Mechi
kati ya Toto Africans na African Lyon ambayo kwa mujibu wa ratiba
ilikuwa ichezwe Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza haitakuwepo, na sasa
itapangiwa tarehe nyingine.
Juzi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilipokea barua kutoka kwa
wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba ikieleza kuwa Februari 5 mwaka huu
uwanja huo utatumika kwa sherehe za kitaifa za kuzaliwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), hivyo hautaweza kutumika kwa Februari 4, 5 na 6 mwaka
huu.
Mpaka sasa hakuna kituo cha televisheni ambacho kimeomba na kushinda
tenda ya kuonesha moja kwa moja (live) mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.
Kwa upande wa vituo vya redio, vyote vimepewa haki ya kutangaza moja
kwa moja mechi za ligi hiyo kwa masharti yafuatayo;
Kuitambulisha
ligi hiyo kwa jina lake (Ligi Kuu ya Vodacom) wakati wa matangazo hayo
ya moja kwa moja, na pia kuweka matangazo ya mdhamini (Vodacom) wakati
wakitangaza mechi husika. Hata hivyo, vituo vya redio bado
vinaruhusiwa kuendelea kutafuta/kutumia matangazo ya wadhamini wao,
lakini ambao si washindani wa kibiashara wa Vodacom.
Mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
unaanza keshokutwa (Januari 21 mwaka huu) kwa mechi nne. Moro United
itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mtibwa
Sugar itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani.
Nayo
Toto Africans itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi
mkoani Pwani na Villa Squad itapambana na Kagera Sugar katika Uwanja
wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
Januari
22 mwaka huu JKT Ruvu na Polisi Dodoma zitapepetana Uwanja wa Azam
Chamazi wakati Januari 22 mwaka huu Dar es Salaam itakuwa na mechi
mbili; African Lyon na Azam (Uwanja wa Azam Chamazi) na Simba na Coastal
Union (Uwanja wa Taifa).
Ratiba
kwa ajili ya waamuzi na makamishna kwa mechi 35 za mwanzo tayari
imeshatoka. Waamuzi wa kati 16 wameteuliwa kuchezesha mechi hizo huku
watatu wakiwa wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA).
Makamishna
ni 28 huku watathmini wa waamuzi (referees assessors) wakiwa kwenye
mechi tano. Watathmini hao ni Charles Mchau, Soud Abdi, Emmanuel Chaula,
Army Sentimea na Joseph Mapunda.
No comments:
Post a Comment