TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, June 13, 2016

SERIKALI YATENGA TSH MILIONI 430 KUFANYA UPEMBUZI YAKINIFU BARABARA YA TARIME- NYAMWAGA- MUGUMU

 
SERIKALI katika mwaka 2016/17 imetenga kiasi cha Tsh. Milioni 430 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa barabara ya Tarime-Nyamwaga- mugumu ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.Aidha Serikali pia imetenga kiasi cha Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mara katika barabara ya Tarime-Nyamwaga-Mugumu.Akijibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alisema kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo hususani katika sekta ya utalii, Serikali imekusudia kuijenga barabara hiyo kwa awamu.Alisema barabara hiyo imeanza kujengwa kutoka Tarime kuelekea mugumu, ambapo hadi sasa jumla ya kilometa 6 za barabara hiyo zimekamilika kwa kiwango cha lami katika eneo la Tarime mjini.Aidha Mhandisi Ngonyani alisema ujenzi wa kilometa 2 unaendelea na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015/16.“Barabara ya Tarime-Nyamwaga- Mugumu (Serengeti) ni barabara ya mkoa yenye urefu wa kilometa 86 ni kiungo muhimu sana kiuchumi na kijamii kwa Wilaya za Tarime na Serengeti” alisema Ngonyani.Katika swali lake, Mbunge Heche alitaka kufahamu Serikali itaijenga lini barabara ya Tarime-Nyamwaga- Serengeti kwa kiwango cha lami

No comments:

Post a Comment