TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, June 14, 2016

DDCA yasaidia kupunguza tatizo la upatikanaji wa maji nchini.

 Wakala wa Uchimbaji visima na Mabwawa (DDCA) Umewezesha kupatikana kwa maji yenye ujazo wa mita zaidi ya milioni 23,000 kutokana na uchimbaji wa visima na mabwawa uliofanywa na wakala huo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa kitengo cha masoko na Uhusianao wa wakala huo Bw. Nungu Egwagwa wakati akitoa taarifa kuhusu miradi iliyokwisha tekelezwa na wakala huo tangu kuanzishwa kwake.
 
 Akifafanua Egwagwa amesema kuwa lengo la wakala huo ni kusaidia kutatua tatizo la upatikanaji wa maji kwa kuchimba visima na mabwawa kwa gharama nafuu ambazo wananchi walio wengi wanamudu.“Tunachokifanya ni kutoa huduma zaidi kuliko kufanya biashara kama Taasisi ya Serikali tukiwa na dhamira ya kusaidia wananchi kuwa na visima na mabwawa yenye ubora unaotakiwa”.
 
Alisisitiza Egwaga.Akizungumzia miradi iliyotekelezwa na Wakala huo, Egwaga amesema kuwa mpaka sasa Wakala umekwishajenga mabwawa 23 katika kipindi cha januari 1997 hadi june,2016 katika mikoa mbamimbali ikiwemo Tanga,Shinyanga, Tabora, Mtwara naPwani.Akitaja mikoa mingine ambako mabwawa hayo yamejengwa Egwaga alisema kuwa ni Ruvuma,Manyara,Mbeya, mwanza, Lindi na Mara.Akitoa mfano wa miradi ya uchimbaji visima Egwaga alisema kuwa moja ya miradi iliyotekelezwa ni ule wa kuchimba visima katika chuo Kikuu cha Dodoma hali iliyosaidia kuondoa kabisa tatizo la maji katika chuo hicho na katikamanispaa ya Dodoma.
Pia Egwaga alitoa wito kwa watanzania kutumia huduma zinazotolewa na wakala huo ikiwemo kufanya utafiti wa maeneo yanayofaa kuchimba visima virefu,kujenga malambo na mabwawa,kupima wingi na ubora wa maji yatokayo kwenye visima na ujenzi wa miradi midogomidogo ya mifumo ya usambazaji maji.Madhumuni ya DDCA ni kuongeza kasi ya kutafuta na kuviendeleza vyanzo vya maji kwa gharama nafuu ili kuboresha huduma ya upatikanaji maji safai na salama na kutosha kwa matumizi mbalimbali yakiwemo ya majumbani,mashambani,mifugo,ufugaji samaki na viwandani

No comments:

Post a Comment