TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 19, 2016
RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akimpongeza Mathias Meinrad Chikawe mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.
Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe ameapishwa leo tarehe 19 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Batilda Salha Burian ambaye Mkataba wake umemalizika.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Mheshimiwa Chikawe ameahidi utumishi uliotukuka na kuiunganisha vyema Tanzania na Japan hususani katika masuala ya kiuchumi.
Mheshimiwa Chikawe ametoa wito kwa watanzania wote hasa waishio Japan na nchi nyingine zinazotumia Ofisi ya Ubalozi huo wa Tanzania, kuutumia vizuri ubalozi huo ili kunufaika na fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji.
Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, pia unatoa huduma za kibalozi katika nchi za Korea Kusini, New Zealand, Papua New Guinea na Australia.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
19 Aprili, 2016.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment