Posted: 02 Dec 2013 10:58 PM PST
- NI WAKATI WA KUIVAA BURUNDI CHALLENGE
Na Mwandishi Wetu, Nairobi
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen
alisema kwamba kuwasili katika kikosi chake kwa wachezaji Thomas
Ulimwengu na Mbwana Samatta kungeongeza nguvu katika kikosi hicho hasa
katika mchezo wao wa Kombe la Challenji dhidi ya Burundi
Samatta
na Ulimwengu waliwasili jijini Nairobi wakitokea kuichezea timu yao, TP
Mazembe ya DRC katika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambayo
walifungwa jumla ya mabao 3-2 na timu ya CS Sfaxien ya Tunisia na hivyo
kukosa kombe.
Akizungumza
jijini Nairobi, Kim alisema ujio wa wachezaji hao ingekuwa ni ahueni katika
kikosi chake ambacho bado kilikuwa kinakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Burundi
kwani aliiona timu hiyo na aliipa matumaini katika kuleta upinzani mkali.
"Wachezaji
niliokuwa nao walikuwa ni wazuri lakini kuongezeka kwa Samatta na Ulimwengu pia
kuliongeza nguvu zaidi katika kikosi changu, hivyo nilitegemea mechi ya
Jumatano ingekuwa nzuri zaidi," alisema kocha huyo.
Alisema
timu zote zilizoshiriki michuano hiyo hakuna timu kibonde, hivyo hata
walipovuka robo fainali bado walikuwa na kazi ngumu katika kuhakikisha
wanatwaa kombe hilo na kurudi nalo Tanzania.
Kim
alisema kuna kila sababu za kuboresha kikosi chake, kwani kuna
mapungufu ambayo aliyagundua walipocheza na Somalia, hivyo anatakiwa
kuyafanyia kazi haraka kabla ya michuano m ingine kuja.
No comments:
Post a Comment