Posted: 07 Jun 2012 01:35 AM PDT
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (kushoto) akishiriki kupima afya yake
wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 10 kuhusu njia bora ya maisha na
kujikinga na kukabiliana na magonjwa sugu yasiyoambukiza iliyoratibiwa
kwa pamoja na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) na Shirika la
Maendeleo la Ujerumani (GIZ)
|
Posted: 07 Jun 2012 12:29 AM PDT
Ndege mpya ya ATCL inayotumika sasa baada ya kutua uwanjani Dar es salaam hivi karibuni.
|
Posted: 07 Jun 2012 12:25 AM PDT
Rais
Jakaya Kikwete (katikati) akiwa na marais wastaafu, Benjamin Mkapa
(kushoto) na Ali Hassan Mwinyi wakati wa harambee ya kuchangia fedha za
mpango wa Mkapa Fellows unaoratibiwa na Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS
iliyofanyika Dar es Salaam juzi. (Picha na Ikulu)
|
Posted: 07 Jun 2012 12:17 AM PDT
Katibu
Msaidizi wa CCM Wilaya ya Temeka, Bi. Anastazia Mwonga (kulia),
akimkabidhi Bw. Yahaya Ndomondo, fomu za kugombea nafasi ya Katibu wa
Siasa na Uenezi wa Wilaya ya Temeke, Dar es salaam juzi, kwa ajili ya
uchaguzi mkuu wa chama hicho. (Na Mpigapicha Wetu)
|
Posted: 07 Jun 2012 12:15 AM PDT
WALIMU
wa Shule za Sekondari wilayani Kahama mkoani Shinyanga ,wameanzisha
kampeni ya kupiga vita tatizo la mimba kwa wanafunzi mashuleni. Mpango
huo ambao wanauitwa 'Rosebug' kwa maana 'ua waridi changa lazima
litunzwe na kulindwa', lengo lake ni kuwaokoa watoto na tatizo la kupata
ujauzito wakiwa shuleni. Kampeni
hiyo ilizinduliwa juzi katika Sekondari ya Nyihogo mjini Kahama na
kuzihusisha shule 15 za Tarafa ya Kahama Mjini, ambapo kulitolewa elimu
ya kuwataka watoto kuachana na vitendo vya zinaa vinavyosababisha mimba
shuleni. Tunaunga mkono mpango huo kwani tunatambua athari za
mimba mashuleni. Ujauzito kwa wanafunzi kwa kiasi kikubwa unaathiri
mipango ya wazazi wanafunzi kwa ujumla, ndiyo maana Serikali imekuwa
mstari wa mbele kupambana na mafataki. Tatizo hilo limekuwa likisababisha kila mwaka maelfu ya wanafunzi wa kike kuacha masomo kutokana na kupata ujauzito. Tatizo
hilo si tu linawasikitisha wazazi waliotumia fedha zao nyingi
kuwasomesha watoto wao, bali pia wanakuwa wameongezewa mzigo wa malezi
ya mtoto. Hali hii huwakatisha tamaa wazazi na ndio sababu baadhi yao wanahofu kuwaendeleza watoto wao wa kike kielimu. Zipo
sababu nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanya mabinti wengi wajikute
wakipata ujauzito na miongoni mwake ni kutokana na kutojua njia dhabiti
za kujikinga na ujauzito na baadhi ya wazazi wanakaa mbali na watoto
wao, hivyo kutopata fursa ya kuwapa elimu ya kujikinga na mimba za
utotoni. Wengine wanadhani jukumu hilo ni la walimu. Hali hiyo
ndiyo inachangia kuongezeka kwa mimba kwa wanafunzi kutokana na watoto
wetu kukosa malezi ya pamoja. Tunatambua kuwa zipo njia za kila aina
ambazo zinaweza kumaliza tatizo hili iwapo kila mmoja ataelewa kuwa
tatizo hilo ni kubwa. Kinachotakiwa ni wazazi na walezi kwa
pamoja ndani ya jamii ni kuzungumza kauli ya kutokomeza ujauzito kwa
wanafunzi wa kike. Hii inawezekana iwapo kila mmoja wetu anatahakikisha
mtoto wa jirani yake analindwa. Hata hivyo tuna imani kama
jitihada za pamoja zitaunganishwa kufanya kampeni kama hiyo, tatizo
hili litaweza kupungua kwa kiasi kikubwa kama siyo kutokomezwa kabisa. Tunachukua
fursa kuwaomba walimu na wazazi katika wilaya nyingine nchini nao
kupanga mkakati kama huo ili kukabiliana na janga hilo.
|
Posted: 07 Jun 2012 12:14 AM PDT
Meneja
Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Simgas Tanzania Ltd, Bw. Tayeb
Noorbhai (kulia) akizungumza na baadhi ya wateja jinsi ya kutumia
gesi550 itokanayo na mabaki ya vyakula na takataka waliotembelea banda
la kampuni hiyo Dar es Salaam jana, inayotumika kwa matumizi ya nyumbani
ambayo pia huzarisha mbolea, wakati wa Maonesho ya Nishati Jadilifu.
(Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 07 Jun 2012 12:12 AM PDT
Na Zahoro Mlanzi KLABU
ya Simba, imepanga kufanya ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanzia
Juni 16 na 17 mwaka huu yenye lengo la kusherehekea kutwaa ubingwa wa
Ligi Kuu Bara. Mbali na hilo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia bia ya Kilimanjaro Lager, imepanga kuikabidhi timu hiyo basi
jipya la kisasa siku ya Simba Day, ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 8. Akizungumza
Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza rasmi ziara hiyo, Mwenyekiti wa
klabu hiyo, Ismail Rage alisema ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya
kupeleka kombe walilotwaa kwa mashabiki wao wa Kanda ya Ziwa. "Tutaanzia
Shinyanga Juni 16 ambapo tutacheza na Toto African na kisha kwenda
Mwanza nako tutacheza na timu moja kutoka Uganda, ambapo mazungumzo
yanaendelea na ikiwa tayari tutaitangaza," alisema Rage. Alisema
mashabiki wa mikoa hiyo watapata fursa ya kufurahia mafanikio ya timu
yao kwa msimu uliopita na watashuhudia ushirikiano uliopo kati yao na
TBL. Naye Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema
wanaishukuru timu hiyo kwa kuendelea kuwaunganisha pamoja Watanzania kwa
mafanikio wanayoyapata na pia kutekeleza yanayopaswa kufanywa katika
mkataba wao.
|
Posted: 07 Jun 2012 12:11 AM PDT
Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma
Pinto (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana
(hawapo pichani), kuhusu tuzo za Mwanamichezo Bora wa mwaka
zitakazotolewa Juni 14 mwaka huu. Katikati ni Meneja Mawasiliano wa SBL,
Imani Lwinga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Maulid Kitenge.
(Picha na Victor Mkumbo)
|
Posted: 06 Jun 2012 11:53 PM PDT
Na Goodluck Hongo, Lindi CHAMA
cha Wananchi (CUF), kimepata pigo baada ya Bw. Mohamed Madebe aliyekuwa
meneja kampeni wa Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini, Bw. Salum Barwany,
kukihama chama hicho na kukimbilia CHADEMA. Uamuzi huo aliutangaza jana katika mkutano wa hadhara maarufu kwa jina la Okoa Mikoa ya Kusini uliofanyika Lindi Mjini. Bw. Madebe alisema ameamua kukihama cha hicho kutokana na chama cha CUF kupoteza mwelekeo na kuyumbayumba. "Nimeamua
kukihama CUF kwa utashi wangu wenyewe bila ya kushurutishwa na mtu
kwani hivi sasa chama hiki kimekuwa kikipoteza mwelekeo na kutokuwa na
sifa kama awali, " alisema. Aliwaomba wananchi wengine kumfuata,
kwani CHADEMA inaoneka kuwa ni chama ambacho kimeonesha nia ya
kubadilisha maisha ya umaskini kwa wananchi. Katika mkutano huo,
Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, alisema chama hicho
kitaendelea na operesheni yake katika maeneo mbalimbali ili kuwaamsha
wananchi waliolala na kunyanyukia CHADEMA.
|
Posted: 06 Jun 2012 11:51 PM PDT
|
Posted: 06 Jun 2012 11:50 PM PDT
Na Mwandishi Wetu TIMU
ya Taifa (Kilimanjaro Taifa Stars), imepanda katika viwango
vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA), kutoka nafasi ya 145 mpaka 139. Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Boniface Wambura ilieleza kwamba Tanzania imepanda kwa nafasi
sita kwenye orodha hiyo inayoongozwa na Hispania. Alisema
timu hiyo ambayo kwa sasa inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager,
ilikuwa namba 145 hivi sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214. "Mei
26, mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi na
kutoka suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano
kutoka ya 102 hadi 107," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Alisema
Ivory Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2, mwaka huu
iliifunga Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15
hadi 16 ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande wa
nchi za Afrika katika viwango hivyo. Wakati huohuo, timu ya
Taifa ya Hispania imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Uruguay, Ujerumani,
Uholanzi, Brazil, England, Argentina, Croatia, Denmark na Ureno. Zingine
ni Chile ambayo ipo nafasi ya 11 ikifuatiwa na Italia, Urusi, Ufaransa,
Ugiriki, Ivory Coast, Sweden, Jamhuri ya Ireland, Mexico na Colombia.
|
Posted: 06 Jun 2012 11:48 PM PDT
Mwendesha
Pikipiki ya abiria 'Bodaboda', (aliyesimama kushoto), akiwa ameshika
nyonga, haamini kilichotokea, huku akimwangalia Polisi wa Kikosi cha
Usalama Barabarani, aliyekuwa akimwandikia faini, baada ya kukutwa na
makosa ya usalama barabarani eneo la Karume, Manispaa ya Ilala Dar es
Salaam juzi. (Picha na Heri Shaaban)
|
Posted: 06 Jun 2012 11:44 PM PDT
Na Zahoro Mlanzi NI
zali limedondoka, ndivyo utakavyothubutu kusema baada ya Mawakala
watatu kutoka nchi mbalimbali kumuhitaji mshambuliaji wa timu ya Taifa
ya Uganda 'The Cranes' na Simba, Emmanuel Okwi akacheze soka la kulipwa
Ulaya. Lakini klabu ya Simba, imeweka wazi kwamba ipo tayari
kumwachia nyota huyo kama wakiwa wameweka kitita cha euro 500,000 na si
vinginevyo. Akizungumza Dar
es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage alisema
wamepokea ofa kutoka kwa mawakala watatu ambao wanafanya kazi na wakala
Ali Selehe wa Zanzibar kwamba wanamuhitaji mshambuliaji huyo. "Mawakala
hao wanataka Okwi akacheze soka la kulipwa katika nchi za Seribia,
England au Australia lakini kati ya hao wakala anayetaka Okwi akacheze
Australia ndiye ambaye tunaendelea kufanya naye mazungumzo. "Tayari
ameshatuma maelezo ya awali ambayo yanapitiwa na mwanasheria wake na
wanamuhitaji kipindi hiki, lakini hao wengine bado hawajaweka wazi ni
lini wanamuhitaji," alisema. Alisema watakuwa tayari kumruhusu
Okwi kwenda popote kwa zaidi ya euro 500,000 kwani wachezaji wao kwa
sasa wapo juu kiuchezaji, hivyo dau hilo ni kwa Okwi na ikitokea kwa
mwingine watazungumza nao. Aliongeza kuwa ukiachana na Okwi, pia
kuna wachezaji wengine watatu wa timu yake ya vijana (U-20), wakati
wowote wanakwenda nchini Ujerumani kufanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa. Mbali na hilo, pia alijibu maswali kuhusu usajili
hususani wa mchezaji Kelvin Yondani ambaye inadaiwa amesaini na Yanga
pia, ambapo alisema: "Yondani ni mali yetu na ameshasaini mkataba
mwingine, hivyo wanaosema kasaini sehemu nyingine hilo ni la kwao." Alisema
si hilo tu, wanajua vitu vingi vinazungumzwa kuhusu kocha wao, Milovan
Cirkovic lakini alithibitisha kwamba wameshamalizana naye na kwamba muda
si mrefu atarejea nchini kuendelea kuinoa timu hiyo katika mashindano
ya Kombe la Kagame.
|
Posted: 06 Jun 2012 11:43 PM PDT
Wachezaji
wa timu ya Taifa (Taifa Stars), wakiomba dua mara baada ya kumaliza
mazoezi yao ya kujiandaa na mechi dhidi ya Gambia itakayofanyika
Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mazoezi hayo yalifanyika
jana kwenye Uwanja wa Karume. (Picha na Rajabu Mhamila)
|
Posted: 06 Jun 2012 11:41 PM PDT
Na Elizabeth Mayemba JUMLA
ya wagombea 28 wa Klabu ya Yanga wamejitokeza kuwania nafasi za uongozi
katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mdogo uliopangwa kufanyika Julai 15,
mwaka mhuu. Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo Francis Kaswahili, alisema awali walijitokeza wagombea 33 lakini wanne hawakurudisa fomu. Aliwataja
wagombea wanaowania nafasi ya Uenyekiti kuwa ni Yusuf Manji, John
Jambele, Edgar Jambele na Sarah Ramadhan, nafasi ya Umakamu ni Ayoub
Nyenzi, Ally Mayai, Yono Kevela na Clement Sanga. Kaswahili
aliwataja wanaowania ujumbe kuwa ni Abdallah Binkleb, Mussa Katabalo,
Ramadhan Kampira, Lameck Nyambaya, Mohammed Mbaraka, Ramadhan Said,
Edgar Fongo, Beda Tindwa na Ahmed Gao. Wengine ni George Manyama,
Aaron Nyanda, Omary Ndula, Shaaban Katwila, Jumanne Mwamenya, Peter
Haule, Justine Baruti, Abdallah Mbaraka, Jamal Kisongo, Gaudisius
Ishengoma na Yono Kevela. Alisema ambao hawakurudisha fomu ni
Muhingo Rweyemamu, Mzamiru Katunzi, Eliakim Mmaswi waliokuwa wanawania
ujumbe na Isaack Chanja Makamu Mwenyekiti. Kaswahili alisema
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na ile ya TFF, kesho watapitia majina ya
wagombea wote na yale yaliyokidhi vigezo yatatangazwa tena.
|
No comments:
Post a Comment