SIMBA NA YANGA ZAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI YA VODACOM
Meneja
wa Kinywaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi
wa habari, katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF wakati kampuni ya bia ya TBL
ilipokabidhi vifaa vya michezo kwa timu za Simba na Yanga, tayari kwa
kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza
Jumamosi Januari 20 2012.
Kutoka
kulia ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah, Steven Kilinde Mkurugenzi
wa Mahusiano TBL, George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro,
Evodius Mtawala Katibu Mkuu wa Simba na Boniface Wambura Msemaji wa TFF
wakionyesha vifaa vilivyokabidhiwa ka timu ya Simba.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Kilimanjaro Steven Kilinde akikabidhi jezi kwa Katibu Mkuu wa timu ya Yanga Selestine Mwesigwa
katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Shirikisho
la mpira wa miguu nchini Tanzania leo katikati ni Meneja wa Kinywaji cha
Kilimanjaro Bw. George Kavishe na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF
Angetile Osiah.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Kilimanjaro
Steven Kilinde, Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe,
Katibu Mkuu wa timu ya Yanga Selestine Mwesigwa
na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah wakionyesha vifaa
vilivyokabidhiwa kwa timu ya Yanga katika hafla ya makabidhiano
iliyofanyika katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini
Tanzania leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batlda
Burian, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es
Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kumuaga rasmi kwenda kuanza
kazi nchini Kenya baada ya uteuzi wake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi
wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batlda Burian, wakati Balozi huyo
alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam leo Januari 19, 2012,
kwa ajili ya kumuaga rasmi kwenda kuanza kazi nchini Kenya baada ya
uteuzi wake.
H-BABA AKAMILISJA SINA RAHA NA BANZA STONE
MSANII
mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Ramadhan ‘H-Baba’
amekamilisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Sina Raha,
akimshirikisha gwiji wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja, ‘Banza
Stone’ Mwalimu wa Walimu.
Akizungumza
na Mtandao wa Sufianimafoto, H-Baba, alisema kuwa kibao hicho ni
miongoni mwa nyimbo zake 10 zitakazokamilisha albam yake mpya
itakayokwenda kwa jina la ‘Shika hapa acha Hapa’ inayotarajia kuingia
sokoni mwezi wa tatu mwaka huu.
Aidha
alisema kuwa wimbo ambao amemshirikisha Banza Stone, amerokodia katika
Studio ya Allan Mapigo, ambapo tayari amekamilisha maandalizi ya
kurekodi video ya wimbo huo mwishoni mwa wiki hii.
H-Baba
alisema kuwa katika wimbo huo mashabiki wake watarajie kupata vitu
tofauti ikiwa ni pamoja na staili mpya na midundo iliyo ‘shiba’ na sauti
murua ya Banza Stone, aliyeonyesha uwezo wake katika wimbo huo.
Alizitaja
studio alizorekodia nyimbo zake zitakazokamilisha albam hiyo kuwa ni
pamoja na KGC Studio, Maneke Studio na Allan Mapigo, zote za jijini Dar
es Saam.
Pia
alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwamo katika albam hiyo kuwa ni
pamoja na, Nipe Kidogo, Shika Kichwa, Kinacho Niumiza, Zaidi yako Wewe
na Nimpende Nani.
No comments:
Post a Comment