TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 25, 2015

Rais Jakaya Kikwete awasili Zambia

ZAM1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka Zambia na kupokewa na mwenyeji wao Rais Edgar Lungu wa Zambia leo asubuhi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.(PICHA NA FREDDY MARO WA IKULU) ZAM2Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka Zambia na kupokewa na mwenyeji wao Rais Edgar Lungu wa Zambia leo asubuhi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili(

MGOGORO WA MWEKEZAJI NA WANANCHI KUHUSU SHAMBA LA MAKANGALE WAMALIZIKA

images
Na Masanja Mabula -Pemba . Mgogoro wa shamba kati ya Mwekezaji  na wananchi wa Shehia ya Makangale umemalizika ambapo  pande hizo zimefikia makubaliano na kuahidi kushirikiana  kulinda na kudumisha amani pamoja na kukuza kipato chao kupitia sekta ya Utalii .
Makubaliano hayo yamefikiwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ambapo Mwekezaji Amit Ladwa amekubali kulipa fidia ya miti aina ya mivinje ambayo imepandwa na wananchi katika shamba hilo .
Akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika kwenye ufukwe wa Vumawimbi liliko shamba  , Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ameiagiza Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Pemba kuharakisha kufanya tathmini na miti hiyo ili wananchi walipwe fidia na Mradi huo uanze kutekelezwa .

BENKI YA POSTA TANZANIA (TPB) YABORESHA ZAIDI HUDUMA KWA WATEJA BAADA YA KUJIUNGA KATIKA MTANDAO WA TTCL KATIKA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

PO1
Benki ya Posta Tanzania (TPB) na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wamekabidhiana rasmi mradi wa huduma kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

SHULE ZA MSINGI MKOANI SINGIDA KUPOKEA VITABU 200

Shule tatu za msingi katika mkoa wa Singida,zitapokea vitabu 200 wiki hii kusaidia katika mchakato wa kuboresha elimu ya shule ya msingi. Vitabu hivi vimetolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Children’s Book Project for Tanzania na italenga maelfu ya watoto nchini kote katika kuwakomboa kielimu.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo,Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali alisema kuwa Watoto wanaotakiwa kupata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu.
 
“Watoto wanaopata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu. vitabu hivi vinatolewa kwa watoto ili waweze kutumia katika masoma yao ya kila siku shuleni.” alisema Ramadhani
 
Msaada huu wa vitabu umejikita katika kukomboa hali ya elimu Tanzania, huku serikali ikijitahidi kuwekaza katika elimu nchini kwa kipindi kirefu. Inakadiriwa kuwa asilimia kubwa ya watoto wa shule ya msingi Tanzania hawajui kusoma na kuandika,Ukosefu wa vitabu unachangia wanafunzi wa shule ya msingi kushindwa kusoma na kuandika.
 
Tafiti mbalimbali kutoka za serikali na sekta binafsi zinaonyesha wazi kuwa kujifunza kusoma mapema ni uwekezaji katika siku zijazo kwa mtoto,kwani elimu katika ngazi ya chini kwa mwanafunzi inachangia kuboresha maisha yake ya baadae.
 
Kwa upande wake Doris Mollel ambaye ni Balozi wa Elimu mkoani Singida anatambua umuhimu wa elimu katika ngazi ya chini na anatumia muda wake mwingi katika harakati za kukomboa elimu ya shule ya msingi. Ziara zake nyingi hujikita katika mikoa ya ukanda wa kati hususani Singida na Tanzania kwa ujumla,Vile vile ni mshauri wa wanafunzi wa shule za msingi.
 
“Msingi wa kujifunza kusoma hufungua uwezo wa kufikiri kwa mwanafunzi akiwa na umri mdogo bila kiini hiki cha msingi maendeleo na mafanikio ya mwanafunzi ni magumu.” alisema Doris
 
Doris Mollel ni Miss Singida kanda ya kati 2014/15 na analenga katika kuboresha maisha ya jamii kwa kupitia elimu na masuala mengine ya kitamaduni.
Miss Singida kanda ya kati 2014/15,Doris Mollel akisikiliza jambo kutoka kwa Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali wakati akipokea vitabu kutoka Children’s Book Project for Tanzania.

JAMHURI KIHWELO (JULIO) AJIUNGA NA COASTAL UNION YA TANGA

jul1Kocha Msaidizi wa Coastal Union,Jamhuri Kiwelu “Julio”kulia akizungumza na wachezaji mazoezini jana mara baada ya kuwasilia mkoani Tanga kuifundisha timu hiyo kushoto ni Kocha Mkuu James Nandwa ,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Coastal Union,Albert Peter,Katibu Mkuu Coastal Union,Kassim El Siagi na Meneja wa Coastal Union Akida Machai. jul2Kocha Msaidizi wa Coastal Union,Jamhuri
Kiwelu “Julio”kulia akisisitiza jambo mazoezini jana mara baada ya
kuwasilia mkoani Tanga kuifundisha timu hiyo kushoto ni Kocha Mkuu
James Nandwa ,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Coastal Union,Albert
Peter,Katibu Mkuu Coastal Union,Kassim El Siagi na Meneja wa Coastal
Union Akida Machai.

PATO LA MWANANCHI MBEYA LAVUKA LENGO LA KITAIFA

index WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameupongeza uongozi wa mkoa wa Mbeya kwa kuvuka lengo la wastani wa pato la mwananchi kitaifa na kuwataka waendeleze kasi ya kupambana na umaskini kwa wakazi wa mkoa huo.
Ametoa pongezi hizo jana usiku (Jumanne, Februari 24, 2015) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa huo na wilaya zote wakiwemo wadau mbalimbali na viongozi wa dini mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Mbeya.
Alisema katika mipango yake, Serikali ililenga kwamba pato la mtu kwa mwaka liwe sh. 1,186, 200, lakini kwa sababu ya jitihada mbalimbali mkoa huo umelivuka. “Katika taarifa aliyonisomea, Kaimu Mkuu wa Mkoa amesema wastani wa pato la mwananchi umeongezeka kutoka sh. 711,201/- mwaka 2008 hadi kufikia sh 1,420,427/- mwaka 2013 na kwamba mkoa unachangia asilimia 7.43 ya Pato la Taifa,” alisema.
Alisema kipato cha mtu mmoja kwa siku ni sh. 3,891/- ambazo ni zaidi ya Dola mbili za Marekani (sh. 3,400/-). “Wakubwa hawa wanatupima kwa kuangalia kipato cha mtu kwa siku. Wanasema nchi ni maskini iwapo watu wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku (sawa na sh. 1,700/-).”

MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI

indexWizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika.
Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014. Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement – MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali
Mha. Ngosi C.X. Mwihava KAIMU KATIBU MKUU 25 Februari, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE AKABIDHIWA RIPOTI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI KWA MAKAMPUNI YA UZIDUAJI NCHINI

si1Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) akimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) ili aweze kuzungumza na timu ya majaji na sekretarieti iliyofanya kazi ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Utoaji wa Huduma za Jamii na Uwezeshaji kwa makampuni ya uziduaji yaani madini na gesi. Timu hiyo iliendesha zoezi hilo mapema Septemba, mwaka jana.

WATANZANIA WAASWA KUTHAMINI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NDANI YA NCHI


KAIMU MENEJA WA SIDO MKOA WA IRINGA, MR NIKO MAHINYA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFINI KWAKE

KAIMU MENEJA WA SIDO MKOANI IRINGA, NIKO MAHINYA AKIWA NA MHANDISI WA KARAKANA YA SIDO IRINGA, MICHAEL MATONYA WAKATI WAKITEMBELEA UTENDAJI KAZI WA KARAKANA HIYO

VURUGU KUBWA IRINGA, POLISI NA WANANCHI WAPAMBANA.

 
Zipo taarifa za kutokea kwa vurugu kubwa katika eneo la Ilula mkoani Iringa.Taarifa zinadai kuwa vurugu hizo ni kati ya jeshi la polisi na wananchi wa kawaida ambao wamefunga barabara kwa kuwasha moto wa matairi ya gari.
Aidha taarifa kutoka kwenye eneo la tukio zinaendelea kueleza kuwa hadi sasa magari manne ya Polisi na Pikipiki moja vimechomwa moto, huku basi linalofahamika kwa jina la Nyagawa linalosafirisha abiria kutoka Njombe kuja Dar es Salaam likiwa limevinjwa vioo vyote.
Taarifa hizo zinadai kuwa tayari polisi wa kutuliza ghasia FFU wameshafika eneo la tukio na kufanikiwa kwa sehemu kutuliza ghasia hizo, na kwamba magari yanayokuja Dar es Salaam na mikoa mingine yameshaanza safari zake.
Ungana nasi baadaye kwa taarifa zaidi
Chanzo Mwananchi
 …………………………………
PICHA KWA HISANI YA IRINGA YETU BLOG

Rais Jakaya Mrisho Kikwete apokea vitabu vya sayansi kwa shule za Sekondari vilivyochapishwa kwa msaada wa watu wa marekani

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya
ya 
Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili katika Shule ya
Sekondari 
ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam leo tayari kwa kukagua ujenzi wa maabara na pia kupokea na kugawa vitabu vya
sayansi 
vilivyochapishwa  na Watu wa Marekani.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maabara katika Shule
ya 
Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam
ambako  pia 
alipokea na kugawa vitabu vya sayansi
vilivyochapishwa  na Watu wa 
Marekani. Wa kwanza
kulia ni Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na 
Mafunzo ya Ufundi,
akifuatiwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda AANZA ZIARA YA MKOA WA MBEYA

1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekndari ya Igomelo wilayani Mbarari akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Mbeya Februari 24, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda AZINDUA UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

66
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua  Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba.
01
Waziri Mkuu Mizengo Pinda   na Naibu Katibu Mkuu  ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHEDEMA  John Mnyika wakitazama kadi mpya ya mpigakura baada ya Waziri Mkuu, Kuzindua uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  katika mji mdogo wa Makambako  Februari 24, 2015.

WARSHA YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WATOTO NCHINI TANZANIA YAfanyika KILIMANJARO

 
 Julieth Swai Mwakilishi kutoka UNICEF akizungumza jambo
 Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia kwa makini

Wizara yatangaza utoaji ruzuku awamu ya pili ya wachimbaji wadogo wa madini

111 
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Matokeo ya utekelezaji wa utoaji wa ruzuku kwa wachimbaji Madini wadogo nchini Awamu ya Pili yanatarajiwa kufanyiwa tathmini na ufuatiliaji kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava wakati akiongea katika Kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa kupitia Televisheni ya Taifa TBC1 mapema leo, ambapo amefafanua kuhusu taratibu za maombi ya namna ya kupata ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa madini Awamu ya Pili. Mhandisi Mwihava ameeleza kuwa, ili kupata matokeo bora ya namna ruzuku hiyo itakavyotumiwa na wachimbaji wadogo watakaokidhi vigezo vya maombi na kunufaika na ruzuku hiyo, mpango wa BRN utatumika ipasavyo kuhakikisha kwamba fedha hizo zinatumika kama ilivyopangwa. “BRN itatumika kufuatilia utekelezaji wa ruzuku. Wizarani tuna Sehemu ya Ukaguzi wa Migodi, lakini pia tuna Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), hawa wote watashirikiana kufanya tathmini yenye matokeo tunayotarajia,” amesisitiza Mhandisi Mwihava.

Mhe. Said Ali Mbarouk atembelea kituo kipya cha kurushia matangazo cha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

1
Ni Mnara wa kurushia matangazo wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ulioko Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
2
Ni chumba chenye mitambo ya kurushia matangazo (Transmitter) kilichopo katika Kituo cha Bungi Unguja.

MKUTANO MKUU WA TFF KUFANYIKA mkoani MOROGORO.

indexKamati ya Utendaji ya Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF iliyokutana jumapili Februari 22 mwaka huu, imefanya mabadiliko ya mahali utakaofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka kutoka Mkoa wa Sinigida na kuhamishia mkoa wa Morogoro.
Hatua hiyo imefikiwa na Kamati ya Utendaji kutokana na sababu za kutokukamilika kwa miundombinu ya mkutano mkuu na kuwepo ka shughuli nyingine za kijamii mkoani humo.
Kamati ya Utendaji inamshukuru Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida (SIREFA), na uongozi mzima kwa kujitolea kuandaa mkutano huo na huko nyuma waliweza kuandaa mkutano wa makatibu wa vyama vya soka vya mikoa.
TFF itaandaa vikao na matukio mengine mkoani Singida itakapotokea hapo baadae, tarehe ya mkutano mkuu itaendelea kubakia ile ile ya Machi 14, 15 mwaka huu.

SHIRIKA LA SPECSAVER LA NORWAY Linatarajia kutoa HUDUMA YA UPIMAJI WA MACHO NA KUTOA DAWA KWA WANANCHI WA ZANZIBAR BILA MALIPO

 1
Naibu Waziri wa Afya  Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wandishi wa habari kuhusu  ujio wa madaktari wa Shirika la Specsaver la Norway ambao watatoa huduma ya macho bila malipo kwa kushirikiana na wataalamu wazalendo wa Zanzibar katika skuli ya Kiembesamaki.
2
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani)  katika mkutano huo uliofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

WAZIRI MKUU AZINDUA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA KITAIFA

images 

Ametoa wito huo leo mchana (Jumanne, Februari 24, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi huo uliofanyika kwenye kata ya Lumumba, Halmashauri ya Mji wa Makambako, mkoani Njombe.
“Ninawasihi viongozi wa siasa tuwahimize wanachama wetu waende kujiandikisha kwa wingi. Tuache kauli za kukatisha tamaa, tuache kauli za kejeli sababu zoezi hili ni jema na lina nia ya kuwawezesha Watanzania wote kutumia haki yao ya kupiga kura,” alisema.

Mkuu wa Idara ya utumishi wa umma Mpanda Bw. Peter Kijika aagwa

kata1
Picha ya pamoja wa kwanza aliyevaa shati jekundu ni Katibu wa TSD Mkoa wa Katavi Deogratias Shija ,wa pili ni aliyekuwa Katibu wa TSD Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Peter Kijika,watatu ni Bi Debora Mwakaje Afisa Utumishi wa TSD,aliyevaa shati jeupe ni Alphonce Mwakyusa Afisa Utumishi Kaimu Katibu TSD Halmashauri ya Mpanda.
kata2
…………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada -Katavi
Watumishi wa Ofisi ya Rais ,Tume ya Utumishi wa Umma Idara ya Utumishi wa Walimu TSD Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imefanya hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo Bw Peter Kijika kwa kuitumikia Idara hiyo kwa utumishi uliotukuka.
Akizungumza akizungumza katika Hafla hiyo mgeni rasmi katika hafla hiyo Katibu (TSD) Mkoa wa Katavi Bw,Deogratias Shija alisema kwa niaba ya Tume ya Utumishi wa Umma  alimshukuru kwa kuitumika Idara kwa utumishi wake uliotukuka.