Posted: 31 May 2012 12:16 AM PDT
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla (kushoto)
akimkabidhi bendera nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja Dar es Salaam
jana ajili ya kwanda nayo Ivory Coast kuipeperusha katika mechi ya
kufuzu Kombe la Dunia 2014 wa pili kushoto ni Meneja wa bia ya
Kilimanjaro, George Kavishe ambao ni wadhamini wa timu hiyo, Kocha Mkuu
Kim Poulsen na katikati ni Mwenyekiti wa BMT, Deoniz Malinzi. Picha na
Rajabu Mhamila.
|
Posted: 30 May 2012 11:03 PM PDT
Rais
Jakaya Kikwete na mgeni wake, Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast
wakiangalia shamba la kahawa mkoani Arusha jana. Ouattara yupo nchini
kuhudhuria mkutano wa Magavana wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB),
unaoendelea Ngurdoto. (Picha na Ikulu)
|
Posted: 30 May 2012 11:00 PM PDT
Na Yusuph Mussa, Lushoto
NAIBU
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bw. January Makamba
amewataka wananchi wa Tarafa ya Mgwashi mkoani Tanga kutumia fursa
mbalimbali ikiwemo kufanya biashara na Halmashauri mpya ya Bumbuli
badala ya kuwaachia wageni waiuzie halmashauri hiyo hadi karatasi za
ofisini.
Chanamoto hiyo aliitoa
juzi wakati anahutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha
Mgwashi Kata ya Mgwashi wilayani Lushoto na kuwaeleza wananchi kuwa kwa
kupata halmashauri ni ushindi mkubwa kwani pamoja na kufanya biashara,
lakini pia huduma za jamii zitaboreka.
"Nitashangaa kama nitaona
hata biashara ya kuuza karatasi (shajala) mtawaachia watu kutoka Arusha.
Sasa ni wakati wenu kufanya biashara na Halmashauri ya Bumbuli kwa
kuchukua zabuni mbalimbali ili kuinua vipato vyenu," alisema Bw.
Makamba.
Bw. Makamba aliwatahadharisha wananchi wa tarafa hiyo
kuwa uteuzi wa yeye kuwa Naibu Waziri hauwezi kumaliza changamoto zao
bali ataendelea kupigana kama Mbunge kuona kero mbalimbali zikipatiwa
ufumbuzi moja baada ya nyingine.
"Jamani mimi nilipokuja hapa
niliomba kazi ya ubunge. lakini sio uwaziri, hivyo nafasi yangu ya
unaibu Waziri hauwezi kumaliza kero na changamoto zenu, bali kama
nilivyopigana kama mbunge wenu wa kupata umeme tangu dunia iumbwe kwenye
Tarafa ya Mgwashi.
"Ndivyo nitakavyo hakikisha barabara ya
kutoka Mbelei hadi Mashewa inatengenezwa huku ikihamishiwa kutoka
halmashauri kwenda TANROADS (Wakala wa Barabara) ambayo itawezesha
kusafirisha mazao yenu, lakini pia tatizo la maji linakwisha," alisema Bw. Makamba.
Awali,
Ofisa Tarafa ya Mgwashi Bw. Moka Urban alimueleza Bw. Makamba ambaye
pia ni Mbunge wa Bumbuli kuwa Kituo cha Afya Mgwashi kinaletewa dawa
kama kata badala ya kituo cha afya, hivyo kusababisha usumbufu kwa
wananchi.
Bw. Urban alisema pia barabara ya kutoka Soni hadi
Mgwashi sio nzuri, umeme bado haujafika kwenye vijiji vingi pamoja na
kufika makao makuu ya kata ya Mgwashi na baadhi ya vijiji havina
mawasiliano ya simu.
|
Posted: 30 May 2012 10:59 PM PDT
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Lazaro Nyalandu akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana, kuhusu hali ya
usalama Visiwani Zanzibar baada ya Serikali kudhibiti vikundi vya watu
waliosababisha vurugu na kukanusha taarifa ya baadhi ya vyombo vya
habari vya nje vilivyoripoti habari za kupotosha watalii. Kushoto ni
Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Bw
Richard Rugimbana. (Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 30 May 2012 10:57 PM PDT
Baadhi
ya watuhumiwa waliokamatwa wakati wa operesheni maalumu ya kukagua mita
za LUKU za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakiwa chini ya ulinzi
wa polisi baada ya kukamatwa eneo la Tabata, Dar es Salaam jana. Hata
hivyo waliachiwa baada ya kubainika kuwa si wahusika. (Picha na Prona
Mumwi)
|
Posted: 30 May 2012 10:54 PM PDT
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma, Bi. Moza Said (katikati) akiangalia maji ya kusafishia udongo wenye dhahabu katika machimbo mapya ya Tumbelo wilayani Kondoa jana. (Picha na Peter Mwenda)
|
Posted: 30 May 2012 10:52 PM PDT
Wakazi
wa Jiji la Dar es Salaam, wakichagua nguo na mabegi ya kuhifadhia nguo
katika Soko la Karume, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala jana.
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo wameahidi kuhamia kwenye jengo la
biashara la Machinga Complex iwapo amri ya kuhama itatekelezwa
ipasavyo. (Picha na Peter Twite)
|
Posted: 30 May 2012 10:35 PM PDT
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Kanda ya Ziwa, Bw. Patrick
Kisaka, akikabidhi Bajaj kwa mshindi wa promosheni ya Vumbua Hazina
Chini ya Kizibo juzi, Bw Godfrey Shao mkazi wa Mkoa wa Mwanza
aliyeshinda kupitia bia ya Tusker Lager. (Na Mpigapicha Wetu)
|
Posted: 30 May 2012 10:33 PM PDT
Na Esther Macha, Mbeya
LICHA ya Serikali kupiga vita ajira kwa watoto hususan wanafunzi bado tabia
hiyo inaendelea kwa wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambapo
kundi hilo la watoto limeshindwa kuhudhuria masomo kwa kufanya kazi
katika mashamba mbalimbali wilayani humo.
Hayo yalibainishwa hivi karibuni wakati mwandishi wa habari hizi alipotembelea mashamba ya mpunga, vitunguu na nyanya yaliyopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Wakizungumzia ajira hizo wanafunzi hao walisema, wanalazimika kufanya kazi hizo kwa malipo ya sh. 200 kwa kila 'kijaruba' hata katika muda wa masomo ili kujikwamua kimaisha.
Hatua hiyo ambayo imekuwa ikipigwa vita na vyombo vya habari na vile vinavyotetea haki za watoto bado wazazi wameendelea kuwaanchia huru watoto wao, ambao hutoroka shule na kujishughulisha na kazi za vibarua katika mashamba ya mazao mbalimbali.
Watoto hao waliokutwa katika ajira hizo ni wale wanasoma darasa la saba na darasa la tano ambao kwa mujibu wao wanalazimika kufanya vibarua hivyo ili waweze kupata michango ya shule kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwasaidia.
Walisema,
hupewa kazi hizo na wakulima kwa kukwepa gharama kubwa na kuwa
wanashindwa kuwapatia vibarua watu wazima ambao huhitaji kiasi kikubwa
cha fedha.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Igomelo Bi.Mima Mkiramweni alisema kuwa tatizo hilo lipo kwa baadhi ya wanafunzi ambao wanakosa mahitaji kutoka kwa wazazi wao na hivyo hutoroka shuleni ili kufanya kazi hizo.
“Hawa wakulima na wafanyabiashara ambao wanatoa ajira mbaya kwa watoto kwa kiasi kikubwa wanasababisha kushuka kwa kiwango cha elimu shuleni hapa, hili si jambo zuri,”alisema Mwalimu huyo.
Akizungumzia kuhusu mrundikano wa wanafunzi darasani Bi. Mkiramweni alisema, kila darasa lina wanafunzi 100 mpaka 121 hali ambayo inasababishwa na ukosefu wa vyumba vya madarasa na hivyo kufanya ufundishaji kwa walimu kuwa mgumu kwa wanafunzi.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Igomelo wa darasa la saba Frank Mbuna alisema, katika darasa lao wapo wanafunzi 121 hali ambayo inawaathiri katika taaluma zao.
Kwa upande wake Ofisa Elimu Shule ya Msingi Wilaya ya Mbarali Bi. Rustika Turuka alisema, kitendo cha wanafunzi kufanya vibarua kipindi cha masomo ni kibaya kwani kinashusha kiwango cha elimu kwa watoto wilayani humo.
Bi. Turuka alisema serikali ilikataza ajira mbaya kwa watoto kwa kuwatumikishwa kwenye mashamba, na kuwataka wazazi wasaidie kupiga vita ajira hizo kwa watoto Wilayani humo
|
No comments:
Post a Comment