TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, April 22, 2016
MADINI YATANZANITE YALIYOKAMATWA YAPIGWA MNADA HADHARA
Na Woinde Shizza,ArushaHatimaye serikali imeamua kuyapiga mnada madini ya vito aina yaTanzanite yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi bila vibali ambapojumla ya kiasi cha sh,1.6 bilioni zimepatikana mara baada ya madinihayo kupigwa mnada.Akizungumza mara baada ya kufunga maonyesho ya tatu ya kimataifa yamadini ya vito jijini hapa kamishna wa madini kanda ya kazkazini,EliasKayandabila alisema kwamba zoezi la mnada huo bado linaendelea nawanatarajia kupata kiasi cha zaidi ya sh,2.5 bilioni.Kayandabila,aliliambia gazeti hili ya kwamba lengo kuu la kuyapigamnada wa madini hayo hadharani ni kuweka uwazi kwenye mauzo ya madini hayo nchini na kuwapa fursa wafanyabiashara wakubwa na wadogokushiriki biashara hiyo kwa uwazi.Akizungumzia maonyesho ya tatu ya kimataifa ya madini ya vitoyaliyofungwa juzi kamishna huyo alisema kwamba kumekuwa na mafanikiolukuki yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa wauzaji wadogowa kushiriki maonyesho hayo tofauti na miaka ya nyuma.Alitaja mafanikio mengine yaliyojitokeza ni pamoja na wauzaji haokununua madini yanayochimbwa katika mgodi wa Tanzanite One tofauti namiaka ya nyuma ambapo kampuni hiyo ilikuwa ikiyauza madini hayo kwawauzaji wakubwa pekee.“Kitendo cha kuruhusu hawa wauzaji wadogo wa madini kushirikimaonyesho haya ni cha kipekee huko nyuma hawakuwahi kupata nafasi hii“alisema KanyandambilaHatahivyo,kamishna huyo alitoa wito kwa wizara ya nishati na madininchini kuhakikisha wanavutia nchi mbalimbali kuja kushiriki maonyeshohayo ikiwa ni pamoja na kuziondolea mlolongo wa kodi na usajili kablaya kushiriki kwa lengo la kuongeza idadi ya washiriki mwakani.Baadhi ya washiriki katika maonyesho hayo walisema kwamba maonyeshohayo yamekuwa na mafanikio makubwa mwaka huu huku wakiiomba serikali kuhakikisha inatoa ushirikiano wa dhati katika kuyapa nguvu mwakani.Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya vito ya Crown Lapidary,Rajan Vermapamoja na mkurugenzi wa kampuni ya madini ya vito ya Tom Gems ,ThomasMunisi walisema kwa nyakati tofauti kwamba maonyesho hayo yatakuwa namafanikio katika siku za usoni endapo yakipewa uzito mkubwa na idadiya wageni ikiongezeka.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment