TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, June 16, 2016

Benki ya Exim yaendesha zoezi la uchangiaji damu kuokoa maisha ya watanzania

Wafanyakazi wa benki ya Exim, wateja pamoja na watu wengine Tanzania jana walijotokeza kwa wingi kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya uchangiaji damu duniani. Akizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi hilo likiendelea, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu kutoka benki hiyo Bw. Frederick Kanga alisema hatua hiyo ni muendelezo tu kwa kuwa kuwa wamekuwa wakifanya hivyo tangu mwaka 2010 na lengo kuu kukabiliana na tatizo upungufu wa damu salama kwenye vituo vya afya hapa nchini. “Mara zote tumekuwa tukijisikia kuwa na furaha ya ajabu inapofika siku kama hii ya leo kwa kuwa tunaamini kwamba tunapata fursa ya kutimiza wajibu wetu kama sehemu ya jamii lakini pia kwa kufanya hivyo tunakuwa tumeshiriki kuokoa maisha ya wenzetu wanaopoteza maisha kwa kukosa damu salama pale wanapoihitaji,’’ alisema. Kauli hiyo ya Bw. Kanga inakwenda sambamba na kauli mbiu ya uchangiaji damu ya mwaka huu inayosema: “Sote tunaunganishwa na damu’’. Kauli mbiu hiyo inalenga kuonyesha namna gani maisha ya watu wenye uhitaji wa damu huokolewa na wenzao wanaojitokeza kuchangia damu. Akizungumza wakati akisimamia zoezi hilo Afisa Uhamasishaji na elimu kwa umma kutoka Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bi. Fatma Mujungu alisema uhaba wa damu hapa nchini umekuwa ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo wa Wananchi walio wengi kwamba wapo tayari kuchangia damu pale tu inapohitajiwa na mmoja wa wanandugu wa familia husika. “Hivyo basi natoa wito kwa Wananchi mmoja mmoja pamoja na taasisi nyingine kuiga mfano wa benki ya Exim Tanzania ambayo imekuwa na utamaduni wa kuchangia damu kila mwaka ili kuokoa maisha ya watanzania wote,’’ alisema. Kwa upande mwingine baadhi ya wafanyakazi na wachangiaji hao walisema wamekuwa wakiguswa na hitaji hilo muhimu la kuchangia damu kila mwaka kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii na wanahitaji kuleta mabadiliko ndani ya jamii kwa kuokoa maisha ya wenzao wenye uhitaji wa huduma hiyo muhimu.

No comments:

Post a Comment