Posted: 02 Dec 2013 10:35 PM PST
Waziri
wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, amesema ataendelea kusimamia sheria ya
barabara namba 30 ya mwaka 1973 hadi anaingia kaburini kwa kuhakikisha
hakuna magari ambayo yanazidisha uzito na kuharibu barabara, anaripoti Goodluck Hongo.
Dkt.
Magufuli aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika hafla ya kutilia
saini mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara za Dodoma- Manyara inayopita
Mayamaya- Babati-Bonga.
Barabara
nyingine ni Tunduru- M a n g a k a - Mtambaswala na kusema kuwa,
barabara hizo z i n a j e n gwa kwa gharama kubwa hivyo watendaji wote
wa Wizara ya Ujenzi kupitia
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wanapaswa kusimamia sheria.
Alisema
usimamizi makini wa sheria za barabara, utasaidia kuzifanya zidumu
zaidi kwani Rais Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara hiyo kusimamia sheria
ambapo kitendo cha wamiliki wa magari kuzidisha uzito, kinamchukiza
sana.
“Sipo
tayari kuona matajiri wachache wakiharibu barabara na kujipatia faida
kubwa wakati barabara hizi zinajengwa kwa mkopo unaolipwa na kodi za
wananchi.
“Msema
kweli ni mpenzi wa Mungu, mimi nitaendelea kusimamia sheria hadi
naingia kaburini kwa kuhakikisha hakuna magari yanayozidisha uzito na
kuharibu barabara,” alisema Dkt. Magufuli.
Aliongeza
kuwa, kama matajiri hao wataachiwa waendelee kuzidisha uzito, barabara
zilizopo hazitadumu kwa muda mrefu na wananchi maskini wataendelea
kulipa kodi.
“Nchini
Ujerumani, uzito wa magari yote ni tani 40, Uingereza tani 40, Ufaransa
40, Urusi 38 lakini Tanzania tani 56, wakati mwingine tunakamata hadi
tani 96,” alisema.
Akiwazungumzia
wakandarasi waliochukua zabuni ya ujenzi wa barabara hizo, Dkt.
Magufuli aliwaonya na kusisitiza kama hawawezi kazi ni bora wasisaini
mikataba hiyo ili watafute wakandarasi wengine wenye uwezo.
Alisema
kama wamekubali kusaini, wanapaswa kuanza kazi mara moja kwani Serikali
ndio iliyokopa na walipakodi ni Watanzania hivyo si kukaa miezi sita
ndio waanze kazi.
“Mameneja
wa TANROADS katika mikoa ambayo miradi hii inafanyika, lazima msimamie
kikamilifu ujenzi huu na kama mradi ukisuasua katika eneo lako ujue
hutufai kufanya kazi hivyo uondoke mara moja,” alisema.
Kwa
upande wake, mbunge wa Kasulu Mjini, mkoani Kigoma, Bw. Moses Machali
(NCCR-Mageuzi), aliipongeza Serikali kwa kusikia kilio cha wananchi na
kuwajengea barabara na daraja la Mto Malagarasi ambapo yeye si
mhafidhina; bali kama serikali imefanya mema inapaswa kupongezwa.
“Jema
ni jema tu hata kama likifanywa na nani hivyo mimi si mhafidhina, kama
Serikali imefanya mema basi inapaswa kupongezwa,” alisema.
Aliongeza
kuwa, licha ya Serikali kuwajengea Daraja la Mto Malagarasi, bado
barabara zingine ikiwemo ya Nyakanazi ina hali mbaya, hivyo pamoja na
kuipongeza serikali kwa kusaini mikataba hiyo, utekelezwaji wake ni
jambo lingine.
“Kusaini
mkataba ni jambo moja na Mkandarasi kufika eneo la mradi ni hatua
nyingine, Daraja la Mto Malagarasi halitoshi bali tunaomba Barabara ya
Nyakanazi nayo iwekwe lami,” alisema.
Naye
Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dodoma kwa tiketi ya Chama cha Wananchi
(CUF), Bi. Moza Abeid Said, alisema anaipongeza serikali ya CCM kwa
kutekeleza ahadi zake, lakini zisifanywe karibu na uchaguzi kwani kilio
cha barabara hizo ni cha muda mrefu.
Alisema
ingawa yeye ni Mbunge kutoka upinzani, anaipongeza Serikali hasa
inapotatua kero za wananchi bali wasiwasi mkubwa ni utekelezaji wake
kwani wabunge wamekuwa wakilalamikia miradi mingi ambayo imesainiwa
lakini haijatekelezwa.
“Waziri
Magufuli ameweza kutekeleza ilani ya CCM katika sekta ya miundombinu ya
barabara... amefanya kazi nzuri, barabara ya Babati-Iringa ikijengwa
kama walivyosaini mikataba, itawasaidia sana wananchi wa Mkoa wa
Dodoma,” alisema.
Naye
Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, alisema mradi huo
unatekelezwa kwa awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza ulitekelezwa kwa
mkopo wa sh. bilioni 472 na awamu ya utatekelezwa kwa gharama ya sh.
bilioni 538.88.
Alisema
fedha zimetoka katika Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na nyingine
kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambapo fedha nyingine zimetoka
serikalini. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wabunge wote kutoka mikoa ya
Manyara, Dodoma, Mtwara na Ruvuma ambao miradi hiyo inapita katika
majimbo yao.
No comments:
Post a Comment