Wabunge
wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara
baadya kumalizika kwa sala ya kuliombea Bunge leo asubuhi mjini Dodoma
na wakiendelea na msimamo wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt.
Tulia Ackson. Mbunge
wa Ukonga (CHADEMA) Mhe. Waitara Mwikwabe akiwa pamoja na Mbunge wa
Same Mashariki (CHADEMA) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) na Mbunge wa
Viti Maalum (CHADEMA) Mary wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge hilo leo
mjini Dodoma kuendeleas na msimamo wao wa wao wa kutomtambua Naibu Spika
wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Mbunge
wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa
Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto) na Lucy Magereli
(katikati) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge hilo leo asubuhi
mjini Dodoma. Mbunge
wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa
Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na
Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika
kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma. Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishina Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki
akibadilishana mawazo na Mbunge wa Sengerema (CCM), Mhe. William Ngeleja
na Mbunge wa Kibaha Vijijini (CCM), Mhe. Hamoud Jumaa (CCM) mara
baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo linaloendelea
mjini Dodoma. Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, ushirikiano wa afrika mashariki na
Kikanda, Mhe. Susan Kolimba, akisalimiana na Mbunge wa Muleba Kusini,
Mhe. Anna Tibaijuka mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha
Bunge hilo leo mjini Dodoma. Wabunge
wa CCM kutoka kushoto Sadifa Juma (Donge), Augustine Vuma (Kasulu
Kusini) na Innocent Bilakwate (Kyerwa) wakibadilishana mawazo nje ya
ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha
asubuhi cha Bunge hilo leo.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA).
No comments:
Post a Comment