ZIARA YA SERIKALI YA JIMBO LA PUNTLAND-SOMALIA NCHINI TANZANIA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua
jambo wakati wa kikao na ujumbe kutoka Serikali ya Jimbo la Puntland
-Somalia walipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake
ni Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland –
Somalia, Mhe. Abdirahman A. Abdulle. 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro
akiukaribisha ujumbe kutoka Serikali ya Jimbo la Puntland - Somalia,
ulipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake ni Waziri
wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland – Somalia,
Mhe. Abdirahman A. Abdulle akiwa na Maafisa alioambatana nao. 
Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland
–Somalia, Mhe. Abdirahman A. Abdulle akizungumzia lengo la Serikali yake
kuitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake ni Maafisa
aliombatana nao.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry
Mambo akieleza namna Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
kitakavyoshirikiana na Serikali ya Jimbo la Puntland – Somalia katika
kuijengea uwezo Sekta ya Umma ya Serikali hiyo.

Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akibadilishana kadi
za mawasiliano na baadhi ya Maafisa kutoka Serikali ya Jimbo la
Puntland - Somalia mara baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha katika
Ofisi ya Rais-Utumishi iliyofanyika mapema leo.
No comments:
Post a Comment