Mratibu
wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza
Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison
Chinyuka akizungumza na Viongozi wa vikundi vya mradi huo (hawapo
pichani) walipotembelea Kata ya Makanya Wilaya ya Same kukagua
utekelezaji wa mradi huo Juni 14, 2016. Afisa
Mtendaji Kata ya Makanya Bw.Josephat Kitunga akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza
Athari za Maafa katika Kata yake alipotembelewa na Wataalamu wa masuala
ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kukagua miradi inayotekelezwa, tarehe
14 Juni, 2016. Mkuu
wa Wilaya ya Same Mhe.Herman Kapufi (katikati) akizungumza na baadhi ya
Wadau wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza
Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame walipotembelea
Wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa mradi katika kata ya Makanya, Vunte
na Hedaru Mkoani Kilimanjaro. Mchumi
Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Magreth Sembuyagi
akifafanua jambo walipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Same
Bi. Monica Kwilulihya (hayupo pichani) ili kuendelea na shughuli za
kukagua miradi inayotekelezwa na Ofisi hiyo.
Mnufaika wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bi.Neema akifurahia mafanikio ya kununua ng’ombe mara baada ya kuuza kuku aliozalisha kupitia mradi huo katika Kata ya Makanya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, tarehe 14 Juni, 2016 Mwenyekiti wa Kikundi cha Ujamaa Bi. Khadija Mrutu akihudumia mifugo aliyozalisha kupitia Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kutembelewa na Wadau wa mradi huo kwa kufanya tathimini za utekelezaji wake.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:
Post a Comment