Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekipa
Kituo cha Televisheni cha ITV haki ya kipekee (exclusive rights)
kuonesha moja kwa moja (live) mechi kati ya Twiga Stars na Namibia
itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Twiga Stars ambayo tayari imeingia kambini Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
kambi ya Ruvu iliyoko Mlandizi mkoani Pwani iwapo itafanikiwa kuitoa
Namibia itafuzu kucheza raundi ya kwanza na mshindi kati ya Misri na
Ethiopia. Twiga Stars ilishinda mechi ya kwanza ugenini mabao 2-0.
Kampuni
ya ZH Poppe Limited imegharamia tiketi za waamuzi na kamishna
atakayesimamia mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za
Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia
itakayofanyika Januari 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mbali
ya tiketi hizo za ndege, pia kampuni hiyo itagharamia hoteli (malazi
na chakula) kwa kamishna na waamuzi hao wanne kwa muda wote
watakaokuwepo nchini kwa ajili ya mechi hiyo.
Gharama za tiketi na hoteli kwa kamishna wa mechi hiyo na waamuzi hao watakapokuwa hapa nchini ni sh. 11,856,000.
Bajeti
nzima ya mechi hiyo ni sh. 74,660,000. Hiyo inajumuisha usafiri, posho
kwa wachezaji, posho kwa benchi la ufundi, gharama za kambi, dawa na
maji ya kunywa wakati wa mazoezi na mechi kwa Twiga Stars. Maeneo
mengine usafiri wa ndege, usafiri wa ndani (magari mawili), posho na
hoteli kwa kamishna na waamuzi.
Gharama
nyingine za timu ya Namibia itakayokuwa na watu 25 ambazo ni usafiri
wa ndani (magari matatu), hoteli (malazi na chakula) na maji ya kunywa
wakati wa mazoezi na mechi.
No comments:
Post a Comment