Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Wafanyabiashara wakiwemo wawekezaji wa kigeni waliopo hapa nchini,
wameonywa kuacha mtindo wa kusafirisha fedha nyingi kutoka eneo moja
hadi lingine pasipo na ulinzi wa Polisi.
Onyo
hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Shamsi Vuai
Nahodha, wakati akizungumza na wawekezaji wenye Mahoteli katika Fukwe za
Bahari ya Hindi na Hifadhi ya Mjini Mkongwe mjini Zanzibar.
Waziri
Nahodha amesema kuwa pamoja na kuwapo kwa usalama na amani hapa
nchini, lakini hali hiyo isiwafanye watu wakajiamini na kusafirisha
fedha nyingi pasipo na ulinzi wa kutosha ili kuepuka kuporwa na
majambazi.
Akizungumzia
Utalii Mh. Nahodha amesema kuwa kwa kutambua kuwa utalii ndio chanzo
kikubwa cha uchumi wa Zanzibar na taifa kwa ujumla, Serikali
itahakikisha kuwa inaweka miundombinu ya kutosha kiusalama ili kuondoa
matishio yoyote kwa wageni wanaoitembelea nchi yetu kwa shughuli
mbalimbali zikiwemo za kitalii.
Aidha
amesema ili kuhakikisha usalama zaidi, wawekezaji hao hawanabudi
kulitumia Jeshi la Polisi katika kufanya uchunguzi kwa watu wanaotaka
kazi kwenye maeneo yao ili kuepuka kuajiri watumishi wasio waaminifu.
“Mnapotaka
kuwaajiri wafanyakazi, wakiwemo walinzi kwenye maeneo yenu,
hakikisheni kuwa mnaowapa nafasi hizo ni vijana wa maeneo jirani ambao
wengi wao wanafahamika kwa sura na tabia kulikoni kutoa watumishi mbali
ambao hata kama wakifanya uhalifu na kukimbia ni vigumu kumpata”.
Alisema Mh. Nahodha.
Mh.
Nahodha ameongeza kuwa athari za kumuajiri mtu wa mbali ni kuwa hata
pale atakapofanya uhalifu na kukimbi haitakuwa rahiisi kwa Polisi
kumpata mtuhumiwa huyo kwa urahisi.
Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Wawekezaji wa Mahoteli Visiwani Zanzibar (ZATI) Zanzibar Association Tourism Industrial Bw.
Abullsamad Saidi, alisema kuwa ipo haja kwa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kusaidia kuongeza kasma ya Jeshi la Polisi Visiwani humo ili
waweze kumudu vema kazi zao zikiwemo za ulinzi wa vivutio vya kitelii
kwa wageni.
Amesema
kuwa pamoja na Jeshi la Polisi kufanya kazi zao vizuri, lakini askari
wamekuwa wakipata vikwazo kutokana na uduni na ukosefu wa vitendea kazi
kama vile usafiri na radio za mawasiliano.
Hoja
hiyo pia imeungwa mkono na Mshauri wa Rais katika Masuala ya Utalii
Bw. Issa Ahmed Othman, ambaye amesema kusipokuwa na usalama wa kutosha
kwenye maeneo ya fukwe na kuna hatari ya kukosa watalii na hivyo
kudhoofisha na kupunguza pato la taifa linalotokana na utalii.
Wakichangia
hoja kwenye mkutano huo, baadhi ya wawekezaji waliiomba Serikali kuwa
na bajeti ya kutosha katika kulinda maeneo ya vivutio vya kitalii.
Bibi Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika akiwalisha kieki
wajukuu zake katika hafla yake iliyofanyika jijini Dar es Salaam wakati
al,ipotimiza miaka 75 ya kuzaliwa kwake
Bibi
Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika akifurahia na kushangiliwa
na marafiki, watoto na wajukuu zake kwa kutimiza miaka 75 iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) na Chuo cha Polisi cha Kimataifa cha Moshi (CCP) wameingia makubaliano ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo vya vijana.
Katika Makubaliano hayo yaliyofikiwa mwezi August, 2011, TPBC na CCP watashirikiana
kuchagua vijana wenye vipaji vya mchezo wa ngumi na kuwaendeleza ili
waweze kucheza michezo ya majeshi pamoja na mashindano mengine ndani na
nje ya Tanzania.
Makubaliano haya yamekuja wakati
ambapo Tanzania inahitaji msukumo mkubwa kwenye medani ya michezo ili
kuweza kufufua ari na moyo wa michezo kama ilivyokuwa katika miaka ya 70 na 80.
Aidha, Makubaliano haya yana lengo la kuandaa jeshi zuri la wanamichezo hodari watakaoleta sifa jeshi la Polisi pamoja na Tanzania
kwa ujumla. Tayari vijana wengi wanafanya mazoezi katika kambi (Gym)
ya ngumi ambayo imewekwa katika viwanja vya michezo vya CCP. Kambi hiyo
inawashirikisha pia vijana kutoka maeneo mengine mkoani Kilimanjaro
ambao sio Polisi.
Katika kusimamia hili, Rais wa TPBC Onesmo Ngowi akishirikiana na Afisa Mipango na Utawala wa CCP Superintendent of Police, Lutusyo Mwakyusa
watahakikisha kuwa vifaa muhimu vinapatikana pamoja na mazingira ya
kufanyika mazoezi na upatikanaji wa wataalam wanaotakiwa wanapatikana.
Naye Superintendent of Police, Yahya Mdogo ambaye ni Afisa wa Michezo katika Chuo cha Polisi cha Kimataifa Moshi ataangalia kwa karibu mwenendo mzima wa mahitaji ya kila siku ya mazoezi.
Tayari TPBC imeshatoa
vifaa muhimu vya mazoezi pamoja na wataalam (Makocha) wa kuwafundisha
mabondia hao wako katika sehemu ya mazoezi. Vijana wengi ambao
walikuwa hawana kazi au mahala pa kwenda wakati wa saa za jioni kwa
sasa wanafanya mazoezi na wenzao katika uwanja wa CCP.
Aidha, baadhi ya mabondia kutoka
katika mkoa wa Kilimanjaro ambao walikuwa wameweka kambi katika jiji la
Nairobi nchini Kenya na Arusha wamejumuika katika kambi hii mpya.
Mabondia hao ni pamoja na Pascal Bruno anayejulikana na wengi kama "Price Kilimanjaro", Emilio Norfat, Charles Damas, Alibaba Ramadhani, Robert Mrosso, Bernard Simon na wengine wengi
Baadhi ya wataalam waliojitokeza kuwafundisha vijana hawa ni pamoja na Felix Joseph na Pius Msele ambao kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa wachezaji na makocha wa timu ya ngumi ya taifa.
Makubaliano haya ni baadhi tu ya
mikakati mipya za TPBC za kuamsha ari ya mchezo wa ngumi kwa
kuzisambaza mikoani kuliko ilivyozoeleka ngumi kufanyika katika mkoa wa
Dar -Es-Salaam peke yake.
"Kwa sasa kazi kubwa tulivyo nayo ni
kuzipeleka ngumi mikoani ambako tunaamini kuna vijana wengi sana wenye
moyo pamoja na vipaji vikubwa" alisema Ngowi.
No comments:
Post a Comment