
Mbunge
wa Arumeru Mashariki Mh. Jeremiah Sumari amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa
akisumbuliwa na maradhi ya uvimbe kichwani.
Kuzaliwa
Marehemu Jeremiah Sumari alizaliwa Machi 2 mwaka 1943 katika kijiji cha Akeri wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Elimu yake
Alisoma elimu ya msingi kati ya mwaka
1950-1957 katika shule ya msingi Meru Magharibi mkoani humo mwaka 1958-
1964 alisoma katika shule ya sekondari ya Old Moshi Mkoani Kilimanjaro
na baadae aliendelea na elimu ya juu huko Uingereza kama ifuatavyo-
ACCA, CIS, Certificate in Marketing. Uk, Lincesed Broker (LR), CPA
(Tanzania).
Utumishi wake
Mwaka 1996-2004 alikuwa Mkurugenzi wa
bodi ya soko la Hisa Stokck Exchange mwaka 1998-2003 Trustee
Privatization Trust, mwaka 1999-2006 alikuwa Mkurugenzi wa bodi Benki ya
maeneleo ya Afrika Mashariki, mwaka 2005 mpaka sasa mbunge wa jimbo la
Arumeru Mashariki Januari 4 mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Waziri wa kazi
Ajira na Maendeleo ya vijana na mwaka 2008 mpaka 2010 alikuwa Naibu
waziri wa Fedha na Uchumi.
Marehemu Jeremiah Sumari alikuwa mbunge wa Arumaru Mashariki mpaka umauti ulipomkuta
Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi Amen.




Kwanza
Tunapenda wasalimu wakubwa wetu Shikamoo na vijana wenzetu Mambo
vipi.. Tunatambua kuwa Wanavyuo wenzetu walimu walikuwa hawana kazi
kwa muda mrefu Jambo ambalo liliwafanya wengi kuwa na wasi wasi na
mwajiri wao. Tunapenda kuwapa tarifa kupitia mtandao wenu wa Matukio na
wanavyuo (www.tzwanavyuo.blogspot.com)
kuwa, Walimu wahitimu wote Jana usiku majira ya sa saba Nafasi hizo
zilitangazwa Rasmi, Pia sisi Tunapenda kuwasilisha majina ya wanafunzi
ambao wamechaguliwa Tunaomba mchukue Muda wenu kutazama kwa umakini
majina yenu yote yapo hapa. Hongereni sana.
Imeandaliwa na,
Matukio na Wanavyuo Crew
No comments:
Post a Comment