TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, June 14, 2016
AZAM KUWEKA WAZI MAJINA YA WACHEZAJI WATAKAOACHWA NA WATAKAOINGIA JULAI MOSI
Na Zainab Nyamka,Globu ya JamiiUONGOZI wa klabu ya Azam umeweka wazi kuanzia Julai 01 watataja majina ya wachezaji watakaoachwa na timu hiyo pamoja na wanaotarajiwa kujiunga nao, hilo linakuja katika kuimarisha kikosi hicho chenye maskani yake Chamazi hasa baada ya kushindwa kufikia malengo waliyoyaweka ya kucheza klabi bingwa Afrika mwakani.Akizungumza na waandishi wa habaru, Afisa habari wa Azam, Jaffari Iddy Maganga amesema kuwa wanataka kutengeneza kikosi ambacho kitakuja kuwa na ushindani mkubwa na kufikia malengo waliyojiwekea hususani kucheza klabu bingwa na kufika mbali zaidi. "Azam tumetolewa mapema kwenye kombe la Shirikisho tuhakamishia nguvu zetu kwenye ligi lakini tukaishia kushika Nafasi ya pili".Amesema Jaffari, Julai Mosi wataweka wazi wachezaji watakaowaacha kwenye timu ya wakubwa na ni wachezaji wangapi wataongezwa kutoka timu ndogo ikiwa pamoja kuwataja wachezaji watakaosajiliwa ili kuboresha kikosi chetu. "Tutawatumia zaidi wachezaji wetu wa kikosi B kwani umefika muda wa kuwapa nafasi za kucheza timu kubwa kwani wameonesha uwezo wa hali ya juu sana katika michuano ya vijana na wana uwezo mkubwa,"amesema.Ukiachilia hilo, amewataka mashabiki wa Azam kuwa na subira na kuacha kusikiliza maneno ya watu zaidi ni kuwa wachezaji kwa sasa wapo mapumziko ila watarejea hivi karibuni kwa ajili ya kujiunga na kuanza mazoezi ya pamoja
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment