TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, June 14, 2016
KANISA LA THE SILOAM LAKABIDHI HUNDI YA SH.MILIONI 19 KWA MKUU WA WILAYA KINONDONI .
Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 19 ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya, Ally Hapi akizungumza na waumini wa kanisa la The Pool of Siloam Church ambao wamefika katika viwanja vya manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kumkabidhi hundi ya sh.milioni 19 ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Jacob Boniface
Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akitoa neno la shukrani katika hafla ya kumkabidhi hundi ya sh.milioni 19 ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waumini wa kanisa la The Pool of Siloam Church waliofika kushuhudia makabidhiani ya mfano wa hundi ya sh.milioni 19 ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amezitaka Taasisi mbali mbali za Dini kujitolea katika kuchangia madawati ili iweze kukabilina na changamoto za madawati katika wilaya hiyo. Hapi,ameseyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokabidhiwa hundi ya sh.Milioni 19 kutoka kwenye kanisa la The Pool of Siloam Church kwa ajili ya kusaidia kumaliza tatizo la madawati. Ambapo amesema kitendo cha Kanisa hilo kusaidia tatizo la madawati ni jambo jema ambalo litasaidia kumalizana na changamoto ya madawati huku akitaka taasisi zengine kuiga mfano wa kanisa hilo. Amesema kwa sasa Wilaya yake inakabilia kumaliza changamoto ya ukosekanaji wa madawati ambapo amedai mpaka kufikia mwisho wa mwezi uwenda tatizo la madawati akatika wilaya hiyo litakuwa limekamilika. Hata hivyo,Hapi amewataka watendaji wa manispaa hiyo kuhakikisha wanazipeleka pesa hizo zilizotolewa kunakohusika na sio sehemu nyengine. Aliongeza kuwa yeye yuko tayari kuwafuata viongozi wa dini ili waweze kumsaidia katika kampeni ya madawati katika kumaliza tatizo hilo katika halmashauri ya Kinondoni kwa wanafunzi kuachana na kukaa chini ya sakafu. Amesema kanisa kujitoa huko atafikisha salamu kwa Rais Dk.John Pombe Magufuli kutokana na mwitikio wa kutambua umuhimu wa elimu na kukubali kuchangia. Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya amesema kuwa mchango wa fedha hizo kwa ajili ya madawati imetokana na mchango wa waumini wa kanisa hilo kwa kuguswa na madawati Eliya amesema ataendelea kuchangia katika hatua mbalimbali kutokana nafasi ya kanisa katika jamii hasa katika matatizo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment