinda tuzo ya wazalishaji wakubwa wa bidhaa bora za maziwa katika mashindano wiki ya maziwa yaliyofanyika juzi kwenye viwanja vya shule ya sekondari Mpechi mkoani Njombe .

Kampuni hiyo imeibuka mshindi wa kwanza baada ya kuongoza katika nafasi zote tatu za ubora wa bidhaa zilizoshindanishwa katika mashindano hayo .Akikabidhi tuzo hizo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo pamoja na kupongeza makampuni yaliyoshiriki katika zoezi hilo bado alipongeza kampuni ya Asas Dairies Ltd kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo ya ubora wa maziwa nchini

Alisema kuwa jitihada zilizoonyeshwa na kampuni hiyo ni kubwa na zinapaswa kuigwa na makampuni mengine hapa nchini.Kwani alisema kuwa kuongoza katika nafasi zote zilizoshindaniwa si jambo dogo ni jitihada kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni hiyo.

Pia aliipongeza bodi ya maziwa Tanzania kwa kuandaa mashindano kama hayo kwani ni sehemu ya kipimo kwa wamiliki wa viwanda vya maziwa nchini na sehemu ya kujitathimini . Kwa upande wake meneja uzalishaji wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Lipita Mtimila alisema kuwa mbali ya kampuni hiyo kuongoza kwa mwaka huu bado ilipata kuongoza katika mashinadano kama haya miaka mitatu nyuma na hii ni mara ya nne kuongoza .
  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo akitembelea banda la kampuni ya Asas dairies Ltd
Viongozi wakitazama bidhaa za kampuni ya Asas

No comments:

Post a Comment