Na Mwandishi Wetu- Arusha
Mwanafunzi
aliyefahamika kwa jina la John Justine(17) mkazi wa makao mapya
amefariki dunia jana katika hospitali ya mount meru wakati akipatiwa
matibabu baada ya kujeruhiwa kwa risasi.
Akizungumza
na wandishi wa habari kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi
mkoa arusha Thobias Andeng'enye amesema kuwa tukio hilo lilitokea
majira ya saa moja na nusu jioni ambapo siku hiyo mama wa marehemu
aitwaye Betty John alikuwa akitoka kwenye sherehe mara baada ya kufika
nyumbani alikuta geti limefungwa ndipo alipowaomba majirani kumsaidia
kufungua.
Andeng'enye
amesema kuwa mama huyo amesema kuwa mara baada ya kuingia ndani akiwa
na mtoto wa jirani alimkuta mtoto wake akiwa chini amelala chini huku
akihema kwa tabu huku damu zikimtoka kifuani ndipo alipotoka nje na
kuomba msaada kwa majirani.
Aidha kamanda
alisema kuwa mma huyo pamoja na majirani walisaidina kumkimbiza
hospitali ya Dkt.Mohamed iliyopo eneo la Tank la maji Ilboru kwa
matibabu ambapo ilishindikana na kumpeleka hospitali ya mkoa ya mount
meru ambapo ailipatiwa msaada lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia.
Hata hivyo
andeng'enye amesema kuwa baada ya polisi kituo kikuu wilaya kupata
taarifa walikwenda eneo la tukio kufanya ukakuzi ambapo walikuta
bunduki aina ya shortgun Pump Action pamija na ujumbe
unaosema"ANASIKITIKA KULAUMIWA NA WAZAZI WAKE PIA ANAWAPENDA SANA"
Vilevile walikuta michirizi ya damu kutoka chumbani hadi alipoangukia.
Kamanda
ameongeza kuwa inasemekana kuwa marehemu alituhumiwa na baba yake mzazi
Jastine Kaizer kuwa aliiba fedha kiasi cha dola za marekani 1500 hivyo
polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa kumhoji baba mzazi wa marehemu .
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha mount meru ukisubiri uchunguzi zaidi wa daktari.
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MKUU wa mkoa wa Dares Salaam Said Mecky Sadick amesema bado misaada zaidi inahitajika ili kuweza kuwasaidia wahanga wa mafuriko hususan ya shughuli za ujenzi na mahitaji ya watoto walioanza shule.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Sadick wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake jijini Dares Salaam mara baada ya kupokea msaada wa hundi ya sh. milioni tano kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, ambayo ilikadhiwa kwake na Mkurugenzi Mkuu Fadhili Manongi.
“Bado
misaada inahitajika tunaendelea kutoa wito kwa watu walioguswa kuweza
kutoa michango yao ili kuweza kusaidia shughuli za ujenzi na mahitaji
ya wanafunzi walianza shule mfano madaftari, vitabu na huduma zingine
zinazohusiana na elimu,” alisema.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine iliyopo
ni kujenga nyumba za walimu na kliniki ya wakinamama na watoto,hivyo
aliwaomba Watanzania, taasisi, mashirika na watu binafsi walioguswa kuendelea kuchangia.
Wakati huohuo, Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (CBCT),kilikabidhi hundi kivuli yenye thamani sh. milioni 10 ya michango ya vitu mbalimbali kwa ajili ya wahanga hao kwa Mkuu huyo, ambayo ilikabidhiwa katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina kwa Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal juzi usiku.
Hundi hiyo ilikabidhiwa
kwa Sadick na Mwenyekiti wa CBRT Zhu Jinfeng, ambapo alisema misaada
mingine imendelea kutolewa hivyo michango hiyo hadi leo(jana) imefikia
sh. milioni 12,550,000.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa alisema agizo la kuangalia uwezekano wa kuwapatia
viwanja wapangaji liko palepale na watalitekeleza kama alivyoagiza
Rais Jakaya Kikwete, hivyo utaratibu utaanza mara baada kukamilisha
zoezi la wamiliki.
Aliongeza kuwa utaratibu huo wa wapangaji pia unahitaji fedha kwa ajili ya kufanya tathimni mpya utoaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha maeneo hayo.
Mkuu
wa Mkoa wa DSM Sadick Mecky Sadick (kulia) akipokea leo rasmi msaada
kupitia kivuli kinachoonyesha vitu mbalimbali na thamani kutoka kwa
mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara wa kichina Tanzania ZHU
JINFENG (katikati) kwaajili ya waathirika wa mafuriko jijini , Msaada
huo umekabidhiwa jana kwa Makamu wa Rais Dkt, Gharib Bilal wakati wa
sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina wenye thamani ya
shilingi milioni10. Pamoja na kukabidhi jan 15,2012 lakini leo
wamewasilisha rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Meck Sadick jumla ya
milioni 12.5 baada ya kuendelea kuchangia vitu vyengine vikiwemo mabati
na saruji, (kushoto) Ni Mmoja wa ofisa kutoka chama cha
wafanyabiashara wa kichina nchini Janson Huang . Picha na Mwanakombo
Jumaa- MAELEZO.
Mkuu
wa Mkoa wa DSM Said Mecky Sadick (kulia) akipokea hundi ya shilingi
milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri
wa Anga nchini Fadhili Manongi (kushoto) leo katika ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa DSM kwaajili ya waathirika wa mafuriko wa mkoa wa Da r es
Salaam (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO),
Mkuu
wa Mkoa DSM (kulia) Sadick Mecky (katikati) Ofisa kutoka chama cha
wafanyabiashara wa kichina nchini Janson Huang pamoja na Katibu tawala
wa Mkoa wa DSM Theresia Mmbando (kushoto) wakijadiliana leo katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM baada ya kukabidhi rasmi msaada huo wa
kivuli cha mchango wenyethamani ya shilingi milioni 10 ambapo michango
hiyo imeongezeka hadi kufikia 12.5/- (Picha na Mwanakombo Jumaa-
MAELEZO).
Baadhi
ya makocha mbalimbali kutoka mikoa ya Tanzania Bara wakiwa katika kozi
hiyo iliyoanza kibaha leo ikitolewa na mkufunzi wa makocha wa Masumbwi
wa kimataifa Josef Diouf kutoka Shirikisho la Dunia la mchezo wa ngumi
(AIBA) Picha na www.superdboxingcoa
Kocha
wa Mchezo wa Ngumi Rajabu (Super D) kulia akibadilishana mawazo na
mkufunzi wa makocha wa Masumbwi wa kimataifa Josef Diouf kutoka
Shirikisho la Dunia la mchezo wa ngumi (AIBA) katikati ni Katibu Mkuu
wa BFT, Makore Mashaga.
(Picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com)
CHAMA
cha Madaktari Tanzania (MAT), kimeipa Serikali saa 72, kuwarejesha
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wanafunzi waliofuzu udaktari waliondolewa
hapo baada ya kugoma wakidai malipo yao.
Tamko hilo lilitolewa na Rais wa chama hicho, Dk Namala Mkopi katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana.
Chama hicho kimemuomba Rais Jakaya
Kikwete, kuwatafutia kazi nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo
Mtasiwa kwa kosa la kumshauri vibaya Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hadji
Mponda. Alisema Dk. Mponda anasamehewa kwani hajui alitendalo ila
inatakiwa awaombe radhi kwa kuwaita madaktari wenzao kuwa si madaktari
bali bado wangali wanafunzi.
Rais wa MAT, Dk. Mkopi, pia
alitangaza kuwa kimefutia uanachama kwa mwaka mmoja, Mganga Mkuu wa
Serikali, Dk. Mtasiwa kwa kosa lake la kuusaliti udaktari kutokana na
kukiuka kiapo cha udakatari kinachosema kuwa Madaktari wote ni ndugu na
nitawatendea haki kama dada na kaka.
Alisema endapo Dk. Mtasiwa
atanendelea na tabia hiyo ya kudharau taaluma ya udakatari, basi chama
kitaamua kumfukuza kabisa na kumuweka kwenye mtandao wa madaktari
duniani, ili iwe fundisho kwa madaktari wengine wenye tabia hiyo.
Dk. Mkopi alisema kuwa chama
kimesikitishwa sana na kwamba hawaoni ni kwa nini Serikali imeamua
kuwaadhibu madaktari wenzao waliokuwa wakidai haki ya msingi, na
kuwaacha kuwaadhibu watu waliosababisha ucheleweshaji wa makusudi wa
kutowalipa malipo yao madaktari.
China
nvjini Tanzania, Liu Xinsheng, wakati akiwasili kwenye Viwanja vya
Mnazi Mmoja jinni Dar es Salaam jana jioni Januari 15, katika sherehe
za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, sherehe zilizoandaliwa na Chama
cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT).
Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiongoza na Balozi wa China nvjini Tanzania, Liu Xinsheng,
wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jinni Dar es Salaam
jana jioni Januari 15, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa
Kichina, sherehe zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina
nchini (CBCT).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya
wa Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina
nchini (CBCT), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam jana jioni Januari 15. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Liu
Xinsheng.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 16, kutoka
kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa
na City Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko
yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka
jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka
mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es
Salaam jana Januari 15.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka
kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa
na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili
ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya
sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari 15.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro Premium Lager
kwa kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) leo
wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa
Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa
2012.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam meneja wa bia ya
Kilimanjaro bwana George Kavishe alisema Mwaka jana Tunzo hizi za
Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo kwa mwaka
huu yataendelezwa na kuboreshwa zaidi. Ambapo Mchakato wa kuwapata
vinara hao utapitia hatua kuu zifuatazo:
1. ACADEMY:
ACADEMY
ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki kati ya
hamsini hadi mia moja( 50 mpaka 100)kutoka mikoa mbali mbali ya
Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua
na hatimae kupata wateule (Nominees) wa kinyang’anyiro hicho baada ya
majaji kujiridhisha kuwa washiriki waliopendekezwa wamekizi vigezo
vyote muhimu ambapo zoezi hili kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika
tarehe 27 na 28 Jan 2012.
2. Majaji:
Hatua
ya pili ni Majaji ambapo huwa ni hatua muhimu sana ambapo majaji huwa
na kazi moja kubwa ya kupiga kura wakizingatia vigezo muhimu vya
kiufundi zaidi na vile vile kuhakiki uteuzi wa washiriki uliofanywa
katika hatua ya awali kwenye Academy husika ikiwa ni pamoja na kura
zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali
vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka
2011, kazi zao za mwaka 2011, Mafanikio n.k. Jopo hili hujumuisha
wadau wa tasnia ya musiki kumi na tano (15).
3. KURA:
Hii
ni ni hatua ya mwisho ambapo wapenzi wa musiki waliopiga kura zao Kura
hizo hujumuishwa katika kuchangua washindi ambapo kwa shindano la
mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia
sabini (70%) na kura za majaji asilimia thelasini (30%.) na katika
kufanikisha upigaji kura kutakuwa njia kuu Njia kuu nne za upigaji wa
kura :
- Njia ya ujumbe mfupi (sms).
- Njia ya barua pepe (Email).
- Njia ya kujaza sehemu maalum katika Magazeti.
- Na njia ya mwisho ni njia ya vipeperushi (Fliers.)
Kwa
upande wake mwakilishi wa baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mzee
Luhaja amewataka wasanii wa tasnia hiyo nchini kutumia vyema fursa ya
tunzo za Kili Music Award kama sehemu ya kuweza kujitangaza katika anga
za muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Alisema
msanii mzuri ni Yule anaeweza kutunga nyimbo zenye lengo la kuelimisha
jamii na kuburudisha kwa kuzingatia maadili na hayo hujidhihirisha
kupitia kwenye tunzo kama hizi ambazo hutoa fursa kwa wasikilizaji
kutoa michango yao juu ya mwanamuziki gani aliyeweza kukonga mioyo yao
kupitia tungo zake.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu
ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM
ambayo yataanza mwanzoni mwa mwezi Februari na kufikia kilele chake
Februari 5, 2012.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema maadhimisho ya kuzaliwa kwake ya
mwaka huu pamoja na mambo mengine kitayatumia kupiga vita wagombea wote
wanaotoa na kupokea rushwa wakati wake mkuu.
Pia kitatumia maadhimisho hayo kuhamasisha wananchama wake waadilifu na
waaminifu kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika mwaka
huu, kuanzia ngazi za mashina hadi taifa.
Hayo yalisemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari,
kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.
Nape alisema, Chama kitatumia fursa hiyo pia kuwaelimisha wanachama wake
na wananchi kwa jumla kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi
yanayokusudiwa kufanyika, ikiwa ni pamoja na msimamo wa kuilinda nchi,
amani, na kupatikana kwa Katiba bora itakayokuwa na manufaa kwa watu
wote.
Alisema, maadhimisho hayo yataanza Februari mosi na kufikia kilele chake
Februari 5, 2012 yakiambatana na shughuli mbalimbali yakiwemo matembezi
ya mshikamano yatakayofanyika kila mkoa wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo
kitakachofanyika Mwanza.
Nape alisema .
"Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi kufikisha
miaka 35 ya uhai wake yangu vyama vya TANU na ASP vilipovunjwa na
kuundwa chama kipya cha CCM chenye nguvu, Februari 5, 1977",lisema Nape
na kuongeza.
"Sherehe hizo huadhimishwa kwa Chama na Jumuia zake kufanya shughuli
mbalimbali za kisiasa na kijamii. Aidha, Kitaifa Chama huteua mkoa
mwenyeji wa sherehe hizi ambazo huambatana na matembezi ya mshikamano".
Alisema kwa kuwa mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu wa Chama kimependekeza
kaulimbiu mahsusi itakayotumika katika sherehe hizo kuwa ni "CCM Imara
na Madhubuti inaanza na mimi; naimarisha Chama Changu kwa kuchagua
viongozi bora na waadilifu".
Nape alisema uzinduzi wa sherehe hizo utafanyika kila mkoa Januari 30,
mwaka huu na kufuatiwa na wiki ya shughuli za Jumuia, ambazo kila Jumuia
itapanga ratiba ya mikutano ya ndani na shughuli za kijamii kama
kupanda miti.
CCM imewataka wajumbe wa Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya mikoa
kutumia wiki hiyo kufanya ziara katika matawi kuimarisha uhai wa Chama
By A Correspondent
EXIM Bank
(Tanzania) Limited has introduced yet another innovative deposit
product aimed at encouraging regular savings among low income earners
and salaried employees and Corporates, known as "Haba na Haba Account"
The bank said in a statement issued in
Dar es Salaam yesterday that the product was a New Year gift to its
clients, who are ready to demystify financial planning and become good
savers.
"You only need to drop just a bit of
your earnings in your Haba na Haba Account after authorising Exim Bank
to set aside a small portion of your savings or salary regularly or
every month, for a fixed period ranging from 12 to 120 months.
"Put your money to work. You will be surprised how money grows on the Exim tree!" the bank said in the statement.
The depositor
gets Tsh 100 mio with a monthly investment of Tsh.515,000/-only for a
period of 10 years, as per the prevailing rates.
It noted that in today’s hard pressed times and fluctuating world
economies, more and more families are finding themselves cash-strapped.
The key word today is security and the only goal is resource
augmentation.
The bank further said the minimum amount to be deposited could be as low as 20,000/- per month, but there is no upper limit.
"The scheme is open for new, existing and corporate clients by just
authorising the bank to set aside every month the desired amount from
the savings account into Haba na Haba Account," it adds.
Exim Bank is Tanzania’s sixth largest bank in terms of total assets,
deposits and finances and has a network of 22 branches and 48 Automated
Teller Machines (ATM) across the country.
It
is the only locally bank which has dared to spread wings outside
Tanzania, with opening of subsidiaries in Djibouti and Comoros Island.
It has a single branch in Djibouti and two branches in the Indian Ocean
Island.
Mkuu
wa kitengo cha mauzo ya Vodacom m-pesa Franklin Bagala,akiongea na
Mawakala wa m-pesa wa Mkoa wa Dares Salaam katika semina iliyoandaliwa
na Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao kujifunza namna ya kutoa
huduma zilizo bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina hiyo ilifanyika kwa
siku mbili katika ukumbi wa Karimjee jijini.
Mmoja
wa mawakala wa mkoa wa Dares Salaam akiinua mkono kuuliza swala katika
semina ya mawakala wa m-pesa wa mkoa wa Dares Salaam iliyoandaliwa na
Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao kwa ajili ya kutoa huduma
bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina hiyo ilifanyika kwa siku mbili
katika ukumbi wa Karimjee jijini.
Baadhi
ya Mawakala wa m-pesa wa Mkoa wa Dares Salaam waliohudhuria katika
semina iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao
kujifunza namna ya kutoa huduma bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina
hiyo ilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Karimjee jijini
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania imefanya maboresho makubwa katika mfumo unaondesha huduma ya
Vodacom m-pesa kwa lengo la kuendana na kasi ya ukuaji na mahitaji ya
huduma hiyo katika soko nchini.
Maboresho hayo sasa yanawawezesha wateja wa Vodacom m-pesa kufanya miamala yao kwa ubora na kasi ya hali ya juu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza amesema maboresho hayo
makubwa yamefanyika Disemba mwaka jana ili kuuongeza nguvu na ufanisi
mfumo wa mawasiliano unaotumika kutoa huduma za Vodacom m-pesa.
“Tumefanya
maboresho kama ilivyodesturi yetu ya kuboresha na kuimarisha huduma
zetu mara kwa mara. Tunatambua kwamba wateja wa Vodacom m-pesa walikuwa
wanakabiliwa na changamoto za hapa na pale ninayo furaha kubwa kuona
kwamba tunaendelea kuiboresha huduma hii”Alisema Bw. Meza
Bw.
Meza amesema katika kipindi chote cha mwishoni mwa mwaka huduma ya
m-pesa imepatikana kwa kasi na ubora zaidi na hivyo huduma ya m-pesa
kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kubadili maisha ya wananchi kupitia
teknolojia ya simu ya mkononi.
“Wakati
wote tunaishi na dhamira yetu ya kutoa huduma bora na kujali mahitaji
ya wateja wetu tutaendelea kufanya hivyo mara kwa mara sambamba na
kutoa kipaumbele cha kuhakikisha usalama huku tukiongeza pia kasi ya
ubunifu na uvumbuzi wa huduma bora”. Alisema Bw. Meza
“Huduma
ya Vodacom m-pesa imekuwa kiungo muhimu cha maisha ya wananchi mijini
na vijijini imezalisha ajira, imerahisisha maisha na biashara ni kiasi
cha kupiga *150#00 kutoka mtandao wa Vodacom na kuanzia hapo
kiganja cha mkono kinakusogeza karibu na ndugu jamaa na watoa huduma
mbalimbali.” Bw.Meza aliongeza.
No comments:
Post a Comment