TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, June 14, 2016

Kaya 60 zimeondolewa katika mpango wa Tasaf III Halmashauri ya Mji Kibaha

Na: Lilian Lundo – MAELEZO Jumla ya Kaya 60 katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha zimeondolewa katika mpango wa kunusuru kaya maskini nchini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III) kutokana na kutokidhi vigezo. Akiongea kwa njia simu Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Innocent Byarugaba amesema kuwa jumla ya kaya 2,388 zimekuwa zikinufaika tangu kuanza kwa awamu hiyo lakini kwa sasa ni kaya 2,328 ndio zitaendelea kunufaika na ruzuku hiyo baada ya kaya 60 kuondolewa katika mpango huo.“Katika awamu hii, kaya 60 zimeondolewa katika mpango huo baada ya kutokidhi vigezo, ikumbukwe kuwa fedha hizi za ruzuku zina masharti tofauti na ruzuku za awamu ya kwanza na pili ambapo kama mnufaikaji hajakidhi vigezo hakuna namna nyingine zaidi ya kumuondoa kwenye mpango,” alisema Byarugaba.Byarugaba aliendelea kutaja vigezo ambavyo vimefanya kaya hizo kuondolewa kwenye mpango huo kuwa ni pamoja na kaya zilizoshindwa kufuatilia watoto wao kwenda shule, kaya zilizoshindwa kuwapeleka watoto chini ya miaka mitano kliniki na zile kaya ambazo hazikustahili kupata ruzuku lakini ziliingia kwenye mpango.Vile vile Byarugaba amesema kwamba, mpango huo unalenga kuwainua wananchi katika sekta ya afya, elimu pamoja na kuwawezesha wananchi kupata milo mitatu.Tangu kuanza kwa TASAF III jumla ya Tshs. milioni 572,840,680 zimeshatolewa kwa walengwa.Aidha Fedha hizo zimekuwa zikitolewa kwa awamu tofauti tofauti ambapo jumla ya Tshs. milioni 87, 608, 295 zimegawiwa katika awamu ya sita kwenye mitaa 40 huku kaya 2,328 zikinufaika ukiondoa kaya 60 zilizoondolewa.Awamu ya kwanza Fedha zilizotolewa ni Tshs. Milioni 106,574,159, awamu ya pili Tshs. milioni 96,354,886, awamu ya tatu Tshs. milioni 94,426,568, awamu ya nne Tshs. milioni 95,276,818 na ya tano Tshs. milioni 92,599,954.

No comments:

Post a Comment