HOSPITALI
ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imepokea msaada wa vifaa afya na tiba
vyenye thamani ya sh. milioni 200.5 kutoka Shirika lilisilokuwa la
kiserikali la Uboreshaji wa Maisha Vijijini la nchini Uingereza
(TRR).
Shirika
hilo lenye wanachama sita ambao ni raia wa nchi hiyo wakishirikiana na
Watanzania wazaliwa wa Wilaya ya Makete ambao wanaishi jijini Dare es
Salaam mara kwa mara wamekuwa wakifanya shughuli za maendeleo katika
wilaya hiyo.
Akikabidhi
misaada hiyo mwakilishi wa Wanamakete hao Bi. Sophia Ng'wango alisema,
misaada hiyo imetolewa kwa lengo la kusaidia sekta ya afya na kutatua
kero mbalimbali ambazo zinaikabili sekta hiyo.
Alisema, Shirika
la TRR lilianza shughuli za kuwasaidia watu wa Makete tangu mwaka 2006
ambapo lilitoa fedha ambazo zilisaidia watoto yatima katika Kituo cha
Bulongwa, ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari ya Mwakauta na
kununua vitabu katika shule ya Usililo na kwamba kila mwaka tangu mwaka
huo shirika limekuwa likitoa fedha kwa ajili ya kusaidia sekta
mbalimbali.
Bi. Ng'wango alisema, katika kipindi ambacho wameanza
mahusiano na wahisani hao tayari wananchi kadhaa wamenufaika na misaada
ambapo hadi sasa kuna maeneo mengi ambayo yamenufaika na msaada huo na
kwamba katika sekta za kifedha wametoa misaada ya fedha za kutunisha
mfuko katika Saccos ya Bulongwa na Juhudu Saccos.
Alisema, pia
Shirika la TRR linajihusisha na utatuzi wa kero ya huduma ya maji katika
maeneo mbalimbali na kwamba vijiji vya Iniho, Bulongwa na Unyangogo
Serikali ilipelekewa fedha na wananchi hao ili kupeleka huduma ya maji
katika maeneo hayo.
Ofisa Tawala wa wilaya hiyo Bw. Joseph Chota
aliwashukuru wahisani na kuomba kama kuna fursa nyingine ni vyema
waangalie uwezekano wa kusaidia serikali katika ujenzi wa nyumba za
watumishi pamoja na kujenga uzio wa hospitali kwani inapungukiwa na vitu
mbalimbali muhimu ikiwa ni pamoja na majokofu katika vyumba vya maiti.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bi. Imelda Ishuza alisema,
ushirikiano unaoonesha na wananchi hao ni mfano wa kuigwa na kwamba
serikali inapunguziwa mzigo wa majukumu na kwamba kama wananchi wengi
wangelikuwa na moyo wa kujitolea kama hao matatizo katika wilaya hiyo
hususan katika sekta mbalimbali yasingekuwepo.
Bi. Ishuza
aliwashukuru wahisani hao na kuongeza kuwa serikali inathamini na kujali
mchango wao na kwamba itasimamia kwa haki kuhakikisha kila
mkilichotolewa kinatumika katika malengo ambayo yalikusudiwa na si
vinginevyo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Bw. Atilio Ng'ondeya kwa niaba ya wananchi aliomba uongozi wa hospitali
hiyo kuhakikisha vifaa hivyo vinanufaisha wananchi wa eneo
lililokusudiwa na kwamba vitumike kwa matumizi sahihi sawa na malengo
yaliyokusudiwa.
ANCHOR
Wananchi kunufaika na mradi wa umeme
SHIRIKA
lisilokuwa la kiserikali la CEFA linalojihusisha na masuala ya kijamii
mkoani Njombe limezindua mradi wa kufua nishati ya umeme katika Kijiji
cha Ikondo ambao unatarajia kugharimu zaidi ya sh. bilioni 3.5.
Aidha,
shirika hilo linafadhiliwa na mashirika ya ulaya na kufanya kazi na
kampuni ya CEFA ya mjini Njombe, Kampuni ya Matembwe iliyopo Lupembe
wilayani humo.
Shirika hilo lilianzisha mradi wa ufuaji wa umeme
zaidi ya miaka 25 iliyopita na kusambaza katika vijiji vya Matembwe,
Barazani na Lupembe.
Akitambulisha mradi huo kwa viongozi wa
vijiji, kata, tarafa, wilaya na halmashauri katika ukumbi wa
halmashauri ya wilaya hiyo hivi karibuni Meneja Mradi wa shirika hilo
Bw. Giacono Spigarelli alisema, mradi wa Ikondo unatarajia kuzalisha
nishati ya umeme zaidi ya 'Kw. 240'
ambapo awali ulikuwa unazalisha 'Kw 80' huku matumizi yakiwa makubwa kulinganisha na kiwango kinachozalishwa.
Bw.
Spigarelli alisema, wananchi wanaohitaji huduma ya nishati hiyo ni
wengi, ambapo mradi uliopo ulianza mwaka 2006 na kwamba mradi
unaotambulishwa hivi sasa utanufaisha wananchi katika kata zaidi ya 10
ambapo wananchi wameshiriki kikamilifu katika kuandaa mpango wa
kukamilisha madi huo unaotarajia kukamilika miaka minne ijayo.
Kwa
upande wake Bw. Johannes Kamonga alisema, CEFA lilianza kushirikiana na
MVC baada ya kubaini kuwa wanaweza kuendesha miradi ya umeme kutokana
na wao kufanikisha kusimamia mradi wao wa umeme ambao ni wa muda mrefu,
na kwamba kazi ya usanifu na mitambo itasimamiwa na MVC.
Alisema,
Kampuni ya MVC imekuwa msitari wa mbele katika masuala ya nishati ya
umeme kwa kuwa pamoja na kujihusisha na mausuala ya uzalishaji
vifaranga, pia wana mradi wa umeme ambao unahudumia vijiji vya Tarafa ya
Kata ya Lupembe.
Bw. Kamonga alisisitiza madiwani na viongozi wa
vijiji kuhakikisha wanasimamia uandaaji wa miundombinu katika maeneo ya
mradi ili mafundi waweza kurahisisha ufikaji katika mradi.
Naye
Father Camirro Cariall alisema, kazi ya ubunifu w a miradi ya maendeleo
imekuwa ikifanywa na yeye na kwamba kila anachokiona chema machoni pake
ni chema kwa jamii, kwa ujumla kwani kazi ya 'umishionari' ni kuangalia
matatizo ya wananchi na kuyatatua.
Akizindua mradi huo Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Bw. Steven Mkalimoto aliwashukuru
wahisani na kuomba uharakishaji katika ujenzi wa mradi huo ili wananchi
waanze kunufaika na mradi huo.
Alisema, sasa ni jukumu la
viongozi kuhakikisha wanashirikiana na wahiisani hao ambao wanakuja
kuangaza maisha ya wananchi ambao kimsingi hawana msaada hususan katika
masuala ambayo ni nyeti na kuhakikisha nishati hiyo inafika katika,
maeneo ya kutolea huduma za afya.
Alisiitiza ushirikiano na
wahisani hao na kwamba, yapo amambo ambayo serikali inapaswa kushiriki
moja kwa moja katika mradi huo, lakini nguvu za wananchi zitaharakisha
kukamilika kwa mradi na kuleta tija.
Katika hafla hiyo fupi ya
utambulisho wa mradi, wadau mbalimbali waliudhuria ambapo Diwani wa Kata
ya Mtembwe Bw. Shaibu Masasi alisema, wananchi wameshiriki kikamilifu
katika masuala ya maandalizi na kwamba ushirikishwaji ni muhimu katika
mradi huo
No comments:
Post a Comment