TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, June 13, 2016

Serikali yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami





Frank Mvungi-Maelezo

Serikali yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kati ya Tanki Bovu na Goba Jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi wa Miradi wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam Bw. Ngusa Julius wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.Akifafanua Mhandisi Ngusa amesema kuwa fidia kwa wakazi hao itakamilika kulipwa wiki hii ili kazi ya ujenzi wa Barabara hiyo iweze kukamilishwa kwa wakati hali itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari.

“Ujenzi wa barabara hii ukikamilika utasaidia kwa Kiasi kikubwa kupunguza foleni kwa kuwa itakuwa kiungo kati ya wakazi wa Mbezi Beach na Kimara na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam.” Alisisitiza Mhandisi Ngusa.Kwa upande wa Barabara ya kinyerezi Kifuru Mhandisi Ngusa amesema kuwa Milioni 431 zimetumika kulipa fidia na ujenzi wa Barabara hiyo unaendelea.


Miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamai inayotarajiwa kukamilika katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha 2015/2016 itasaidia kupunguza msongamano wa magari kwa kiwango kikubwa katika jiji la Dar es salaam.Awamu ya Tatu ya ujenzi itahusisha barabara za Goba - Wazo hill -Tegeta Kibaoni (13.0Km), Mbezi Mwisho - Malambamawili- Kifuru (6kM), Goba - Makongo ardhi (9km ) na Pia kukamilisha usanifu wa outering road Bunju B - Mpiji Magohe - Victoria Kifuru hadi Pugu kiltex 33.7.

Wakala wa Barabara nchini TANROADS unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara katika jiji la Dar es salaam kwa kiwango cha lami ambapo barabara hizo zinatarajiwa kuondoa tatizo la msongamano wa magari katika jiji hilo.

No comments:

Post a Comment