Posted: 01 Jun 2012 12:21 AM PDT
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akipongezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dkt. Donald Kaberuka (kulia) mara baada
ya hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo
Afrika (AfDB) Mjini Arusha jana. Katikati ni Rais wa Ivory Coast Dkt.
Alassane Ouattara. (Picha na Ikulu)
|
Posted: 01 Jun 2012 12:17 AM PDT
Na Zahoro Mlanzi KAMPUNI ya ZUKU imedhamini Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF) kwa dola milioni moja kwa miaka 10 kwa lengo la kusaidia kukuza filamu ambapo kwa mwaka huu limepangwa kuanza Julai 7 mpaka 15, mwaka visiwani Zanzibar. Akizungumza Dar es Salaam juzi usiku katika sherehe maalumu za kusherehekea kutimiza miaka
15 tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo na kutangaza rasmi udhamini huo,
Mwenyekiti wa Wanachi Group, Ali Mafuruki alisema lengo la kudhamini
tamasha hilo kwa muda huo ni kuhakikisha wanalitangaza zaidi kimataifa
huku wasanii husika wakinufaika nalo. Alisema tamasha hilo
litakuwa la aina yake kwa Afrika, kazi za wasanii hao watazitangaza
duniani kote kupitia wasambazaji wao wa ZUKU Pay TV ambapo kwa hivi sasa
wameenea katika Ukanda wa Afrika Mashariki na lengo lao ni kuenea
zaidi. Aliongeza kwamba anajua watu watakuwa na maswali mengi kwa nini wameamua kudhamini ZIFF,
hata hivyo alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na sasa ni wakati wa
wasanii kunufaika na kazi zao, kwani kwa kipindi kirefu wamekuwa
wakilia kutoona matunda ya kazi zao. Alisema ni lazima wabadili dhana za wasanii hao kwa kuhakikisha wanafanya kazi zenye ubora zaidi, ambapo zitasababisha kuwapa wao kiburi cha kuzidi kutangaza katika mabara mengine. Naye Mwenyekiti wa ZIFF, Mahmoud Thabit Kombo aliishukuru kampuni hiyo kwa udhamini wao na kwamba ana imani mambo mazuri yatazidi kuja katika tamasha hilo kupitia kampuni hiyo. Alisema huo ni mwanzo mzuri wa ushirikiano waliounzisha na kwamba wao ndiyo watakuwa wadhamini wakuu, lakini watu wengine wanafunguliwa milango kudhamini tamasha hilo kwani lengo ni kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao. Mwenyekiti
huyo alisema tamasha hilo lilikuwa linakabiliwa na changamoto nyingi
hasa katika masoko, udhibiti wa hakimiliki ambapo kutokana na kuingia
kwa ZUKU ana uhakika matatizo hayo yatapungua.
|
Posted: 01 Jun 2012 12:16 AM PDT
|
Posted: 01 Jun 2012 12:11 AM PDT
Na Patrick Mabula, Kigoma WANANCHI
wa Wilaya mpya ya Kakanko mkoani Kigoma wametakiwa kutumia fursa za
mipango ya Serikali katika kilimo ili kujikwamua na umaskini na
kujiletea maendeleo. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Bw.
Christopher Chiza ambaye pia ni Mbunge wa Buyungu Wilaya ya Kakonko
aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutobweteka na badala yake kuzitumia
fursa za mipango ya Serikali katika kilimo. Akihutubia
wananchi wa wilaya hiyo hivi karibuni Bw. Chiza alitoa onyo kwa
watumishi watakaopangwa kufanya kazi wilayani humo kuhakikisha
wanawatumikia wananchi katika mipango kupitia fursa za Serikali. Alisema,
Wilaya ya Kakonko ina fursa mbalimbali katika kilimo, hivyo asingependa
kuona mtumishi wa umma akifanya kazi kinyume na maelekezo na watu
kubweteka badala ya kuchangamkia fursa hizo ili kujikwamua na umaskini, kujiongezea kipato na kupata maendeleo. "Ndugu
zangu viongozi na wananchi wa Kakonko, nafurahi sana kuona mmeacha
itikadi za kisiasa na kujikita katika masuala ya maendeleo, nami naitaka
Serikali kuhakikisha inateua watumishi waaminifu na siyo walarushwa,"
alisema Waziri Chiza. Katika kuwasaidia wananchi wa Kakonko
kujikwamua na umasikini, alisema amekuwa akisisitizia kilimo cha mazao
mbadala ya chakula na biashara ikiwemo mpunga, kahawa, alizeti na ufuta. Kwa
upande wake Ofisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya ya Kibondo Bw. Omar Bori,
alisema Kakonko ina fursa nyingi hasa katika kilimo kwa sababu mazao
mengi ya chakula na biashara hustawi vizuri na kuwaomba wananchi
kuzitumia fursa hizo. ********** Washauriwa kuwajengea uwezo watoto yatima Richard Konga na Queen Lema, Arusha JAMII
zimeshauriwa kuachana na uchangiaji wa shughuli za hanasa badala yake
ijikite zaidi kuyajali makundi yasiyojiweza hususan watoto yatima na
wenye maambukizi ya Ukimwi wanaolelewa bila msaada wa uhakika kwenye
vituo vya watoto yatima. Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa
Kikundi cha Mshikamano cha jijini Arusha Bw. Godilizeni Temba wakati
kikundi hicho kilipotembelea na kutoa msaada wa vyakula na vinywaji
wenye thamani ya shilingi milioni moja kwa vituo viwili vya kulelea
watoto yatima mjini hapa. Vituo hivyo ni pamoja na Sant Lusia
kilichopo Moshono kinacholea watoto wenye maambukizi ya ukimwi pekee na
Kituo cha Sant Joseph kilichopo Kata ya Mlangarini wilayani Arumeru. Bw.
Temba aliwaomba Watanzania kujijengea utaratibu wa kujisaidia wenyewe
na kuachana na dhana iliyojijenga ya kutegemea wafadhili pekee kutoka
nje ya nchi ambao wengi wao wamekuwa wababaishaji huku wakiweka masharti
magumu na misaada yao. Aidha, alisema jamii ina kila sababu ya
kuguswa na tabu wanayoipata watoto yatima kwani mbali na kukabiliwa na
changamoto nyingi kimaisha wamekosa msaada muhimu ya kijikimu hususan
elimu bora itakayowasaidia kuondokana na utegemezi hapo baadaye. Pia
alitoa rai kwa kila Mtanzania kwamba jukumu la kuyasaidia makundi hayo
ni wajibu wa kila mtu iwapo ataguswa na kujitolewa hata kwa kuchangia
mtoto mmoja kila mwaka ikiwepo kumsombesha na kuachana na uchangiaji
mkubwa wa hanasa ambao umekuwa ukipoteza fedha nyingi kwa muda mfupi. "Suala
la kuwasaidia watoto ni jukumu la kila mtu ni vizuri basi kwa kila
Mtanzania, iwapo ataguswa kwa namna yake na kutoa mchango kwani wengi
wetu tumekuwa tukijitoa sana kuchangia harusi za kifahari, bila kujali
kuwa michango yetu pia inahitajika kwa makundi mengine muhimu," alisema Naye
Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima cha St.Lucia Bi. Winfrida Mrema alisema
kuwa kituo chake kinalea watoto wenye umri wa miaka mwili hadi 10 wenye
maambukizi ya VVU na kimekuwa kikikabiliwa na changamoto kubwa ya
upungufu wa lishe bora kwa watoto hao. Aidha, kwa upande wa
mmiliki wa Kituo cha St.Joseph Sister Crispin Mnate alisema kuwa kituo
hicho kina jumla ya watoto yatima 46 na wamekuwa wakilelewa katika
mazingira magumu kutokana na kukosa ufadhili wa kudumu.
|
Posted: 01 Jun 2012 12:09 AM PDT
MAPAMBANO Mkazi
wa jiji (kushoto) akijaribu kujinasua mara baada ya kufungwa pingu na
askari aliyevaa kiraia (kulia) kwa tuhuma za kupigana hadharani, kama
walivyokutwa makutano ya Barabara za Uhuru na Msimbazi Dar es Salaam
jana. (Picha na Rajabu Mhamila)
|
Posted: 01 Jun 2012 12:07 AM PDT
Na John Gagarini, Kibaha JUMLA ya kaya 2,331 zinazoishi kwenye mazingira magumu wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani zimenufaika na Mpango wa Uhawilishaji Fedha kwa kaya hizo kwa kupatiwa kiasi cha sh. milioni 239.8. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF) Wilaya ya Kibaha Bw. Harry Godson alisema kuwa mpango huo wa kuzipatia kaya duni ulikuwa wa majaribio na utafikia mwisho Julai mwaka huu. Bw. Godson alisema kwamba, mpango huo umeonesha mafanikio makubwa kwenye vijiji 12 katika kata sita ambazo ni Tumbi, Soga, Kikongo, Kwala, Magindu na Gwata kwa kuwa walengwa ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 na watoto chini ya miaka 18 wanaosoma shule za msingi pia watoto chini ya miaka mitano. “Kila kaya inapatiwa shilingi 10,200 kwa wazee na watoto 5,001 kila mwezi, kwa walengwa walio kwenye mradi huo unaotekelezwa kwenye wilaya tatu nchini ambazo ni Kibaha, Bagamoyo za Mkoa wa Pwani na Chamwino mkoani Dodoma,” alisema Bw. Godson. Alisema
kuwa, masharti wanayopewa kwa wazee ni kuhudhuria kliniki japo mara
moja kwa mwaka, watoto chini ya miaka 18 wanaosoma shule za msingi
wahudhurie darasani angalau kwa asilimia 80 kwa mwaka na watoto chini ya miaka mitano wapelekwe kliniki mara sita kwa mwaka. “Katika mpango huu tumepata mafanikio makubwa kwa walengwa ambapo wazee wameweza kupata matibabu na kutibu magonjwa yaliyokuwa yakiwasumbua, ufaulu wa wanafunzi umeongezeka na mahudhuria yamekuwa juu, kipato cha kaya kimeongezeka na uchumi wa vijiji husika nao umepanda,” alisema Bw. Godson. Naye
Mratibu wa mpango huo Bw. Costa Kauki alisema kuwa mbali ya mafanikio
pia wamekumbana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na umbali wa
benki kwa ajili ya kuhifadhia fedha, baadhi ya kaya zisizostahili kuwa
kwenye mpango huo kutaka kujumuishwa. “Kaya zinazonufaika na mpango huu ambao sasa utakuwa wa nchi nzima na vijiji vilivyosalia, ni zile ambazo zina kipato duni, kula mlo mmoja, kushindwa kupeleka watoto hospitali, shule na kushindwa kuwahudumia,” alisema Bw. Kauki. Bw. Kauki alisema kuwa watu wanaonufaika hutambuliwa kupitia kamati ya mradi na baadaye hupitishwa na mikutano mikuu ya kijiji husika ambao wao wanawatambua hata hivyo mradi huo unafadhiliwa na wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na Serikali Kuu.
|
Posted: 31 May 2012 11:55 PM PDT
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dkt. Terezya Huvisa
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana
kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
itayofanyika Juni 5 mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira wa Ofisi
ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu. (Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 31 May 2012 11:51 PM PDT
Na Mwandishi Wetu, Maili Moja WAKAZI
wa Mtaa wa Ungindoni Kata ya Maili Moja wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani
wameiomba Halmashauri ya Mji wa Kibaha kuifanyia matengenezo Barabara ya
Sheli Maili Moja Shule ya Msingi ambayo haijatengenzwa tangu mwaka 2009
hivyo hawaoni sababu ya kuendelea kuibua miradi mipya. Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti mjini Kibaha jana,
wakazi hao walisema kuwa barabara hiyo imekuwa ikipitika kwa shida
kutokanana mashimo mengi na kipindi cha mvua hali imekuwa mbaya zaidi. Walisema kuwa, waliibua mradi wa barabara kwenye mkutano wa mtaa ikiwa kama ni kero na kupeleka halmashauri kwenye bajeti ya mwaka 2010 na kuandika barua ya kukumbushia bajeti ya miaka miwli iliyofuata, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika. “Ilifika
wakati tukajichangisha fedha kwa ajili ya kukarabati sehemu korofi,
kwani barabara ilikatika kabisa na kukawa hakuna mawasiliano kabisa,
lakini wananchi tulijitolea na kuweka kalavati na kurejesha
mawasiliano,” Alisema Bw. Mussa Juma miongoni mwa wakazi hao. Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Geofidor Nombo alisema kuwa wananchi waliibua mradi huo wa barabara hiyo na kupeleka sehemu husika ikiwa ni pamoja na vikao vya kata na halmashauri, lakini toka wakati huo hawajafanikiwa. “Tuliandika
barua za kukumbushia kwenye bajeti za mwaka 2011 na 2012 ambapo
wananchi walisema hawataibua miradi mingine hadi huo utakapotekelezwa
kwani ni kero kubwa kwao,” alisema Bw. Nombo. Naye Mhandisi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bw. Ezekiel Kunyaranyara alisema kuwa, kwenye bajeti inayoishia Juni mwaka huu barabara hiyo haijatengewa fedha zozote. “Barabara hiyo imetengewa fedha kwenye bajeti ya mwakani, ambapo kiasi cha shilingi milioni mbili na barabara hiyo ina urefu wa kilomita mbili na itajengwa kwa matengenezo ya kawaida yaani kiwango cha changarawe,” alisema Bw. Kunyaranyara.
|
Posted: 31 May 2012 11:29 PM PDT
Mkuu
wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya NMB Bw. Imani Kajula (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana
wakati wa uzinduzi wa huduma mpya na promosheni ya 'Jenga Maisha yako na
NMB', itayowawezesha wateja wote watakaofungua akaunti na kuongeza
amana kwenye NMB Bonus watajishindia tani 1 ya saruji na zawadi
mbalimbali. Kushoto ni Meneja Masoko , Bw. Shilla Senkoro na Meneja
Amana. (Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 31 May 2012 11:27 PM PDT
Na Israel Mwaisaka, Mbeya SERIKALI
ya wilayani ya Kyela Mkoa wa Mbeya imesema haitawavumilia waganga na
wauguzi watakaoshindwa kutoa huduma sahihi kwa wazee kufuatia tamko la
Waziri Mkuu la kutaka wazee wote nchini watibiwe bure. Katibu
Tawala wa wilaya hiyo Bw. John Komba aliyasema hayo kwa niaba ya Mkuu
wa Wilaya ya Kyela Bi. Magreth Malenga kwenye mkutano maalumu
uliowashirikisha waganga na wauguzi wafawidhi wa hospitali, vituo vya
afya na zahanati. Mkutano huo ulioandaliwa na Asasi ya SWOLO ili
kuweza kuzungumza kwa pamoja na kujua nini tatizo la Wazee kushindwa
kupata matibabu bila malipo wakati serikali ilishatoa tamko. Baada
ya mkutano huo, alisema hatarajii tena kusikia malalamiko kutoka kwa
wazee juu ya kutopata matibabu kwa sababu hawana pesa na kuwa kama kuna
mtumishi wa afya anaona hawezi kutoa huduma kwa wazee bure, kama sera
inavyoeleza ni bora akaiacha kazi hiyo ili wabaki waganga na wauguzi
watakaoitekeleza sera hiyo ya serikali. "Sioni sababu ya mtumishi
wa afya kununa kwa sababu mzee anapewa huduma bure, kwani hiyo ni haki
yake na dawa ni za Serikali wala siyo zake, sasa kama wapo watumishi wa
aina hiyo basi watupishe kabla hawajachukuliwa hatua kali za kisheria,"
alisema. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya Bw. Festo Ndugange alisisitiza kuwa
huduma bure kwa wazee ni utaratibu uliowekwa na Serikali, hivyo ni
lazima watumishi hao wa afya kuona wazee kupata huduma bila malipo ni
haki yao. Alisema, ofisi yake ilishatoa waraka kwenda katika
hospitali, vituo vya afya na zahanati zote juu ya agizo hilo na kusema
kama kuna mtumishi anakwenda kinyume na agizo hilo hatavumiliwa kwa
kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi.
Alifafanua kuwa, wazee wamelitumikia taifa hili kwa muda mrefu
na baadhi ya matunda wanayofaidi wauguzi yametokana na wazee hao, hivyo
ni lazima wakaenziwa kama Serikali yenyewe ilivyowatambua. Mkurugenzi
wa Shirika la SWOLO linalojishughulisha na utetezi kwa wazee mkoani
Mbeya Bw. Abel Ambakisye alisema lengo la kuitisha mkutano huo ni kutaka
kuweka maazimio ya pamoja kuhusu matibabu ya wazee bila malipo ikiwa ni
pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo na namna ya kuzitatua.
|
Posted: 31 May 2012 11:26 PM PDT
Mkazi
wa jiji ambaye (hukutaja jina) akiwa amebeba maboksi zilizotumika
ambazo huziuza kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao hatumia kuhifadhia
samaki kwenye Soko la Samaki la Kimataifa la Feri, kama alivyokutwa eneo
hilo, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 31 May 2012 11:25 PM PDT
Richard Konga na Queen Lema, Arusha JAMII
zimeshauriwa kuachana na uchangiaji wa shughuli za hanasa badala yake
ijikite zaidi kuyajali makundi yasiyojiweza hususan watoto yatima na
wenye maambukizi ya Ukimwi wanaolelewa bila msaada wa uhakika kwenye
vituo vya watoto yatima. Hayo
yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano cha jijini
Arusha Bw. Godilizeni Temba wakati kikundi hicho kilipotembelea na kutoa
msaada wa vyakula na vinywaji wenye thamani ya shilingi milioni moja
kwa vituo viwili vya kulelea watoto yatima mjini hapa. Vituo
hivyo ni pamoja na Sant Lusia kilichopo Moshono kinacholea watoto wenye
maambukizi ya ukimwi pekee na Kituo cha Sant Joseph kilichopo Kata ya
Mlangarini wilayani Arumeru. Bw. Temba aliwaomba Watanzania
kujijengea utaratibu wa kujisaidia wenyewe na kuachana na dhana
iliyojijenga ya kutegemea wafadhili pekee kutoka nje ya nchi ambao wengi
wao wamekuwa wababaishaji huku wakiweka masharti magumu na misaada yao. Aidha,
alisema jamii ina kila sababu ya kuguswa na tabu wanayoipata watoto
yatima kwani mbali na kukabiliwa na changamoto nyingi kimaisha wamekosa
msaada muhimu ya kijikimu hususan elimu bora itakayowasaidia kuondokana
na utegemezi hapo baadaye. Pia alitoa rai kwa kila Mtanzania
kwamba jukumu la kuyasaidia makundi hayo ni wajibu wa kila mtu iwapo
ataguswa na kujitolewa hata kwa kuchangia mtoto mmoja kila mwaka ikiwepo
kumsombesha na kuachana na uchangiaji mkubwa wa hanasa ambao umekuwa
ukipoteza fedha nyingi kwa muda mfupi. "Suala la kuwasaidia
watoto ni jukumu la kila mtu ni vizuri basi kwa kila Mtanzania, iwapo
ataguswa kwa namna yake na kutoa mchango kwani wengi wetu tumekuwa
tukijitoa sana kuchangia harusi za kifahari, bila kujali kuwa michango
yetu pia inahitajika kwa makundi mengine muhimu," alisema Naye
Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima cha St.Lucia Bi. Winfrida Mrema alisema
kuwa kituo chake kinalea watoto wenye umri wa miaka mwili hadi 10 wenye
maambukizi ya VVU na kimekuwa kikikabiliwa na changamoto kubwa ya
upungufu wa lishe bora kwa watoto hao. Aidha, kwa upande wa
mmiliki wa Kituo cha St.Joseph Sister Crispin Mnate alisema kuwa kituo
hicho kina jumla ya watoto yatima 46 na wamekuwa wakilelewa katika
mazingira magumu kutokana na kukosa ufadhili wa kudumu.
|
Posted: 31 May 2012 11:20 PM PDT
|
Posted: 31 May 2012 11:18 PM PDT
Na Mwandishi Wetu KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager, jana imetangaza
tarehe na zawadi zitakazokabidhiwa kwa wajasiriamali ambazo ni
vitendea kazi kwa walioshinda katika amshindano ya 'Wezeshwa na Safari
Lager'. Wajasiriamali hao watakabidhiwa zawadi katika matasha mbalimbali, ambayo yataandaliwa na kampuni hiyo. Akizungumza
Dar es Salaam jana Dar es Salaam Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo alisema wajasiriamali hao watakabidhiwa ruzuku zao kwenye
kanda walizofanyia mafunzo ya ujasiriamali. “Tutaandaa matamasha
ya kuwazawadia wajasiriamali wetu, ambapo tunawaalika pia
wafanyabiashara wengine wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali
wetu. “Kituo cha Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi
(kesho) katika Uwanja cha CCM Ilomba, Arusha litafanyika Juni 9 katika
viwanja vya Soweto, Mwanza litafanyika Juni 16 katika Uwanja cha
Furahisha na tutamalizia Dar es Salaam ambapo tamasha litafanyika Juni
23 kwenye viwanja vya Leaders Club,” alisema. Akielezea mchakato
wa kuwapata wajasiriamali hao, Shelukindo alisema baada ya kutangaza
kuanza kwa mashindano haya mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za
maombi 9,738 zilikusanywa. Alisema fomu hizo zilikaguliwa na
majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80
walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Shelukindo alisema
wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha
uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndiyo
waliopatiwa mafunzo. Meneja huyo alisema wajasiriamali 26
waliondolewa katika hatua hii kutokana na upungufu mbalimbali, kama
kuomba kuwezeshwa wakati biashara si za kwao na kutokuwa na biashara
inayoendelea. "Wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika
mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti
kama mafundi wa kushona nguo za aina tofauti, mafundi seremala na
magari. "Wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa
samaki, ufugaji wa kuku na kutengeneza mizinga ya nyuki, wengine ni
wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua na
teknolojia ya mawasiliano,” alisema. Bwana Shelukindo
aliwataja tena wajasiriamali watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili
kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali
watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu
Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi,
Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina J Buzuka,
Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na
Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha
Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo,
Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M.
Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa. Bwana Shelukindo aliendelea
kuwataja wajasiriamali watakaojipatia ruzuku katika kituo cha Mwanza
ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya
Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos
Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda
Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface
Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata
ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko,
Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip
Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa,
Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya
thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa. Bwana
Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki
shindano la Wezeshwa na Safari Lager, alisema “Shukrani nyingi ziende
pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima
la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee
kufurahia bia yetu”. Aliwakaribisha kuhudhuria matamasha haya na
aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea
kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la
Wezeshwa na Safari Lager baadae mwaka huu.
|
Posted: 31 May 2012 11:17 PM PDT
Meneja
wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionesha baadhi ya vifaa
vitavyokabidhiwa kwa wajasiriamali waliofuzu katika mashindano ya ruzuku
ya 'Wezeshwa na Safari Lager' Dar es Salaam jana. Na Michael Machella
|
Posted: 31 May 2012 11:13 PM PDT
Na Zena Mohamed, Aliyekuwa Bagamoyo WANACHAMA wa Chama cha Kutoa Mikopo kwa Wanawake Wajasiriamali nchini (INUKA) wamewaalani madaktari na wauguzi wanaowanyanyasa wazee na wajawazito katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani. Hayo yalisemwa jana mjini humo na Mkurugenzi wa INUKA Bw.David Msuya katika mkutano
wa kujadili vyanzo vya maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi (VVU)
kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wilayani hapa. Mkutano huo uliudhuriwa na wajumbe wa chama hicho ambapo mada zilizongumziwa ni pamoja na unyanyasaji kazini, huduma kwa wazee na wajawazito, misaada kwa watoto yatima kutowafikia walengwa na mazingira. Bw. Msuya alisema huduma za matibabu kwa wazee zimekuwa ngumu kupatikana hali ambayo imepelekea wazee hao kuelekezwa vituo vingine vya kupata huduma badala ya Hospitali ya Serikali kama ilivyohaidiwa na serikali. "Huduma kwa wazee inatakiwa itolewe bure, lakini kwa hapa wazee wanatozwa fedha na matokeo yake kuilaumu, Serikali kwajili ya mtu mmoja kutokana na wagonjwa wenyewe kalalamika kimya kimya nakutotoa taarifa sehemu husika," alisema Bw.Msuya. Pamoja na hayo aliwaasa wanachama hao kwa kushirikiana na wananchi wengine kutoa elimu jamii kwa jamii kwa ujumla ili kuweza kutatua matatizo hayo.
|
Posted: 31 May 2012 11:12 PM PDT
Na Mwandishi Wetu MASHINDANO
ya kumsaka 'Malkia wa Tabata' Miss Tabata 2012, yanatarajia kufanyika
leo katika Ukumbi wa Da’ West Park Tabata, Dar es Salaam. Akizungumza
Dar es Salaam jana mratibu wa mashindano hayo, Joseph Kapinga alisema
licha ya kumsaka Malkia huyo pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka
kwa bendi za Mashauzi Classic na Mashujaa. Mratibu
huyo alisema mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho atapewa sh.
500,000 na king’amuzi ambayo imelipiwa miezi sita yenye thamani ya sh.
800,000 iliyotolewa na Multichoice. Alisema mshindi wa pili atapata sh. 500,000, wa tatu sh. 350,000 wakati wa nne na watano kila moja atapata sh. 200,000. Kapinga alisema warembo watano wataiwakilisha Tabata kwenye mashindano ya Miss Ilala 2012. Mratibu
huyo alisema warembo wengine watakaoingia 10 bora, kila moja atapata
sh. 100,000 wakati waliyosalia watapata sh. 50,000 kila moja. Kapinga alisema mashindano hayo pia yatatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa Miss Tabata. “Mashindano
ya mwaka huu si ya kukosa, kwani yatakuwa ni ya aina yake ikizingatiwa
kwamba yatatumika kusherehekea miaka 10 tangu kuanza kuandaa Miss
Tabata,” alisema Kapinga. Alisema warembo waliyowahi kushinda mataji mbalimbali ya mashindano hayo, pia wamealikwa kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata. Mratibu
huyo alisema mashindano hayo yamedhaminiwa na Dodoma Wine, Redd's,
Integrated Communications, Fredito Entertainment, Multichoice Tanzania,
Screen Masters, Kitwe General Traders, Step In Electronics, Brake Point,
Atriums Hotel na Lady Pepeta.
|
Posted: 31 May 2012 11:12 PM PDT
Warembo
wa Miss Tabata wakiwa katika picha ya pamoja wakati ya mazoezi jana,
kujiandaa na fainali ya kumpata Miss Tabata 2012 ambayo inatarajia
kufanyika leo. Na Mpigapicha Wetu
|
Posted: 31 May 2012 11:06 PM PDT
Na mwandishi wetu BENDI
kongwe ya muziki wa dansa nchini, Msondo Ngoma ya jijini Dar es salaam
inatarajia kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya wa burudani wa Emirates
uliopo Masasi, Mtwara Juni 2 mwaka huu kwa lengo la kufanya shoo zao. Akizungumza
Dar es Salaam jana Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D'
alisema wamealikwa kwa ajili ya kutoa burudani siku ya ufunguzi wa
ukumbi huo, ambapo wamepania kutoa burudani ya nguvu. "Unajua
sisi ni Baba ya Muziki nchini, ndiyo maana wapenzi wengi wa dansi
wanahitaji burudani kutoka kwetu, tunapopata nafasi ya kwenda mikoani
tunakwenda kufanya kazi ya nguvu," alisema Super D. Alisema siku
hiyo wanatarajia kupiga vibao vyao vya zamani na vipya kwa lengo la
kuwakumbusha wapenzi wa bendi hiyo nyimbo zao, ambazo zilitamba na
kupendwa katika tasnia ya muziki wa dansi. Alivitaja baadhi ya
vibao vitakavyonogesha uzinduzi huo kuwa ni Suluhu uliotungwa na Shabani
Dede, Nadhiri ya Mapenzi (Juma Katundu) na Baba Kibene (Eddo Sanga).
|
No comments:
Post a Comment