TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, June 12, 2016

OLE SENDEKA AWATAKA JAMII YA WAMASAI KUTEUA CHIFU MPYA MWENYE HEKIMA NA BUSARA YA KUTOSHA


Na Bashir Nkoromo, KibahaMsemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, ameongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani. Katika shughuli hiyo ambayo ilifanyika kimila, Sendeka ambaye alialikwa kuongoza shughuli hiyo Kama kiongozi wa Kimasai anayeheshimika, aliwataka Jamii ya Wamasai Kanada za mikoa hiyo, kuwa na Umoja na kutumia hekima na busara katika kumpata mrithi wa nafasi iliyoachwa na Chifu Ole Maitei. Aliwataka kumteua Chifu au Laiboni, mwenye sifa zinazostahili ambazo hata kama Chifu Ole Maitei angekuwepo angerithika kuwa anafaa kuwa mrithi wake. Kwa heshima aliyopewa katika shughuli hiyo Ole Sendeka, aliweka kwenye kaburi kibuyu na usinga ambavyo ni vifaa alivyokuwa akitumia Chifu Ole Maitei ambaye ndani ya Jamii hiyo anatambuliwa zaidi kwa cheo cha Laiboni ambaye ni kiongozi mkuu wa viongozi wanaofuatia hadhi yake wanaoitwa Laigwanani. Uwekaji vifaa hivyo ulifayika huku ukishuhudiwa na ndugu jamaa na wanajamii hiyo, Mjane na Dada wa Marehem. Mmoja wa Malaigwanani waliohudhuria shughuli hiyo, alisema, Kibuyu hicho alichoweka Ole Sedeka kwenye kaburi, ndani kilikuwa na mawe ambayo Chifu Ole Maitei alikuwa akiyatumia kubashiri yanayoweza kutokea mbele ya safari huku usinga akiutumia kupungia kuwasalimia wageni au kufukuzia mbali mifarakano na balaa katika jamii yao. Kabla ya kuweka vifaa hivyo kwenye kaburi, Sendeka alitanguliwa na watoto wote wa kiume kumwaga kwenye kaburi hilo asali, maziwa ya ng'ombe na mafuta ya kidari cha dume maalum la ng'ombe kama ishara ya kutekeleza mila na desturi. Chifu Ole Maitei ambaye alikuwa kiungo muhimu kwa kuunganisha jamii hiyo ya Kimasai hasa katika utatuzi wa migogoro yawafugaji kutoka jamii hiyo na wakulima katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa alipokea nafasi ya Uchifu kutoka kwa Laibon Labani Moreto ambaye alifariki miaka ya 2005.
asai wa jamii ya Parakuyo wakiwa wamelizunguka kaburi la Kiongozi wao wa kimila Chifu Moreto Ole Maitei, wakati Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, alipowaongoza katika shughuli ya arobaini ya Kiongozi huyo, wa jamii hiyo Kanda ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa,  iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani.
 Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, akilitazama kaburi, alipoongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani.
 Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, na baadhi ya viongozi wa kimila wakiwa mbele ya kaburi, alipoongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani..
  Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, na baadhi ya viongozi wa kimila wakiwa mbele ya kaburi, alipoongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani
 Mtoto wa kwanza wa kiume wa  aliyekuwa Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, akimwaga maziwa kwenye kaburi la kiongozi huyo, wakati wa shughuli ya arobaini iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani
 Mtoto wa kwanza wa kiume wa  aliyekuwa Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, akimwaga asali kwenye kaburi la kiongozi huyo, wakati wa shughuli ya arobaini iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani
  Mtoto wa kwanza wa kiume wa  aliyekuwa Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, akimwaga maziwa kwenye kaburi la kiongozi huyo, wakati wa shughuli ya arobaini iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani
 Vijana wa jamii hiyo wakiwa na vibuyu vyenye asali na maziwa kwa ajili ya Watoto wa kiume wa Chifu huyo kumwagia kwenye kaburi
  Mtoto wa pili wa kiume wa  aliyekuwa Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, akimwaga maziwa kwenye kaburi la kiongozi huyo, wakati wa shughuli ya arobaini iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiwa na badhi ya viongozi wakati wa shughuli hiyo. Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini mkoa wa Pwani George Kifuku
 Mtoto wa pili kutoka mwisho wa Chifu huyo, Lesimeli Moreto (6) akisaidiwa kumwaga maziwa kwenye kaburi
 Mtoto wa mwisho wa Chifu Moreto, Likadi Moreto (3) akisaidiwa kumwagia mfuko wa chakula wa ng'ombea dume,  kwenye kaburi
 Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, akiweka majani kweye kaburi, alipoongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani. .
 Kijana Lucas Moreto akiweka majani kwenye kaburi
 Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, akiomba duaa ya kimila kabla ya kuweka kibuyu cha utabiri cha Chifu kweye kaburi, alipoongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani.
 Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, akiendelea kuomba duaa ya kimila baada ya  kuweka kibuyu cha utabiri cha Chifu kweye kaburi, alipoongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani.
 Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, akiwa na mjane wa Chifu Moreto Magdalena Tikwa,
(Picha Zote na Bashir Nkoromo).

 

No comments:

Post a Comment