Mmoja
ya majaji wa shindano la Airtel Trace Music Stars mtunzi wa nyimbo na
mwaimu wa Muziki Anthony Joseph Namata“JOETT (kulia) akitoa hoja kwa
jopo la majaji wenzake wakati wakichagua vijana waliofudhu kuingia kumi
bora katika wiki hii. Zoezi hili lilifanyika katika ofisi za makao makuu
ya Airtel Tanzania zilizoko Moroco jijini Dar es Saalam Jana. Pichani
ni mtengenezaji wa Muziki na mfanyabiashara Luciano Gadie Tsere
(katikati) na Lucy T. Ngongoseke, mratibu wa Airtel Trace Music Stars.
Washiriki 10 waingia ndani ya kumi bora ya wiki ya shindano la Airtel Trace Music Stars
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Leo imetangaza washiriki kumi bora
wa wiki wa shindano kubwa barani Afika lijulikanallo Airtel Trace Music
Stars lililolizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa pili na kuwapatia fursa
vijana kuonyesha vipaji vyao.
Kabla ya kutangaza washindi hao Jopo la majaji linaloshirikisha wasanii
na wataalamu wa muziki akiwemo mtangazaji wa TV mahiri, Mwanamuzi,
Mwigizaji na msanii aliyejikita katika maeneo mengi, Jokate Urban
Mwegelo, mtunzi wa nyimbo na mwaimu wa Muziki Anthony Joseph
Namata“JOETT pamoja na mtengenezaji wa Muziki na mfanyabiashara Luciano
Gadie Tsere likikaa mwishoni mwa wiki na kuchagua waimbaji 10 bora
kati ya vijana walioweza kushiriki mpaka sasa.
Akitangaza baadhi ya vijana waliioingia katika kumi bora , Jaji Anthony
Joseph Namata“JOETT alisema “moja kati ya vigezo vilivyotumika kuwapata
hawa walioingia kumi bora ni pamoja na uwezo wao wa kuimba pamoja na
sauti lakini pia idadi ya kura anazozipata kutoka kwa wasikilizaji.
Hivyo basi napenda kuchukua fulsa hii kutangaza vijana waliofanikiwa kuingia katika kumi bora ambao ni pamoja na Teddy Benedict
Code 55210241, Beny Sule Code 55210243, Eddy Zone (Jack) Code
55210245, Anneth Stanley Code 55210248, Sarah Code 55210249, Nicole
Grey Code 55210253, Yvone Masai Code 55210254, Adili Kwezi Code
55210115, Anneth Komba Code 552101256 , David Benson Mahenge Code 55210244”
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema
“Tunafurahi kuona vijana wengi wamejitokeza kushiriki na kuonyesha
vipaji vyao kwa mwaka huu, natoa wito kwa vijana kuendelea kushiriki
kwani mashindano bado yanaendelea.
Sambamba na hilo tunawaomba watanzania wawapigie kura washiriki
wanaowapenda pamoja na vijana hawa ili waweze kuendelea kutetea nafasi
zao na hatimae kuingia kwenye tano bora na kisha kupenya kwenye fainali
za kitaifa zitakazofanyika hapa jijini Dar es saalam mwishoni mwa mwezi
Mei”.
‘Ili kupiga kura kwa mshiriki unaempenda unatakiwa kupiga 0901002233 Kisha kuingiza code namba ya mshiriki au tuma SMS yenye code ya namba ya mshiriki kwenda namba 15594” aliongeza Mmbando.
Huu ni msimu wa pili wa Shindano la Airtel Trace Music Stars ambapo
sasa shindano hili lipo katika hatua kitaifa, fainali za taifa
zinategemea kufanyika 20 Mei 2016 ambapo mshindi wa kwanza atajishindia
shilingi million 50, pamoja na kupata nafasi ya kwenda kushiriki katika
mashindano ya taifa mwezi Juni Lagos nchini Nigeria. Mshindi wa pili
ataondoka na shilingi million 5 na watatu shilingi milioni 2 Ili
kushiriki piga namba 0901002233.rekodi wimbo wako sasa
No comments:
Post a Comment