Na: Patricia Kimelemeta
Aliongeza mpaka sasa Tanzania ina upungufu wa watalaam wa afya katika hospitali nyingi, zikiwemo za kata, wilaya na mikoa, hii inatokana na kuwepo kwa idadi ndogo ya watalaam hao, jambo ambalo limesababisha datari mmoja kutibu wagonjwa zaidi ya 50,000 hadi laki moja.
Alisema, mkataba wa ujenzi huo unamalizika miezi miwili kutoka sasa, ambapo serikali itakuwa imepata hasara ya kulipa deni hilo bila ya ujenzi kufanyika, kutokana na hali hiyo juhudi za haraka zinahitajika ili chuo hicho kiweze kujengwa.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kuliangalia suala hilo kwa undani ili kupunguza matatizo ya watalaam wa afya ambao ndio wanaobeba jukumu la wananchi kwa ujumla.
Hata hivyo, Makamu Mkuu wa Muhas, Profesa Kisali Pallangyo alisema kuwa, ujenzi wa chuo hicho umefadhiriwa na serikali ya Korea kusini kwa mkopo wa riba nafuu katika kipindi cha miaka ishirini.
"Serikali ya Korea Kusini imetoa msaada zaidi ya dola 74 bilioni(ambazo ni sawa na Sh100) kwa riba nafuu, ikiwa ni pamoja na kuleta watalaam wa ujenzi ili waweze kufanikisha mradi huo, lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika zaidi ya kuishia kupanga,kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kuliangalia suala hilo ili tuweze kupata watalaam,"alisema Profesa Pallangyo.
Aliongeza kumalizika kwa chuo hicho kutasaidia kupata watalaam 900 hadi 1200 ambapo kwa sasa chuo hicho kinazalisha watalaam 200 hadi 200, jambo ambalo linaweza kupunguza uhaba wa watalaam.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kulipa kiasi hicho ili watalam hao waweze kufanya kazi yao kama ilivyokusudiwa.
Mkataba wa ujenzi wa chuo hicho ulifanyika mwaka 2010 ambapo watalaam hao walitakiwa kujenga katika kipindi cha miaka mitatu na miezi miwili, ambapo kwa sasa umebaki muda wa miezi miwili tu kumalizika kwa mkataba wake.
KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC) imeshindwa kupitia hesabu
za Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili(Muhas) kutokana na serikali
kushindwa kulipa kiasi cha Sh1.6 bilioni kwa ajili ya kulipa fidia ya
wakazi wa Mloganzila eneo la Kibamba ambako kwa
ajili ya kujenga chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema kuwa, mkataba wa ujenzi wa chuo hicho ulisainiwa mwaka 2010, ambapo serikali ilitakiwa kulipa fidia ya wakazi 2523 wa eneo hilo kwa Sh9.66 bilioni,lakini mpaka sasa zimetolewa kiasi cha Sh 8.06 bilioni bado Sh 1.6 bilioni kwa wakazi 604.
Alisema kutokana na hali hiyo kamati hiyo imewataka makatibu wakuu wa Wizaya ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Wizara ya Fedha na Uchumi ili waweze kutoa maelezo ya kushindwa kulipa fedha hizo.
"Tunashindwa kuzalisha watalaam wa afya wakiwemo madaktari na wengineo kutokana na serikali kushindwa kulipa kiasi cha Sh 1.6 bilioni. Lakini fedha za kulipa fidia kwa waathirika wa aina mbalimbali zipo, kutokana na hali hiyo kamati yangu haiwezi kupitia mahesabu hayo mpaka kieleweke,"alisema Zitto.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema kuwa, mkataba wa ujenzi wa chuo hicho ulisainiwa mwaka 2010, ambapo serikali ilitakiwa kulipa fidia ya wakazi 2523 wa eneo hilo kwa Sh9.66 bilioni,lakini mpaka sasa zimetolewa kiasi cha Sh 8.06 bilioni bado Sh 1.6 bilioni kwa wakazi 604.
Alisema kutokana na hali hiyo kamati hiyo imewataka makatibu wakuu wa Wizaya ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Wizara ya Fedha na Uchumi ili waweze kutoa maelezo ya kushindwa kulipa fedha hizo.
"Tunashindwa kuzalisha watalaam wa afya wakiwemo madaktari na wengineo kutokana na serikali kushindwa kulipa kiasi cha Sh 1.6 bilioni. Lakini fedha za kulipa fidia kwa waathirika wa aina mbalimbali zipo, kutokana na hali hiyo kamati yangu haiwezi kupitia mahesabu hayo mpaka kieleweke,"alisema Zitto.
Aliongeza mpaka sasa Tanzania ina upungufu wa watalaam wa afya katika hospitali nyingi, zikiwemo za kata, wilaya na mikoa, hii inatokana na kuwepo kwa idadi ndogo ya watalaam hao, jambo ambalo limesababisha datari mmoja kutibu wagonjwa zaidi ya 50,000 hadi laki moja.
Alisema, mkataba wa ujenzi huo unamalizika miezi miwili kutoka sasa, ambapo serikali itakuwa imepata hasara ya kulipa deni hilo bila ya ujenzi kufanyika, kutokana na hali hiyo juhudi za haraka zinahitajika ili chuo hicho kiweze kujengwa.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kuliangalia suala hilo kwa undani ili kupunguza matatizo ya watalaam wa afya ambao ndio wanaobeba jukumu la wananchi kwa ujumla.
Hata hivyo, Makamu Mkuu wa Muhas, Profesa Kisali Pallangyo alisema kuwa, ujenzi wa chuo hicho umefadhiriwa na serikali ya Korea kusini kwa mkopo wa riba nafuu katika kipindi cha miaka ishirini.
"Serikali ya Korea Kusini imetoa msaada zaidi ya dola 74 bilioni(ambazo ni sawa na Sh100) kwa riba nafuu, ikiwa ni pamoja na kuleta watalaam wa ujenzi ili waweze kufanikisha mradi huo, lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika zaidi ya kuishia kupanga,kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kuliangalia suala hilo ili tuweze kupata watalaam,"alisema Profesa Pallangyo.
Aliongeza kumalizika kwa chuo hicho kutasaidia kupata watalaam 900 hadi 1200 ambapo kwa sasa chuo hicho kinazalisha watalaam 200 hadi 200, jambo ambalo linaweza kupunguza uhaba wa watalaam.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kulipa kiasi hicho ili watalam hao waweze kufanya kazi yao kama ilivyokusudiwa.
Mkataba wa ujenzi wa chuo hicho ulifanyika mwaka 2010 ambapo watalaam hao walitakiwa kujenga katika kipindi cha miaka mitatu na miezi miwili, ambapo kwa sasa umebaki muda wa miezi miwili tu kumalizika kwa mkataba wake.
No comments:
Post a Comment