Posted: 29 May 2012 12:06 AM PDT
Pamela Mollel na Jane Edward, Arusha
WATANZANIA
wametakiwa kujitangaza kiuchumi kupitia mkutano wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) ulioanza jijini Arusha ambao umewajumuisha marais sita
wakiwemo magavana wa nchi mbalimbali za Afrika.
Hayo
yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Dodoma Bw. Juma
Mwapachu mjini hapa ambapo alisema kuwa hiyo ni fursa ya pekee kwa
Watanzania kushiriki kikamilifu katika mkutano huo.
Bw. Mwapachu
alisema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa nchi ya Tanzania na unawajumuisha
watu mashuhuri na si vikao vya Magavana tu pia Umoja wa Mabenki ya
Biashara ya Afrika pamoja na vyombo vya habari mashuhuri.
Aliongeza
kuwa katika mkutano huo pia kuna vyombo vya kupima ubora wa uchumi wa
nchi mbalimbali na mfano Tanzania uchumi wake umekuwa ukitolea mfano
katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Alisema kuwa,
kupitia Benki hiyo pia wameweza kufadhili ujenzi wa miundombinu ya
Barabara ya Namanga hadi Arusha na bado wapo mbio kuhifadhili barabara
ya Moshi hadi Holili.
“Kweli uchumi wetu unabadilika kiharaka
sana na ukitazama mtikisiko wa kiuchumi 2008-009 ambao kweli kuna nchi
ambazo zimetikiswa kiuchumi," alisema Bw.Mwapachu
Naye Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania Bw.Richard Kasesera alisema kuwa
ni fursa adhimu ya kukuza uchumi kwa Mkoa wa Arusha na kuvitaka vyombo
vya habari kuwa chachu ya kutangaza uchumi wa Tanzania wakati huu
mkutano unapoendelea.
Aliongeza kuwa ni jambo la muhimu kwa
vyombo vya habari kuelezea matatizo ya kiuchumi na kuacha kuzipa
kipaumbele habari za vurugu za Zanzibar za vikundi vichache kwckuwa
kufanya hivyo ni kuwanyima Watanzania kupata taarifa sahihi na kuwatia
hofu wahisani.
Mkutano huo wenye kauli mbiu 'Afrika katika
Ulimwengu wa Utandawazi, Changamoto na Fursa' unafanyika kwa siku nne na
kukusanya zaidi ya washiriki 2,000.
|
Posted: 29 May 2012 12:04 AM PDT
|
Posted: 29 May 2012 12:00 AM PDT
WALI
ilikuwa ikifikirika kuwa kazi ya uuguzi ni wito, hivyo kila
anayefanyakazi hiyo ana sifa ya kuwa na ukarimu, upendo, upole na sifa
zingine. Kadri siku, miezi hadi mwaka inavyokwenda ndivyo sifa hizo zinavyotoweka. Kutokana
na ukosefu wa ajira nchini vijana wamejiamulia kujiingiza katika fani
mbalimbali licha ya kutokuwa na sifa zinazostahili kuingia kwenye fani
husika.
Hali hiyo imekuwa
ikiendelea na kusababisha ukiukwaji wa baadhi ya maadili mbalimbali na
kusababisha wananchi kuangamia na wengine kupoteza maisha. Mwishoni
mwa wiki iliyopita mwanamke Bi. Rukia Vulai, mkazi wa Magereza Manispaa
ya Mtwara alijikuta akijifungulia ndani ya pikipiki ya miguu mitatu
maarufu kama bajaji baada ya wauguzi waliokuwa zamu kumtolea lugha
chafu. Mwanamke huyo alifika kituoni hapo akiwa na uchungu mkali na
kumuomba muuguzi mmoja amsaidie kwa kumkimbiza wodini kwa kuwa tayari
dalili za kujifungua zilianza kuonekana baada ya chupa kuvunjika. Badala
ya muuguzi huyo kutakiwa kutoa huduma ya kwanza ili kuokoa maisha ya
mama huyo anadaiwa kuanza kumtolea lugha chafu mwanamke huyo na kudai
kuwa yeye hahusiki na kuwasaidia akina mama wajawazito. Imedaiwa kuwa
licha ya wagonjwa wengine waliokuwa pembeni kumbembeleza muuguzi huyo
kumsaidia mama huyo hakuweza kufanya hivyo na badala yake aliendelea
kumtolea lugha ya matusi mama huyo. Kutokana na mabishano hayo
kuendelea mgonjwa huyo aliweza kujifungua ambapo alisaidiwa na wanawake
wengine ambao walifika hospitalini hapo kwa ajili ya kupata huduma
mbalimbali na kujifungua ndani ya bajaji. Kwa kweli suala hili
limenisikitisha sana hata kama huyo muuguzi mama mjamzito alikuwa ni
adui yake kwanza alitakiwa kumpa huduma kisha uadui wake auendeleze. Wauguzi
kama hawa wamekuwa vikwazo vikubwa katika vituo mbalimbali vya afya na
hata hospitalini na kusababisha baadhi ya akimama kufariki ama watoto
wao kutokana na kukosa huduma zinazostahili. Imefika wakati sasa hakuna kuwaonea aibu wala kuwaachia wauguzi kama hawa kwa kuwa hawana huruma wala upendo kwa wagonjwa. Malalamiko
kama hayo yamekuwa yakiwapata akinamama wengi na kushindwa mahali pa
kwenda kueleza kero hizo na hata wanapokwenda kutoa malalamiko hayo
katika ngazi za juu huwaziba midogo kwa kuwadaganya kuwa kero hizo
zitatatuliwa. Hata hivyo hainiingii akilini ni kwanini wauguzi kama
hawa waendelee kuwepo kwenye hospitali zetu na kuwa kero kwa jamii, ni
bora kukawa na ofisi maalumu kwa ajili ya kupokea malalamiko ya wagonjwa
na kufanyiwa kazi na kuchukuliwa hatua zinazostahili bila kuonea haya
na kutangazwa. Ukweli ni kuwa hivi vitendo vya kuwanyanyasa wanawake
pindi wanapokwenda kujifungua vikomeshwe kwani vinawasababishia
kuathirika kisaikolojia kutokana na kuwaza kubeba tena ujauzito na
kuhofia kutukanwa. Lakini pia matukio ya unyanyasaji kwa asilimia
kubwa yamekuwa yakifanywa na wanawake ambao nao wapo katika mstari mmoja
wa harakati za kumkomboa mwanamke kimapinduzi hivyo imefika wakati sasa
tukashirikiana katika kukomesha vitendo hivyo. Nionavyo mimi ni kuwa
kama kuna wauguzi wa namna hii ni bora wapewe adhabu kali ambazo
zitasababisha wauguzi wengine kuogopa na pia kuwepo kwa timu maalumu ya
wafanyakazi wanaotembelea wodini na kusikiliza kero za wagonjwa na si
kungoja kuletewa maofisini.
|
Posted: 28 May 2012 11:57 PM PDT
Na Zahoro Mlanzi
SIKU
2 baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), kuitaka Klabu ya Yanga kufanya uchaguzi wa viongozi wapya Julai
15 mwaka huu, homa ya uchaguzi huo imeanza kupanda huku viongozi
waliowahi kuiongoza klabu hiyo, Francis Kifukwe, Godson Karigo na Ahmed
Falcon wakitajwa kuwania nafasi za juu.
Uchaguzi
huo umelazimika kufanyika tarehe hiyo kutokana na wajumbe nane wa
Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kujiuzulu huku mjumbe mwingine
kufariki, hivyo kufanya nafasi zijazwe kwa ibara ya 28 ya katiba ya
Yanga.
Viongozi hao waliamua kujiuzulu kutokana na kuona klabu
hiyo ikiendelea na malumbano kati ya uongozi uliopo chini ya Mwenyekiti,
Llody Nchunga na Wazee wa Baraza la Muafaka ambapo wazee hao walitaka
Nchunga ang'oke baada ya kudai timu imemshinda.
Kwa mujibu wa
taarifa ambazo gazeti hili imezipata kutoka Makao Makuu ya klabu hiyo,
Mitaa ya Twiga na Jangwani, zilieleza kwamba tayari kumeshaanza
kufanyika kwa vikao vya siri kati ya viongozi mbalimbali waliowahi
kuiongoza timu hiyo huku baadhi ya wanachama wakiwapigia chapuo
waliowahi kuiongoza.
“Tayari vikao vimeshaanza na kuna baadhi ya
wanachama wameanza kupanga safu zao za uongozi huku wengine wanataka
kumrudisha Kifukwe, wengine mara Karigo au Falcon na kwamba inaonekana
uchaguzi huu utakuwa na msisimko wa aina yake,” alisema kiongozi mmoja
ambaye alijiuzulu katika uongozi uliopita.
Alisema kwa jinsi
mwelekeo wa wanachama unavyoonekana, endapo mmojawapo kati ya waliotajwa
akionesha nia ya kutaka kugombea hatakuwa na upinzani kwani inaonekana
wanakubalika.
Gazeti hili lilifika klabuni hapo na kushuhudia
kuwepo kwa vikundi vya wanachama wakiuzungumzia uchaguzi huo, huku
wakiyataja baadhi ya viongozi waliopita lakini hawakuwa tayari kueleza
zaidi mpaka Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, iliyo chini ya Jaji John
Mkwawa itakapotangaza rasmi.
|
Posted: 28 May 2012 11:53 PM PDT
Na Amina Athuman
MICHUANO
ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ngazi ya wilaya, Kanda ya Ilala
yalimalizika juzi kwa New Team FC kuifunga timu ya Sanry FC kwa mikwaju
ya penalti 6-5 katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo ambao ulivuta umati mkubwa wa mashabiki kutokana na timu
zote kuwa jirani, ulianza kwa kasi na ilibidi kipa wa New Team kufanya
kazi ya ziada dakika 20 za kwanza kwa kuokoa mabao matatu ya wazi kutoka
kwa washambuliaji wa Sanry FC, Twalib Mohammed na Hassan Kamoti.
Hata
hivyo baada ya mashambulizi hayo, Sanry FC walitulia na kuanza kupeleka
mashambulizi mfululizo langoni mwa wapinzani wao, lakini mabeki
walisimama vyema kuondoa hatari zilizoelekezwa kwao.
Kipindi cha
pili kilianza kwa timu zote kufanya mashambulizi kwa zamu lakini hadi
mwamuzi alipopuliza filimbi ya kumaliza mechi hiyo hakuna timu
iliyoliona lango la mwenzake.
Baada timu hizo kutoka suluhu
katika dakika 90 za kawaida, mwamuzi alilazimika kutumia sheria ya
kupigiana mikwaju ya penalti ili kupata mshindi ndipo New Team FC
ilibuika kidedea kwa mikwaju 6-5 dhidi ya wapinzani wao.
Mchezo
huo ulikuwa ni hitimisho la kuchangua wachezaji watakaoungana na timu ya
kombaini ya Mkoa wa Ilala kisoka, ambayo itaiwaikilisha kwenye fainali
za Copa Coca-Cola zitakaoanza Juni Mwaka huu.
Katika mchezo wa
kutafuta mshindi wa tatu, timu ya Aggrey FC iliifunga Young Stars FC
5-4, mchezo ambao pia uliamuriwa kwa mikwaju ya penati baada ya timu
zote kumaliza muda wa kawaida bila kufungana.
|
Posted: 28 May 2012 11:52 PM PDT
Na Yusuph Mussa, Korogwe
MBUNGE
wa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Tanga, Mary Chatanda ameiokoa timu ya
soka ya Korogwe United kuweza kushiriki mashindano ya Kanda, baada ya
kuwasaidia sh. milioni moja za kuwapiga jeki katika michuano hiyo.
Michuano hiyo itatoa timu zitakazopanda Daraja la Kwanza msimu ujao, ambapo timu hiyo imepangiwa kituo cha Musoma,Mara.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jana mjini hapa, Mkurugenzi wa Korogwe
United ambayo ndiyo mabingwa wa Mkoa wa Tanga, Filbert Mpezya alisema
mbunge huyo aliwaingizia fedha hizo kwenye akaunti yao, ambapo pia
zitawasaidia kukodisha basi dogo aina ya Coaster kwa ajili ya kwenda
Musoma kwenye mashindano hayo.
"Unajua mashindano haya ni gharama
hasa ukizingatia hayana udhamini, hivyo kwa kupata msaada wa sh.
milioni moja kutoka kwa Mama imetusadia sana sisi kuweza kufika kwenye
kituo cha mashindano na timu yetu inacheza mchezo wa kwanza leo na timu
ya Red Cross ya Dar es Salaam," alisema Mpezya.
Naye Chatanda
alisema ameamua kuisaidia timu hiyo, ili iweze kufanya vizuri kwenye
mashindano hayo hatimaye iungane na Coastal Union na Mgambo JKT kucheza
Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Nimewaingizia sh. milioni moja kama
ahadi yangu niliyoitoa kwenye sherehe zao za ubingwa wa mkoa, lakini pia
nitaendelea kuisaidia timu hii kama Mbunge na mkazi wa Korogwe kuona
inacheza Ligi
|
Posted: 28 May 2012 11:51 PM PDT
Na David John, Aliyekuwa Shinyanga
SERIKALI
imeshauriwa kuwasaidia waandishi wa habari ambao wanaripoti habari za
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na siyo kuwawekea vikwazo vya
kuwatisha pindi wanaporipoti habari hizo.
Mwito huo ulitolewa na
Mkurugenzi wa Shirika la Under The Same Sun Bw. Peter Ash mkoani
Shinyanga baada ya kutembelea Shule ya Msingi Buhangija ambayo imefanywa
kuwa moja ya kituo cha kulelea watoto wenye ulamavu wa ngozi.
Kituo hicho kilitengwa na Serikali baada ya kutokea mauaji ya albino miaka sita iliyopita.
Bw.
Ash alisema kuwa anatambua kuwa serikali itakuwa inajisikia vibaya hasa
kuendelea kuripotiwa kwa habari hizo kwa kutambua kuwa mauaji hayo
yametia doa utulivu na amani ya nchi katika nyanja za kitaifa na
kimataifa.
"Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikisomeka kuwa ni
miongoni mwa nchi ambayo imefanikiwa kulinda amani na utulivu wa nchi,
lakini baada ya kutokea mauaji hayo yamechafua uhalisia wa amani ya
nchi,"alisema Bw Ash.
Alisema ili serikali ionekane haiungi mkono
mauaji ya walemavu wa ngozi inatakiwa kuendelea kuunga mkono waandishi
wa habari kupinga mauaji hayo ili kulisafisha taifa liendelee kuonekana
kuwa ni kisiwa cha amani na upendo.
Mbali na rai hiyo Bw. Ash
alitumia fursa hiyo kutoa vifaa mbalimbali kwa watoto hao ikiwa pamoja
na miwani kwa ajili ya kujikinga na jua, kofia, madawa ya ngozi, losheni
za kujipaka kwa ajili ya kuzuia miozi ya jua.
|
Posted: 28 May 2012 11:50 PM PDT
Na Mwandishi Wetu, Lindi
MSHAURI
Mkuu wa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia, Danda
Juju ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho amesema ni
hatari wananchi kubadili mitazamo yao kisiasa kutokana na maisha magumu
yanayowakabili.
Alisema,
kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitaki kuondoka madarakani kwa hiari,
siku wananchi wakiamua kukiondoa madarakani machafuko yanaweza kutokea.
Hayo aliyasema jana Mjini Liwale Mkoa wa Lindi,alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
"Hiki
Chama Cha Mapinduzi kimechoka, nasema kimechoka kweli kweli na hakina
tena sifa za kutawala nchi hii ingawa viongozi wake hawataki kulikubali
hilo.
"Sisi hatutaki kufika huko, Tanzania ni nchi ya amani,
Tanzania ndiyo nchi inayoheshimika duniani kwa amani na utulivu, lakini
narudia tena, binadamu anapobadilika kwa sababu ya shida zinazomkabili
anakuwa mbaya zaidi kuliko hata mnyama," alisema Mjumbe huyo wa
Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi.
Wakati huo huo, alisema CCM ya
sasa siyo CCM ya kuwavutia watu kwa sababu chama hicho hakifuati misingi
ya utawala bora na kwamba ili kuondokana na kero zinazosababishwa na
utawala wa chama hicho wananchi hawana budi kukikataa kwa vitendo.
|
Posted: 28 May 2012 11:49 PM PDT
Na Daud Magesa, Mwanza
MABINGWA
wa zamani wa soka Tanzania Pamba ya Mwanza, imeondoka jijini hapa ikiwa
na matumaini makubwa ya kufuzu fainali za Kanda ili kucheza Ligi Daraja
la Kwanza.
Pamba ambao ni mabingwa wa soka Mkoa wa Mwanza,
iliondoka juzi kwa basi la kukodi ikiwa na kikosi cha wachezaji wake
wote chini ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ramadhan Muzzo na kuahidi
ushindi.
Wadau wa soka
jijini hapa ambao walifika kuwaaga wachezaji wa timu hiyo, makocha na
viongozi, walisema silaha pekee itakayowasaidia kufuzu katika michuano
hiyo ni nidhamu kwa kila mchezaji na kutimiza majukumu yao.
Wadau
hao waliwataka wachezaji wa timu hiyo iliyowahi kutikisa soka la
Tanzania katika miaka ya 1980 na mwishoni mwa 1990, kuwakilisha vyema
mkoa na kubwa ikiwa ni kupata nafasi ya juu ili kufuzu kucheza Ligi
Daraja la Kwanza.
Walisema wakishikamana na kufuata maelekezo ya makocha na wakizingatia nidhamu katika michuano hiyo ni wazi watafanya vizuri.
"Kikubwa
ni kuzingatia nidhamu, kuonesha mshikamano wenu kama timu uwanjani na
nje ya uwanja, kila mchezaji atimize wajibu wake pamoja na changamoto
mliyonayo ya ukata," alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Waandishi wa Habari
ya Kuhamasisha Pamba ishinde, Mashaka Baltazar
Naye Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora,
alisisitiza nidhamu kwa wachezaji hao akisema mkoa huo upo pamoja nao
kuhakikisha wanafanya vizuri.
Pamba iko katika Kituo cha Kigoma
pamoja na wenyeji JKT Kanembwa, Majimaji ya Tabora, Mwadui ya Shinyanga,
Mabingwa wa Mkoa wa Singida, CDA ya Dodoma na Bandari ya Kagera.
|
Posted: 28 May 2012 11:46 PM PDT
Na Elizabeth MayembaKAMPUNI
ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania imekabidhi vifaa vya michezo kwa
timu za vijana chini ya miaka 17 zitakazoshiriki mashindano ya Aitel
Rising Stars, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho katika mikoa
sita.Mikoa ambayo itashiriki michuano hiyo ni Lindi, Mbeya,
Arusha, Ilala, Temeke na Kinondoni, ambapo kwa upande wa Ilala mechi
zitakuwa zikichezwa Uwanja wa Airwing, Kinondoni Mwenge na Temeke mechi
zitachezwa Uwanja Twalipo.Akikabidhi
vifaa hivyo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) Sanifu Kondo, Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde,
alisema jumla ya timu 24 zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo.Alisema vifaa vilivyotolewa ni jezi na mipira na kila timu itapatiwa jezi mbili."Mwaka
huu tumeboresha zaidi michuano hii ikiwa ni pamoja na kushirikisha
timu za wasichana tofauti na hapo awali, ambapo kila mkoa utatoa timu ya
wanawake ambayo itakuwa kombaini."Mwaka huu mashindano
yatashirikisha mikoa sita kwa kuanzia ngazi ya mikoa kabla ya ile ya
taifa itakayoanza Juni na timu bingwa itashiriki mashindano ya siku nne
nchini Kenya yajulikanayo kama Inter Continental Tourmament
yatakayoshirikisha mataifa zaidi ya 16," alisema Jane.Alisema
mbali na timu hiyo pia watateua wachezaji sita bora ambao watashiriki
kliniki ya soka maarufu kama Coaching Stars itakayofanyika nchini Kenya
chini ya jopo la makocha kutoka Academy ya soka ya Manchester United ya
Uingereza.
|
No comments:
Post a Comment