TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, June 15, 2016
SERIKALI KUTOA VIFAA TIBA KWA WAJAWAZITO 500,000 NCHINI
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO
SERIKALI katika mwaka 2016/17 imekusuduia kutoa vifaa vya kujifungulia kwa wanawake wajawazito 500,000 ili kuwasaidia kukabiliana na
matatizo ya uzazi pingamizi ikiwemo ugonjwa wa Fistula.
Hatua hiyo imekusudiwa kuchochea na kuwahamasisha wanawake wajawazito kujifungulia katika vituo vya huduma ya afya nchini badala ya
kufika kwa wakunga
wa jadi.
Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mgeni Jadi Kadika.
Mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kutokomeza tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.Waziri Ummy alisema ugonjwa wa fistula umekuwa ukiwapata wanawake wa hadhi ya chini hususani wale wa vijijini ambapo kuna uhaba wa miundombinu ya vituo vya afya, uhaba wa wataalam
na msongamano wa wa kupata huduma.
Waziri Ummy alisema ugonjwa wa fistula hausababishwi na kurogwa, laana au kutembea na wanaume wengi, kama ambavyo baadhi ya wanajamii wanavyoelewa, hivyo ili kukabiliana na uginjwa huo Serikali imekuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wanawake kujifungulia katika vituo vya afya.
“Tutawahamisha wanawake wote wajawazito hususani wa kiuanzia miezi 2 na kuendelea wanaanza kliniki mapema ili kuwasadia na uzazi pingamizi,”
alisema Ummy.
Aidha Waziri Ummy alisema Serikali pia imekusudia kuhakikisha kuwa hospitali za rufaa za mikoa nchini zinakuwa na huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wa fistula ili kuwawezesha wanawake wenye tatizo hilo wanapata huduma za matibabu kwa ufanisi.
Alisema ugonjwa wafistula umekuwa na madhara ya kijamii, kiafya na kiuchumi ikiwemo wajawazitowengi kupoteza watoto, wanawake kuachwa na waume zao pamoja na akina mama haokushindwa kujihusisha shughuli za maendeleo
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment