Posted: 02 Dec 2013 10:47 PM PST
Kampuni
na taasisi mbalimbali nchini zimeshauriwa kujua hali ya afya za
wafanyakazi kwa sababu itasaidia pia kuongeza mchango wao uzalishaji
katika sehemu zao za kazi, anaripoti Mwandishi Wetu.
Kauli
hii ilitolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Dar es Salaam (RAS),Teresia Mbando wakati wa maadhimisho ya Siku
ya UkimwiDuniani katika makao makuu ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Bi.Mbando
alisema huku suala la maambukuzi ya VVU / Ukimwi yakiwa yanaongezeka,
ni muhimu kwa kampuni na taasisi kuchukua hatua ya kujua hali ya afya za
wafanyakazi wake akisema kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kutekeleza
harakati na mpango wa serikali wa mapambano dhidi ya Ukimwi.
Alisema
Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kutokomeza ugonjwa huo na
kusema kuwa kwa 'kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya
Ukimwi ya " kufikia asilimia sifuri katika maambukizi mapya,unyanyapaa
na idadi ya vifo vinavyotokana na Ukimwi, inaonyesha kwamba juhudi zaidi
zimeelekezwa kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Mbando
aliipongeza TBL kwa kuweka mbele suala la afya ya wafanyakazi wake na
kutoa wito kwa kampuni na taasisi nyingine kuiga mfano huo, kwani kwa
kufanya hivyo kutapunguza kwa kiasi kiwango kikubwa cha maambukizi
mapya.
Kwa
upande wake, Meneja Rasilimali wa TBL, David Magesa alisema tokea mwaka
1990, kampuni hiyo ilikuwa na mpango ambao unawawezesha kupata huduma
ya upimaji wa hiari na Ushauri nasaha.
Magesa
alisema pia hadi sasa asilimia 80 ya wafanyakazi wa TBL wanajua hali ya
afya zao, akibainisha kuwa mpango huu unafanyika kutokana na kuungwa
mkono na utawala wa kampuni hiyo.
"Mbali
na upimaji wa hiari na Ushauri nasaha, kampuni kupitia kliniki yake
ambayo imejitosheleza inatoa bure dawa za kurefusha maisha (ARVs) na
mpango huo pia unashirikisha zaidi ya asilimia 40 ya wanafamilia wa
wafanyakazi," alisema.
Aidha,
Magesa alisema kupitia programu hiyo wameweza kupunguza idadi ya vifo
kwa asilimia 99.9 pamoja na kupunguza kesi za maambukizi ya magonjwa ya
zinaa (STDs) na kuongezea kuwa programu hiyo imekuwa ya manufaa makubwa
si tu klwa wafanyakazi bali hata wasio wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mbali
na hayo alisema kuwa kampuni hiyo hadi sasa ina waelimishaji rika 116
ambao wanashiriki katika kutoa ushauri kwa wafanyakazi wenzao ili
kuwafanya wawe na ufahamu katika kutambua umuhimu wa kujua hali ya afya
zao.
No comments:
Post a Comment