Posted: 02 Dec 2013 10:33 PM PST
Waziri
Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa (mwenye suti),akiwaaga waumini wa
Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mtandi,Wilaya ya Masasi,mkoani
Mtwara,baada ya kuendesha harambee ya kuchangia shughuli za maendeleo ya
Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKU),mwishoni mwa wiki ambapo
sh.milioni 103 zilichangwa katika harambee hiyo. Kulia kwake ni Askofu
wa Kanisa hilo,Dayosisi ya Newala,Oscar Mnung'a.
ACHANGISHA MILIONI 103/-,AMMWAGIA SIFA MKAPA
Na Mwandishi Wetu, Masasi
Waziri
Mkuu aliyejiuzulu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa,
amesema yuko tayari kushirikiana na mtu yeyote katika mapambano ya
kuondoa umaskini kwenye jamii.
Bw.
Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Mjini Masasi mkoani Mtwara,
katika harambee iliyofanyika kwenye Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya
Masasi, mkoani humo.
Harambee
hiyo ilikuwa na lengo la kuchangia shughuli za maendeleo za Ushirika wa
Mama wa Kikristo (UMAKI) na kusisitiza kuwa, yeye ni mdau wa mapambano
hayo.
“Mtu
yeyote anayepambana kuondoa umaskini katika jamii, niko tayari
kushirikiana naye katika harambee za harakati hizi,” alisema Bw. Lowassa
na kuongeza kuwa, wanawake ni jamii inayochukia sana suala zima la
umaskini.
“Wanawake
ni wadau wakubwa wa kupambana na umaskini ndiyo maana chama changu CCM,
katika rasimu ya Katiba Mpya inataka kuwe na asilimia 50 kwa 50 ya
uwakilishi bungeni kati ya wanawake na wanaume kwa sababu kinawapenda,”
alisema.
Alisema
kwa sababu hiyo, ndiyo maana ameridhia kushiriki harambee hiyo ambapo
kufika kwake kanisani hapo kumetokana na Wilaya hiyo kutoa kiongozi
makini, mwadilifu na shupavu mkubwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw.
Benjamin Mkapa.
“Hapa
pana historia ya kutoa kiongozi aliyeiongoza nchi yetu kwa uadilifu na
umakini mkubwa, walikuwepo watu waliyojaribu kumsema sema katika vyombo
vya habari.
“Mwisho
wa siku watu hao wamekiri kuwa Bw. Mkapa alikuwa kiongozio makini,”
alisema Bw. Lowassa ambaye wakati kiongozi huyo akiwa madarakani,
alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano
kabla ya kupelekwa Wizara ya Maji na Mifugo.
Katika
harambee hiyo, zaidi ya sh. milioni 103 zilipatikana ambapo Bw. Lowassa
na marafiki zake alichangia sh. milioni 10 na kuvuka lengo ambalo
lilikuwa sh. milioni 100.
No comments:
Post a Comment