Zilikuwa ni ndoto za alfajiri wakati
nilipostuka kutoka usingizini, nikagundua kwamba nilitoka kwenye lindi la
mawazo mazito(ndoto) ambazo zilinionyesha jinsi viumbe walivyoweza kubarikiwa
na mungu kuishi wawili wawili, hapo hapo niliinuka haraka hadi bafuni ambapo
niliweza kujimwagia maji kasha nilivaa nguo kwa ajili ya kwenda kanisani.
Kwa upande wa Regina yeye ilikuwa ni
tofauti baada ya kuwa ametoka kwenye viwanja vya michezo yetu ya kikapu maeneo
ya Tanesco drive in opposite na jingo la drive in Cinema(Ubalozi wa Marekani),
alikuwa amechanganyikiwa kutokana na kauli zangu kwake siku hiyo, ambapo
aliondoka bila furaha kuelekea nyumbani kwake mikocheni maeneo ya mlalakuwa
katika nyumba za watu matajiri, akiwa na gari aina ya rand lover discover,
akuweza kufika nyumbani salama baada ya kupata ajali mbaya ambayo hata hivyo ni
gari pekee iliyoweza kuharibika huku yeye akitoka mzima bila jeraha lolote.
Maisha yaliendelea tena kama kawaida
ambapo siku iliyofuata mimi kama kawaida yangu siku za jumatatu hadi ijumaa uwa
ni lazima kufanya mazoezi asubuhi na jioni, hivyo nilikwenda mazoezi ya mpira
wa miguu, ambapo niliamka mapema sana ili kuwahi kwenda kwenye miangaiko yangu
ya kila siku motto wa mlala hoi, nakumbuka nilikuwa nasoma huku nafanya kazi za
vibarua mbali mbali kwenye viwanda na mida ya jioni nilipendelea kwenda kwenye
viwanja vya michezo ili kutimiza ndoto yangu ya kucheza basketball(mpira wa
kikapu).
Jambo moja kubwa tulilokuwa nalo kwa
kila mmoja wetu, yaani mimi na Regina ni ushawishi wa kuweza kusikilizwa na
watu, na mara zote alipokuwa amesimama regina basi utakuta amejaliwa na vijana
wakiendelea kumsikiliza , naye bila ajizi alikuwa akipenda sana kuwapa michapo
mbali mbali za hapa na pale ikiwemo stori za soka la majuu, zaidi ikiwa ni ligi
ya uingereza na mchezo wa kikapu nchini marekani, maana nakumbuka wakati huo
bado kulikuwa na uhaba wa vyombo vya habari hivyo wenye pesa ndiyo waliokuwa
wakitazama zaidi mambo ya kwenye mitandao na hata tv pia walikuwa nazo
wachache.
Baada ya kufika uwanjani muda huo
nikitokea kwenye viwanja vya mchezo wa soka ili niende kucheza kikapu, na
nilipofika uwanjani taa za uwanja zilikuwa zimezima kutokana na itilafu ya
umeme, hivyo siku hiyo hakukuwa na mazoezi zaidi ya kupiga stori na wakati huo
tayari regina alikuwa bize kuwapa michapo, ndipo mimi baada ya kuwasili eneo
hilo maana sikuwa na tabia ya kwenda kujichanganya sehemu alipokuwa regina,
nilikuwa na tabia ya kukaa sehemu ingine
ili kumpa uhuru wake na pia sikupenda kujichanganya kuwa mmoja wa wasikilizaji
wake au wapambe wake.
Lakini jambo kubwa nililokuwa pia
likimuumiza kicha ni pale ambapo alikuwa akishindwa kuelewa jambo hili, nikiwa
sipo uwanjani alikuwa akisikilizwa yeye wakati wote lakini mara nilipokuwa
nikiwasili maeneo hayo vijana wengi walikuwa na tabia pia ya kuja kwangu
kunisikiliza, maana nakumbuka nilikuwa na vipaji vingi sana, wakati huo
nilicheza mpira wa migu katika timu ya taifa ya vijana wenye umri wa miaka
chini ya 23, lakini pia nilikuwa naigiza filamu ya Oparation ya hatari,
iliyokuwa gumzo kwa wakati huo, mtunzi wake akiwa ni nyakasagani masenza,
mtunzi maarufu sana wa adithi natamthilia
za cinema.
Ilibidi
niamaki baada ya kuona vijana wote wametoka kwa regina ambaye alikuwa anawapa
michapo na sasa wameamia kwangu, moyoni nilitamani waendelee kumsikiliza yeye,
lakini aikuwa hivyo waliweza kumwacha mpweke, kitendo ambacho mimi hakikuwa
kikinifurahisha, alibaki peke yake eneo alilokuwa akiwasimulia vijana habari
zake, na kwa kuwa mafahari wawili hawakai zizi moja yeye pia hakuwa na desturi
ya kuja eneo nililokuwapo, ni kama tulikuwa na tabia zinazofanana kimatendo,
hivyo aliishia kunitazama tu hadi ilipofika wakati wa kuondoka maeneo hayo ya
viwanja.
Kwa kuwa siku hiyo hakukuwa na umeme,
nilipata fulsa nzuri ya kuweza kumtokea bint rafiki yake regina Edna, kwa kweli
alikuwa ni dada mrembo ambaye pia alikuwa amebarikiwa kuwa mchezaji hodari sana
wa mchezo huo, na katika timu ya pazi qeen yeye na regina ndiyo waliokuwa
wachezaji wakali kutokana na kuufahamu vyema mchezo huo wa kimarekani, wengine
walikuwapo kwa upande wa timu ya wadada lakini hawakuwa wakicheza lama hawa,
naweza kusema kwamba walikuwa wakijifunza zaidi katika kuutambua mchezo huo
chini ya kocha mzoefu wa siku nyingi Kalemaa mkongo aliyebobea Tanzania katika
fani ya ufundishaji wa mchezo wa kikapu, na alifanikiwa kuinua vipaji vingi kwa
upande wa timu ya wavulana na wasichana.
Baada ya kufanya mazungumzo ya kina
na Edna dauson, akusita kunikatalia wazi wazi kwa madai yake, ambapo aliweza
kunieleza juu ya upendo aliokuwa nao dada yake kwangu, edna alinieleza vitu
vingi sana kuhusu regina na azima yake kwangu, kwamba asitaili kuwa mpenzi wangu
kwa kuwa yupo ambaye alikuwa akinitamani usiku na mchana, ambaye ni regina,
“dada yangu anakupenda sana shaaban, na sijui kama unatambua hilo, si unamuona
mwenyewe amefikia umri wa kuwa na mume, sasa wewe kwa nini usipeleke barua ya
kwenda kuchumbia? Au utaki awe mke wako, niambie shaaban, na ikitokea akakuta
umesimama na mimi hapa sijui nitambebea mbeleko gani, tafadhali nakuomba sana
usije ukanigombanisha na rafiki yangu, wewe ukitaka mfuate yeye mweleze maana
yupo na anakuzungumzia kila siku, na hata ujio wake hapa siku hizi ni kwa ajili
yako, nadhani umenielewa shaaban” alimaliza edna nikabaki nimeduwaa sina jibu.
Ilikuwa ni siku ya jumatano
nilipopigiwa simu kupewa taarifa ya kwenda kujiunga na timu ya mpira wa miguu
iliyokuwa ikishiriki ligi kuu ya Tanzania, wakati huo ikijulikana kama safari
lager, nilitakiwa kwenda kwenye majaribio mjini Dodoma kujiunga na timu ya CDA watoto
wa nyumbani, hivyo sikuwa na njia ingine zaidi ya kuondoka jijini dare s salaam
kuelekea Dodoma kwa ajili ya kufanya majaribio nakumbuka ulikuwa mwezi wa kumi
baada ya kuwa ligi kuu imemalizika na wakati huo timu zote za ligi kuu zilikuwa
katika maandalizi ya kufanya usajiliwa wachezaji.
Sikuwa na mawasiliano ya moja kwa
moja na regina, maana tulikuwa hatujazoeana na wote kila mmoja alikuwa ni
fahari kwa mwenzie, kwa tabia yangu ya kutopenda kujipendekeza kwa mtu au
kunyenyekea kwa watu wenye pesa, sikuwahi kuwa mtumwa wa aina hiyo, niliamini
nab ado naamini kwamba maisha siyo pesa, unaweza kuwa na pesa lakini ukawa
hauna afya nzuri, kikubwa mimi niliamini kwamba maisha ni kumtumainia mungu
pekee, hivyo niliishi Dodoma kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye hoteli ya jambo
lee.
Nilirejea dare salaam baada ya mwaka
mmoja, na kwa kipindi hicho chote sikuweza tena kuwasiliana ama kukutana na
regina, sikuwa nimemuweka sana moyoni kwa wakati huo kutokana na kwamba yeye
alionekana kuwa na umri mkubwa sana, na hata maelezo ya edna pia niliyasikiliza
lakini sikumpa majawabu zaidi ya kubaki natafakari juu ya maelezo aliyokuwa
ameniwasilishia edna.
Baada ya mwaka mmoja kupita nilirejea tena
kwenye makazi yangu maeneo hayo ya drive in, nakumbuka nilirudi majira ya saa
za jioni na kupitia maeneo hayo ya viwanja vya wazi drive in tanesco, na kwa
bahati nzuri siku hiyo kulikuwa na watu (vijana wengi) waliokuwa wamekwenda
kufanya mazoezi na wengine kuangalia, mara baada ya kuniona ilikuwa kama
shangwe maana vijana kutokana na kutoniona kwa kipindi cha mwaka mmoja, wengi
walikuwa na hamu sana ya kuniona na hakika walikuwa wamemisi sana habari na dondoo
za stori nilizokuwa nikiwapa, ghafla nilijikuta nimezungukwa na kundi la vijana
wengi walipenda kuniita kaka shaaban, “kaka shaaban karibu sana,yaani
tumekumisi sana kaka yetu, ilikuwa ni
kauli ya Kelvin ambaye tuliishi nyumba jirani, nilipenda sana kuwa naye karibu
katika kumfundisha mambo mbali mbali, asante mdogo wangu nimerudi tena kwa hiyo
tuko pamoja, nawaomba nifike nyumbani kwanza niweke mizigo yangu kisha
nitarejea tena, niliwaacha vijana wengi na shahuku kubwa ya kuningoja nirudi,
nawakumbuka kina Eric Mwingizi, Dotto, Gwantwa Mwasakyeni pamoja na wengine
wengi akiwepo mdogo wangu(Milobo Mkama) ambaye ni afrikast yaani chotara wa
kizungu niliyekuwa nikiishi naye nyumba moja.
Ni siku ya jumamosi ilikuwa wakati
nimeamka asubuhi nikiwa na uchovu wa safari
pamoja na uchovu wa mzunguko wa muda wa mwaka na timu ya CDA ya Dodoma
watoto wa nyumbani, kwa kuwa niliitaji kupumzika zaidi siku hiyo sikuweza
kuamka asubuhi kama inavyokuwa kwa siku zingine, nilihisi uchovu sana hivyo
niliamua kupumzika tu kusubiri kwenda kuangalia na kujifunza kucheza mpira wa
kikapu, na kama unavyojua tena mchezo wa kikapu ni mchezo wa watu wastarabu
ambao hawapendi kuchafuka, na sifa yao kubwa ni kwamba utofauti uliopo kati ya
wacheza soka na wacheza kikapu ni jinsi ya miili yao, wacheza soka wao misuli
yao imekakamaa sana, kutokana na kufanya mazoezi sana wakati wa jua kali, huku
wacheza kikapu wao misuli yao iko laini kutokana na kufanya mazoezi muda mwingi
wakati wa usiku ama eneo ambalo jua limepungua hivyo wanaonekana laini hata
kama misuli yao imejengeka, lakini uwezi kulinganisha na wacheza soka.
Niliamka majira ya saa nne, nikaenda
kujimwagia maji, kasha niliweza kunywa chain a wadogo zangu, Aghata, emele, joo
na jovi mkama ambao kwa wakati huo walikuwa ni wadogo na walinipenda sana,
hivyo muda mwingi walifurahi kutembea na mimi na hata wakati mwingi pia
niliweza kwenda nao maeneo hayo ya uwanja nikiwa pia na binamu yangu mzungu
Eugen.
Kati ya vitu ninavyovipenda sana ni
ufugaji wa wanyama, hivyo nilikuwa na mifugo hapo nyumba (Mbuzi) ambao sikuona
aibu kuwatoa na kwenda kuwafunga kwa ajili ya kupata chakula, na wakati
mwingine nilipenda kwenda kuwafunga pembezoni mwa viwanja vya kikapu vilivyopo
ndani ya makazi yetu, hiyo ilikuwa ni tabia yangu ya kila siku kuwakumbuka
mbuzi wangu kwenda kuwatafutia maeneo ambayo wangeweza kupata majani mazuri.
Shaaban mpalule, iliita sauti kutoka
kwa rafiki yangu Aluta Warioba, na mimi niliitika, bwana mkubwa, nikiwa
namaanisha ni heshima ambayo utolewa na watu waliopo Gerezani wakiwa na maana
ya kuwapa heshima askari magereza na heshima hiyo ilikuwa kama imekuwa ni tabia
kwa rafiki zangu, na hiyo ilitokana na mimi mwenyewe kuwa niliwahi kuishi
gerezani wakati nilipokwenda kufanya utafiti kuchunguza vifo vya mahabusu
vilivyokuwa vikiendelea ndani ya gereza hilo.
Wakati huo tulikuwa kwenye viwanja hivyo na muda huo tayari wachezaji
wengi walikuwa wameshafika eneo hilo akiwepo Regina wakiendelea na mazoezi kama
kawaida ya siku za mazoezi viwanjani hapo.
Usikose kufuatilia Adithi hii kila siku 0713869133/0767869133
No comments:
Post a Comment