Muogeleaji
nyota wa kiume wa Tanzania, Hilal Hilal (wa kwanza kulia) akiwa kwenye
jukwaa mara baada ya kupokea medali yake ya Shaba katika mashindano ya
Kanda ya Nne ya Cana.
Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania kinanchoshiriki katika mashindano ya Cana
Kanda ya nne. kutoka kulia ni Amani Doggart, Catherine Mason, Hilal
Hilal na Smriti Gokarn.
Na Mwandishi wetu
Muogeleaji
wa Tanzania, Hilal Hilal ametwaa medali ya Shaba katika mashindano ya
kuogea ya Cana Kanda ya Nne yanayoendelea nchini Mauritius.
Hilal
ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa katika mchezo huo, amemaliza katika
nafasi ya tatu katika staili ya butterfly kwa kutumia muda wa sekunde
26.70 katika mashindano hayo magumu yaliyoshirikisha nchi za Uganda,
Kenya, Rwanda Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Sudani
Kusini na Sudan.
No comments:
Post a Comment