TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 19, 2016
HADITHI: NDOA YA MTOTO WA TAJIRI BILIONEA NA MTOTO WA MASIKINI_MKULIMA SEHEMU YA TATU.
Ilikuwa ni siku ya mvua kubwa ambayo ilinyesha katika jiji la dare s salaam, hata kusababisha shuguli za maendeleo kusimama kutokana na serikali kutangaza mafuriko, yaliyosababisha barabara nyingi kujaa maji na kuwafanya madereva kushindwa kuvuka maeneo mbali mbali, na mara baada ya kupata taarifa hizo nilikuwa ni miongoni mwa Watu tuliokuwa katika pita pita kukagua maeneo ambayo yaliweza kuathilika ili kutoa taarifa kwa wahusika kuweza kutoa msaada wa haraka, ilisemekana mvua hiyo iliambatana na mvua ya mawe iliyoleta maafa kwenye baadhi ya maeneo ya bonde la mkwajuni na hata maeneo ya jangwani.
Taarifa mbali mbali kutoka kwenye vyombo vya habari ziliripoti kuhusiana na mvua hiyo hatari ambayo ilipelekea Serikali kutangaza hali ya hatari na kuwataka watu wote kuondoka sehemu zote za mabonde, hivyo ilibidi pia niweze kukimbia kwa anti yangu sehemu za mkwajuni ili kuona kama ameweza kunusurika, lakini baada ya kufika maeneo hayo nilikuta anti yangu nyumba yake na za jirani zimejaa maji kitendo cha wao kushindwa kuwepo ndani ya makazi hayo, hivyo nilianza zoezi la kumsaidia anti yangu kuamisha vyombo vilivyokuwa ndani ya maji kwa wakati huo, na kufanikiwa kulikamilisha zoezi hilo.
Nilikuwa ni miongoni mwa watu waliopeleka taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na hali, Sikuwa Mwanahabari lakini nilikuwa nikiipenda sana kazi ya habari, nilitumia pia fulsa hiyo kuishauri serikali kufanya mipango ya kuhakikisha itawatafutia maeneo ya kuishi watu waliopata majanga ya mafuriko kutokana na taarifa za mamlaka ya hali ya hewa kwamba mvua hiyo ilikuwa inaendelea kunyesha ambayo ingeweza kuja kuleta madhara makubwa.
Kwa upande mwingine kutokana na mvua ile hatukuweza tena kuwasiliana na Regina kwa kuwa hali ya hewa aikuwa nzuri, watu wengi walishinda majumbani mwao kwa kuofia usalama wao, na hata wachezaji pia walishindwa kufika viwanjani kutokana na mvua hizo zilizonyesha kwa zaidi ya wiki tatu.
Michezo mbali ilibidi kusimama kwa muda kutokana na zile mvua, kwa hiyo hata ligi kuu ya Safari Lager pia ilibidi kusimama kutokana na shamba la Bibi (Uwanja wa Uhuru) kuwa katika hali mbaya, na taarifa zilionyesha kwamba mvzile zilinyesha takribani mikoa yote ya Tanzania.
Niliumia sana Moyoni mwangu kutokana na hali niliyoikuta kule kwa anti yangu Mama Neema, ambaye hakika kwa zaidi ya wiki aliishi katika mazingira ya kujibanza kwa majiraniakiwa na watoto ambao ni wadogo zangu na mimi ndiye niliyekuwa na jukumu kwa wakati huo la kuwafuata kila siku kwa mama yao na kwenda nao kwa baba yao ambaye kwa wakati huo ndiye aliyekuwa mlezi wangu kama baba yangu.
lakini pia iliniwia ugumu sana kuwatoa mbuzi wangu kwenda kwenye malisho, pamoja na kwamba haikuwa tatizo kuwapeleka umbali mkubwa, lakini maeneo waliyokuwa wamezoea kuchunga yalikuwa yamejaa maji, hivyo nililazimika kuhakikisha kwamba nawatoa mbali ya eneo la ndani ya nyumba za wafanyakazi wa tanesco na kuwapeleka maeneo ya jengo la Drive in cinema ambako usiku pamoja na mvua zile lakini Watu hawakuisha kwenda kuangalia picha (movie za kihindi) na zaidi walikuwa ni wahindi ambao walifaidi kuangalia huku wakiwa kwenye magari yao maana eneo lote la ukumbi huo lilikuwa wazi kwa juu tofauti na majumba mengine ya Cinema.
Zaidi ya hizo shuguli nilipenda pia kufanya mazoezi ya kuinua vyuma vizito ambapo nilikuwa nimejitengenezea vifaa vya mazoezi na ilibidi niwambie vijana wenzangu juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ya kujaza misuli, hivyo walifanikiwa kunipa ushirikiano mkubwa sana vijana wengi waliokuwa wakiishi ndani na nje ya kota za Tanesco, mara waliingia Doto Peter na Richad Lunaga ambao walikuwa na tabia ya kufanya mazoezi wakati wa jioni na kuanza kuniita kama kawaida yao jina la utani, "Shaaban Mpalule" aliita Richard Lunaga ambaye kwa wakati huo tulitaniana, Bwana Mkubwa< nikiwa namaanisha mkubwa wangu wa kazi, nikiwaiga askari na wafungwa ambao ufanya tabia hiyo wakati wote wawapo gerezani.
Power, weweeeeee power kuja nilimtania Richard ambaye alipewa jina hilo kutokana na kuwa menene kwenye sehemu zake za kifua na mikono kwa ajili ya kuinua vyuma vizito, leo ufanyi mazoezi Shabba? maana pia alipenda kuniita Shabba, akinifananisha na mwanamuziki wa Marekani Shabba ranks, "nilimwambia siwezi kushiriki mazoezi kwa kuwa nilikuwa na kazi ya kufyeka majani, hivyo baada ya wao kuanza kufanya mazoezi mimi nilichukua fyekeo na kuanza kukata majani ambayo kwa wakati huo yalikuwa marefu kupindukia. .
Usikose kufuatilia Adithi hii kila siku 0713869133/0767869133
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment