Posted: 02 Dec 2013 10:38 PM PST
Watu
wawili akiwemo mlinzi wa nyumba moja mkoani Tanga, wamehukumumiwa
kifungo cha miaka 20 gerezani kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya
kupakua na kuhifadhi meno ya tembo 114 yenye thamani ya sh. milioni
44,044 kinyume cha sheria, anaripoti Mashaka Mhando, Tanga.
Washtakiwa
hao ni Bw. Joseph Mwarabu na Bw. Richard Abdallah, ambapo hukumu hiyo
ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tanga, Mairasaanane
Kashonde.
Hakimu
Kashonde alisema, washtakiwa walitiwa hatiani chini ya Sheria ya
Uhifadhi ya Wanyamapori kifungu cha 86 (i), (ii) C na Kifungu 14 D, cha
sheria ya uhujumu uchumi sura 200 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma
hukumu hiyo, alisema washtakiwa hao walishiriki kushusha meno hayo
kutoka kwenye gari la jeshi na kuyahifadhi kwenye nyumba ambayo haikuwa
mali yao.
“Mah
a k ama ime s h in dwa kumhusisha mmiliki wa nyumba hiyo, Bw. Michael
Kijangwa ambaye wakati huo hakuwepo, hivyo mshtakiwa wa kwanza na pili
mnatiwa hatiani kwa kuhusika kikamilifu katika tukio hili,” alisema.
Kwa
upande wake, Mwanasheria wa Serikali, Veridiana Mlenza akiwa na
mwenzake Sabrina Joshi, waliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa
washtakiwa kwani matukio ya watu kukutwa na meno hayo yamekuwa
yakiongezeka.
“Ni vyema mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine kutokana na ongezeko la vitendo hivi,” walisema.
Washtakiwa
hao walipotakiwa kujitetea, kila mmoja aliiomba mahakama isiwape adhabu
kali kwani wana familia ambazo zinawategemea.
Hakimu
Kashonde alisema kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori, inatoa fursa kwa
hakimu kutoza faini mara kumi ya thamani ya nyara inayokamatwa kwa
mshtakiwa lakini aliwahukumu kifungo hicho iwe fundisho kwa wengine.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari Mosi 2010, katika Mtaa wa
Chumbageni, kwenye nyumba inayomilikiwa na Bw. Kijangwa na walikutwa
wakiwa na vipande hivyo.
Shtaka
la pili ambalo lilikuwa likiwakabili washtakiwa hao, inadaiwa Desemba
31, 2009, huko Chumbageni, walishindwa kutoa taarifa juu ya uwepo wa
nyara za serikali kwenye nyumba ambayo walikuwa wakifanya kazi.
Hata
hivyo, washtakiwa hao walikana na kudai meno hayo hayakuwa ya kwao bali
ya bosi wao Bw. Kijangwa ambaye kwa wakati huo alikuwa Lushoto na
familia yake ambako walikwenda kula sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Inadaiwa
meno hayo yalipelekwa katika nyumba hiyo iliyopo jirani na Hospitali ya
Tumaini, eneo la Chumbageni na gari la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) na maofisa wawili Desemba 31, 2009.
No comments:
Post a Comment