TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, June 16, 2016

Watanzania watakiwa kutumia fursa za soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe 16.06.2016

WAFANYABIASHARA wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika soko la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuuza bidhaa zao ndani ya Jumuiya hiyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

“Wafanyabiashara wanatakiwa kuchangamkia fursa ya biashara katika soko la pamoja kwa kuwa ni haki yao na ni utekelezaji wa malengo ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu cha tano ambapo ilianzishwa itifaki ya umoja wa forodha ” ,alisema Bi. Mindi

Wafanyabiashara hao pamoja na wasafirishaji wanaotaka kufanya biashara katika soko la Jumuiya hiyo watatakiwa kuonesha cheti cha uasilia wa bidhaa wakati wakiingia nchi wananchama wa Jumuiya hasa kwa wafanyabiashara wadogo wenye bidhaa zisizozidi dola za kimarekani 2000, ambapo hawalazimiki kuwa na wakala wa forodha.


Wanatakiwa kufuata utaratibu kwa kufika katika kituo chochote cha forodha kilichopo mpakani wakiwa na bidhaa zao ili wapewe cheti cha uasilia wa bidhaa.Naye, Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, katika Wizara hiyo, Bw. Geofrey Mwambe, amesema ni vyema wafanyabiashara wakatoa taarifa endapo watakumbana na vikwazo visivyo vya kiforodha kupitia mfumo wa ujumbe mfupi kwa kuandika neno ‘NTB’ kwenda namba 15539.

Bw. Mwambe amesema pia ,madereva wanaosafirisha mizigo kwenda nchi wanachama watakapokutana na vikwazo visivyo vya kiforodha barabarani watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi kupitia namba 0713631780.

No comments:

Post a Comment