Mpango wa Fedha kutoka TASAF wawanufaisha wakazi wa Kongwe Kiona
Diwani
wa kata ya kamange, Husein Juma Hading’oka akielezea jambo kwa
wanakijiji wa Kongwe Kiona pamoja na Wanahabari , tarehe 13 Decemba,
2013, wakati walipotembelea kijiji cha Kongwe Kiona, ambapo baadhi ya
Kaya zimenufaika na Mpango wa Uhawilishaji Fedha kwa Maendeleo Endelevu
ya Kaya, Mpango huu unalenga kunusuru kaya maskini, kwa kutoa ruzuku
kwa kaya maskini sana ili ziweze kupata huduma za elimu na afya.
Baadhi
ya waandishi wa habari na wahariri wakiwa pamoja na wanakijiji wa
Kongwe Kiona wakimsikiliza Afisa Mtendaji wa kata ya Kamange, Suleiman
Jumanne(hayupo pichani) akisoma taarifa fupi, kuhusu manufaa ya mpango
wa Uhawilishaji Fedha kwa wakazi wa kijiji cha Kongwe Kiona.
Wanakijiji wa Kongwe Kiona wakimsikiliza Diwani wa kata ya kamange, Husein Juma Hading’oka (hayupo pichani).
Mkazi
wa Kijiji cha Kongwe Kiona, Sufiani Juma Sungura akitoa ushuhuda wa
jinsi alivyo nufaika na Mpango wa Uhawilishaji Fedha, kutoka Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF), Kupitia Mpango huu Ndugu Sungura ameweza
kuezeka nyumba yake kwa bati pamoja na kuweza kujikimu dhidi ya njaa kwa
kuhifadhi mazao ya chakula.
Mkazi
wa Kijiji cha Kongwe Kiona, Bi. Khadija Said Sengwira, akieleza ni kwa
kiasi gani mpango wa Uhawilishaji Fedha kutoka Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF),umebadili maisha yake, nasasa ni mfugaji wa bata wa
biashara.
Mkazi
wa Kijiji cha Kongwe Kiona, Said Juma Kwavi akionesha Magunia ya
Mahindi aliyoweza kuzalisha na kuhifadhi baada ya kunufaika na Mpango wa
Uhawilishaji Fedha, kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF), Zuhura Mdungi akifafanua jambo kwa Wanahabari,
tarehe 13 Decemba, 2013, wakati walipotembelea kijiji cha Kongwe Kiona,
ambapo baadhi ya Kaya zimenufaika na Mpango wa Uhawilishaji Fedha kwa
Maendeleo Endelevu ya Kaya, Mpango huu unalenga kunusuru kaya maskini,
kwa kutoa ruzuku kwa kaya maskini sana ili ziweze kupata huduma za elimu
na afya. Kwasasa Mpango huu unatekelezwa katika Kaya za wilaya tatu za
Mkoa wa Pwani ikiwemo Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment