



Na Zahira Bilal Maelezo Zanzibar
Waziri
wa kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika Haroun Ali Suleiman
amesema kuwa idadi ya vyama vya ushirika vinavyoaandikishwa imekuwa
ikiongezeka na kwamba vyama hivyo vimekuwa vikiongezewa nguvu ya
usimamizi na utaalamu.
Hayo
aliyasema leo wakati akijibu swala la Mwakilishi wa nafasi za
wanawake Salma Mussa Bilali alietaka kujua hatua zinazochukuliwa na
wizara katika kuimarisha vyama vya ushirika wilayani huko katika ukumbi
wa baraza la wakilishi chukwani
Waziri
Haroun alisema kuwa zoezi la kukusanya takwimu za vyama
litakapokamilika litasaidia kujua mahitaji ya wataalamu na watendaji
kwa ujumla
Aidha
alisema wizara yake inajitahidi kujipanga ili kuweza kuimarisha
utendaji wilayani na katika vitengo maalumu vya idara ya ushirika pia
kusimamia mpango wa mafunzo kwa maofisa wa ushirika wa ngazi mbali
mbali ili kuongeza utaalamu na uwezo wao wa kuhudumia vyama vya
ushirika kwa ufanisi zaidi
Alisema
wizara yake inampango wa kuanzisha vituo vya stadi maalumu kwa ajili
ya kutoa elimu kwa washirika na kuweza kuimarisha vyama vya ushirika
kwa kila wilaya
Alisema
kufanya hivyo inaweza kuondoa usumbufu wa tatizo la ucheleweshaji
wa usajili wa vyama vya ushirika na kuongeza kasi ya kukagua na
kupewa usajili kwa haraka
Sambamba
na hayo alisema kufanya hivyo ni kuwawasaidia wananchi wa mijini na
vijijini kupata ajira na kuwaondoshea umasikini na ndio malengo ya
wizara hiyo







No comments:
Post a Comment