Mkononi alishika funguo za gari aina
ya Land Rover(free Rander) ya kisasa kabisa, alikuwa ni Christopher aliyekuja
kunikabidhi siku hiyo wakati tukiwa kwenye Msiba wa Mwenzetu patric Nyembela
aliyekuwa amefiwa na kaka yake maeneo ya Mwananyara, “shika hizi funguo amenipa
dada Regina” alisema Chriss wakati huo nikiendelea kumtazama Chriss ambaye alikuwa
akinikabidhi funguo za gari,
“asante chriss
nilisema huku nikijaribu kupepesa macho yangu
na moja kwa yaliweza kugongana na macho ya Regina ambaye kwa wakati huo alikuwa
akishuhudia tukio kwa mbali huku akiwa ameketi kati kati ya wanawake wenziwe kwenye
mkeka wakati huo” wakati huo macho ya Regina yalikuwa makali sana kutokana na
sikuwa tayari kupokea hizo funguo kwa chriss.
“chukua ilikuwa ni sauti ya Regina,
wakati huo pia nilikuwa na wenzangu vijana, wengi na miongoni mwao alikuwa ni
Aluta Warioba ambaye alinisisitiza kuchukua zile funguo, nilizipokea kisha
akasema niliondoe lilipokuwa limeegeshwa gari hilo, lakini kutokana na kwamba
sikuwa na ujuzi wa kuendesha gari, sikuweza ilibidi nimuombe tena Aluta aweze
kunisaidia kuliondoa mahala hapo na kuliweka pembeni kasha aliponirejeshea
funguo nilimuomba na mimi tena kwa upendo Chriss amrudishie Regina funguo zile
kwa kuwa sikuwa tayari kuendesha gari kutokana na kwamba sikuwa mjuzi wa
kuendesha.
“nakupatia funguo za gari utaki kwa
nini”?
‘’hapana, siku ingine Regina nilimwambia, umenikwaza sana Shaaban
alisema “ najua ila kuna sababu ndiyo maana nimefanya hivyo, pole ila jisikie
tu huru, waala hakuna tatizo nilimwambia, alionekana kutabasamu maana mwanzo
alionekana kama kachukizwa sana na kitendo kile, na baada ya hapo alitoa wito
wa kuwapa chakula watu wote waliokuwa kwenye msiba wakati huo, ambapo aliwaomba
tuongozane kwenda kupata chipsi kuku ama niseme kila mtu apendacho maeneo
maarufu sana kwa hapa jijini Americani chipsi na wote tukaelekea maeneo hayo.
Baada ya kufika kila mmoja
alielekezwa utaratibu wa chakula kwamba anaweza kuagiza kile apendacho, sikuwa
tayari kuagiza kutokana na mimi sipendi kula kula sana, na tabia hiyo hata
nyumbani uwashangaza sana ndugu na familia yangu, hivyo baada ya watu wote kuagiza
nilibaki mimi ambaye nilikuwa sijaagiza chakula, lakini alipogundua aliniuliza
kwa nini sikuagiza chakula nilimjibu kwamba nimeshiba,
“hapana shaaban inabidi
ule pia, hivyo ilibidi awaite wahudumu kuja kunisikiliza na mimi ilibidi
niagize tu pamoja na kwamba nilikuwa nimeshiba, nilimuomba mhudumu
anitengenezee chipsi mayai pekee, maana sikuwa na sehemu ya kukiifadhi kile
chakula tumboni mwangu, kilipoletwa nilikula kidogo wakati huo akinishuhudia na
kwa kuwa alikuwa yupo na wanawake wenzio na tulikuwa kwenye msiba baada ya
kuona nimeanza kula aliondoka kuungana na wenziwe na mimi nikibaki kwenye kundi
la wenzangu vijana tukiendelea kubadilishana mawazo na kuzungumza masuala mbali
mbali ususani vichekesho na masuala ya michezo.
Baada ya tukio hilo wote tulirejea
tena kwenye msiba pale ambapo wengi walikuwa wameacha magari yao akiwepo yeye
maana kutoka eneo la msiba hadi americani chipsi aikuwa mbali, hivyo tulikwenda
kwa miguu, “baada ya kufika eneo la msiba tulikaa kwa muda wa nusu saa na
ilipotimia majira ya saa 5 tano za usiku kila mmoja sasa alikuwa tayari
kuondoka maana tulikaa zaidi ya masaa 6 pale kwenye msiba huo.
“baba naondoka alinifuata Regina na kuiaga na
mimi nikamtakia siku na safari njema usiku ule, na wakati yeye yeye akiondoka
name pia niliweza kuondoka na rafiki zangu kina Eric Mwingizi, Dotto Peter na
wengine wengi kuelekea maeneo ya Tanesco drive in kwa usafiri wa Eric mwingizi
na kuwaacha wengine kama kina Aluta Warioba, Wasira Nyerere,Abdul Kanali Misuli
tulizoea kumuita Abdul kutokana na jinsi misuli yake ilivyojengeka kwa mazoezi,
na Kalemaa wakiendelea kumfariji Patric
Nyembela usiku ule na watu wengine waliendelea kuwepo hadi kesho yake.
Tukio hilo la msiba lilitufanya tena
kutoonana kwa kipindi cha wiki nzima ambapo wengi walishinda katika msiba
kutokana na Patric alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa kutumainiwa wa pazi
hivyo ilikuwa ni heshima ya pekee kusubiri kwa muda bila kukutana ama bila
wachezaji kufika uwanjani, hivyo hata mimi sikuwa tayari kwenda uwanjani pamoja
na kwamba niliishi maeneo hayo ya uwanja zaidi tulikuwa tukipishana kwenye
msiba, nikifika naambiwa Regina kaondoka lakini baada ya Wiki kumalizika maisha
yaliendelea tena kama kawaida kwa kushiriki michezo yetu kama ilivyokuwa kwa
siku zote.
Usikose kufuatilia Adithi hii kila siku 0713869133/0767869133
No comments:
Post a Comment