Posted: 12 Jun 2012 11:48 PM PDT
Na Faida Muyomba, Geita MKAZI
wa Kijiji cha Mwagimagi, Wilaya ya Geita, mkoani Geita, Bi. Dome Shaban
(35), ameuawa kwa kupigwa na mumewe baada ya kumfumania akifanya
mapenzi na mwanaume mwingine.Akizungumza na waandishi wa habati,
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paulo, alisema tukio hilo
lilitokea Juni 11 mwaka huu, saa nane usiku na kumtaja mtuhumiwa wa
mauaji hayo kuwa ni Bw. Faida Anthony (45), ambaye ni mume wa mwanamke
huyo.Alisema mwanamke huyo
alifumaniwa akiwa na mwanaume mwingine ambaye jina lake halikufahamika
wakifanya mapenzi chumbani wakati mumewe hayupo.“Mtuhumiwa
aliporudi nyumbani aligonga mlango na kukuta mkewe akifanya mapenzi na
mwanaume mwingine ambaye alifanikiwa kukimbia na hadi sasa hajulikani
jina lake na mahali anapoishi,” alisema Kamanda Paulo.Aliongeza
kuwa, mtuhumiwa alichukua kitu chenye ncha kali na kumchoma sehemu ya
jicho la kulia la kushoto kabla ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili
hadi kusababisha kifo chake.Alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya mauaji hayo ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:47 PM PDT
Na Salim Nyomolelo
SERIKALI
imeanza kuchukulia hatua kwa taasisi, mashirika na watu mbalimbali
wanaotumikisha watoto walio chini ya miaka 18 na kuwakosesha haki zao za
msingi ikiwemo ya kupata elimu.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,
Dkt. Makongoro Mahanga, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika kilele
cha Siku ya Kimataifa ya kupiga vita utumikishwaji watoto iliyoandaliwa
na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Alisema
tayari hatua za kisheria zimechukuliwa kwa watu wanaotumikisha watoto
walio chini ya miaka 18, ambao walichukuliwa na kupewa haki zao za
msingi ikiwamo elimu.
Aliongeza kuwa, suala la malezi, matunzo na
kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vinavyolenga kuhujumu haki zao
ni jukumu la wadau wote kutokomeza vitendo hivyo.
“Utumikishwaji
watoto katika kazi hatarishi ni hujuma kwa haki za mtoto kuishi, kukosa
muda wa kupumzika, malezi bora, kucheza na kupata elimu,” alisema Bw.
Mahanga
Alisema utumikishwaji watoto ni tatizo la kitaifa na
kimataifa, ambapo kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ILO mwaka 2010,
zinaonesha watoto milioni 215 wanatumikishwa katika sekta mbalimbali
duniani kote.
“Katika Afrika nchi zilizo katika Jangwa la Sahara,
zinakadiriwa kuwa na watoto milioni 65 wanaotumikishwa katika kazi za
hatari, upande wa Tanzania kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa mwaka
2005/2006, asilimia 18.7 ya watoto wenye umri kati ya miaka mitano hadi
17, wanatumikishwa katika shughuli mbalimbali,” alisema Dkt. Mahanga.
Aliongeza
kuwa, Serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa na imeanza kutekeleza
mpango kazi wa kitaifa wenye lengo la kutokomeza utumikishwaji watoto.
Mpango
huo umelenga kutimiza malengo ya milenia ifikapo mwaka 2015 ambapo
Serikali imefanikiwa kuandaa orodha ya kazi hatarishi ambazo hazipaswi
kufanywa na watoto chini ya umri wa miaka 18.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:52 PM PDT
Mtoto
ambaye jina lake halikupatikana akiangua kilio baada ya karanga na
mayai aliyokuwa akiuza kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Kawe
kumwagika kutokana na upepo makali kama alivypnaswa na kamera yetu.Tukio
hilo lilitokea jana ikiwa ni Siku ya Kupinga Utumikishwaji kwa Watoto
Duniani yenye kauli mbiu "Haki za binadamu na usawa katika jamii
tokomeza utumikishwaji wa watoto". (Picha na Blog ya Immatukio).
|
Posted: 12 Jun 2012 11:37 PM PDT
Na Godwin Msalichuma, Mtwara
WATUMISHI
wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, wamefikishwa mbele ya Hakimu
Mkazi, Bi. Agnes Futakamba, wa Mahakama ya Wilaya hiyo wakituhumiwa kwa
kosa la ubadhilifu wa sh. milioni 12.32 zilizotolewa kwa ajili ya
kuendesha mafunzo ya makuzi na malezi ya mtoto. Washtakiwa
hao ni Bw. Hassan Mwakipa ambaye ni Ofisa Tabibu Msaidizi na Mhasibu
Bw. Absolum Ntakandi ambaye hakuwepo mahakamani ambao wankabiliwa na
mashtaka 15.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU), Bw. Sospeter Tyeah, alisema washtakiwa wote
wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Juni 11-16, 2009. Alisema
makosa hayo yamegawanyika katika maeneo matatu, ambayo ni kula njama za
kumdanganya mwajiri wao na kubadilisha matumizi ya fedha kwa manufaa yao
binafsi, kugushi nyaraka na kuhujumu uchumi. Bw. Tyeah alisema katika kosa la kwanza, washtakiwa wanadaiwa kutengeneza
nyaraka za malipo ya washiriki 25 wa mafunzo ya makuzi na malezi ya
mtoto Juni 11, 2009 na kila mmoja kulipwa sh. 320,000. Kosa la
pili, katika kipindi hicho washtakiwa wanadaiwa kutumia karatasi zisizo
na tarehe kuwalipa washiriki saba sh. 450,000 kila mmoja maelezo ambayo
ni ya uongo. Mashtaka mengine ni kumlipa Bi. Elizabeth Macha, sh.
560,000 kwa madai ya kuhudhuria mafunzo hayo kama mwezeshaji na kuandaa
stakabadhi namba R07584 ya Januari, 4, 2010. Stakabadhi hiyo
ilieleza kuwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo alimlipa
Mkurugenzi wa Chuo cha Ushirika, tawi la Mtwara, sh. 129,000 kama
gharama za ukumbi. Bw. Tyeah ambaye alitumia zaidi ya dakika 20
kusoma tuhuma hizo, alidai washtakiwa walitumia tiketi ya ndege PW/MQQB7
ya Juni 9, 2009 wakidai ilitumiwa na Bi. Elizaberth Macha kwa ajili ya
safari ambayo gharama yake ni sh. 368,000. Stakabadhi nyingine
haikuwa na tarehe ikionesha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo alimlipa sh.
750,000, Mkuu wa Chuo cha Ushirika kwa ajili ya ukumbi.
Shtaka lingine ni kuwepo risiti inayoonesha Juni, 12, 2009, Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri hiyo amemlipa mtu ambaye hakutajwa jina sh.
320,000 ili kununua karatasi kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo.
Bw.
Tyeah aliieleza mahakama kuwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya
kugushi nyaraka, kubadilisha matumizi ya fedha na kuisababishia
halmashauri hasara ya sh. milioni 12.32.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:35 PM PDT
Rais
waZanzibar na Mwenyekiti wa Balaza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein,
alipokua akizungumza na wahariri na wahandishi wa habari wa vyombo vya
habari mbalimbali vya Bara naVisiwani, kuhusu vurugu za kundi la uhamsho
zilizotokea visiwani humo kwa siku tatu mfululizo (Juni 26,27 na 28
mwaka huu).Mazungumzo hayo yalifanyika mjini Zanzibar katika ukumbi wa
Ikulu hivi karibuni ambapo Serikari ilisisitiza vurugu hizo kusitishwa
mara moja.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:26 PM PDT
Na Zahoro Mlanzi KATIKA
kile kinachoonekana kuguswa na sakata la usajili la beki wa timu ya
Taifa (Taifa Stars) na Simba, Kelvin Yondani, Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, amesema suala hilo lina
mwisho wake kwani chombo husika kitalifanyia kazi pale muda utakapofika.
Beki huyo hivi sasa amekuwa
gumza si katika vyombo vya habari hata katika baadhi ya mitaa nchini
kutokana na namna ambavyo inadaiwa kusajiliwa na Yanga akitoroshwa
kambini usiku. Kutokana na tukio hilo, uongozi wa Klabu ya Simba,
ilitishia kuishtaki Yanga kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) kutokana na kushindwa kufuata taratibu husika. Akijibu
swali kuhusu sakata hilo Dar es Salaam jana, Tenga alisema Yondani
hajatoroshwa kama inavyodaiwa ila anachofahamu ni kwamba beki huyo ni
mtu mkubwa ambaye anaweza kuamua lolote, hivyo hakutoroka ila aliondoka
kambini. "Mimi ninadhani tuna mambo mengi ya kufanya kuliko
kuanza kuzungumzia hili la Yondani, hiki ni kipindi cha usajili la
lolote linaweza kuzungumzwa, si kitu cha ajabu mchezaji kutoka timu moja
kwenda nyingine," alisema Tenga na kuongeza; "Ila hapa tatizo ni
kwamba ametokaje kambini, je alipewa ruhusa na viongozi wake au
alijiondokea tu na hilo tumewaachia viongozi wake walishughulikie na
litakapokamilika watatupa majibu ya hatua gani wamechukua." Alisema
usajili una taratibu zake na muda wake hivyo kama mchezaji akiwa na
mkataba atacheza lakini asipokuwa nao hawezi kucheza na kwamba ndio
maana suala hilo la usajili lipo mikononi mwa klabu zenyewe. Alisema
ana imani muda ukifika hakuna shaka chombo kinachohusika kitalifanyia
kazi na mwisho wa siku itajulikana atachezea klabu ipi lakini
yanayoendelea hivi sasa ni 'unazi' wa mashabiki wa klabu hizo. Aliongeza
kutokana na tukio hilo, hivi sasa wameingia mikataba maalum na
wachezaji wao ambao utakuwa ukiwaelekeza taratibu za kambi, hivyo
mchezaji akienda kinyume na taratibu hizo hatua za kuchukuliwa zitakuwa
wazi. Mbali na hilo, Tenga aliipongeza timu ya Taifa (Taifa
Stars) kwa ushindi walioupata wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia na kwamba
ameomba kikosi hicho kilicho na vijana wengi kilelewe ili baadaye ilete
matunda kwa taifa. Alisema amekoshwa na kiwango kilichooneshwa
kwani hakuaimini kama wangeshinda katika mchezo huo lakini kutokana na
kujituma katika dakika zote 90 ndivyo zilizosababisha kupata matokeo
mazuri.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:25 PM PDT
Na Victor Mkumbo ALIYEKUWA
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Marcio Maximo, ameshindwa
kuja nchini kama ilivyopangwa kutokana na kumalizia majukumu yake ya
kuifundisha Democrata F.C ya Mjini Rio de Jeneiro, Brazil. Kocha huyo alitarajiwa kutua nchini jana mchana kwa ajili ya kuja kusaini mkataba na mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga. Akizungumza
Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa timu ya Yanga, Luois Sendeu alisema
kocha huyo ameshindwa kuja kama walivyopanga baada ya kutokea dharula
na sasa atatua nchini mwishoni mwa wiki hii. Alisema sababu kubwa
iliyomfanya kocha huyo kushindwa kuwasili jana, ni kutokana na timu
anayoifundisha kwa sasa ya Democrata F.C kukabiliwa na mchezo mgumu
Jumamosi. "Maximo tayari amekwishatumiwa tiketi ya safari ya kuja
hapa nchini, ameshindwa kuwasili leo (jana) kutokana na Klabu yake
anayofundisha kukabiliwa na mchezo mgumu," Sendeu alisema kuwa
Marcio mara baada ya kuwasili nchini atafanya mazungumzo na Uongozi wa
Klabu ya Yanga ikiwemo kusaini Mkataba na Klabu ya Yanga kabla ya kuanza
kazi ya kukinoa kikosi hicho. Wakati gazeti hili, likienda
mitamboni lilipata taarifa kwamba timu hiyo haipo tayari kumuacha
kirahisi kocha huyo, hivyo hawezi kuja nchini mpaka baadhi ya vitu
waviweke sawa.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:52 PM PDT
|
Posted: 12 Jun 2012 11:23 PM PDT
TATIZO la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini, linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu. Takwimu
za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinathibitisha kuwa tatizo hili
limekuwa likiongezeka siku hadi siku hasa baada ya kuanzishwa shule za
kata. Pamoja na shule hizo kupunguza tatizo la wanafunzi kukosa nafasi za masomo, bado zinakabiliwa na changamoto nyingi. Miongoni
mwa changamoto hiyo ni tatizo la mimba kwa wanafunzi ambao wengi wao
hulazimika kukatisha masomo, uhaba wa vifaa, vyumba vya madarasa, walimu
na madawati. Tafiti mbalimbali zimebaini kuwa, tatizo la mimba
kwa wanafunzi hasa wa sekondari ni kubwa na linagusa hisia za kila
mpenda maendeleo lakini jamii kubwa bado haijahamasika kutoa
ushirikiano wa karibu kwa vyombo vya dola ili kuwafichua wahusika wa
vitendo hivyo. Baadhi ya wazazi hupokea rushwa kutoka kwa
watuhumiwa ili wasifikishwe katika vyombo vya sheria na kuchukuliwa
hatua stahiki ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za aina hiyo. Sisi
tunasema dhamira yetu ni kuona wazazi wanashirikiana na vyombo hivyo
kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa ili sheria iweze kuchukua mkondo
wake. Kama jamii itaona umuhimu huu, Tanzania yenye wasomi
wazuri waliobobea katika fani mbalimbali itawezekana na maendeleo
yatakuwa kwa haraka. Kitendo cha jamii kuendelea kuwaficha
wahusika wa vitendo hivi, kinarudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau
wa elimu kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora. Imani yetu
ni kwamba, uwajibikaji wa viongozi wa vyama na Serikali unahitajika kwa
kuhamasisha jamii iboreshe maendeleo ya elimu hasa kwa mtoto wa kike na
kukomesha tatizo la mimba. Umefika wakati wa wanafunzi wetu,
kupewa elimu ya kujitambua na kufahamu wajibu walionao kwa jamii na
Taifa ili waweze kujithamini na kuepuka vishawishi vinavyoweza
kusababisha wapate mimba au kuacha shule. Elimu ni nyenzo muhimu
kwa maendelo ya Taifa lolote Duniani kwani mapinduzi mengi ya maendeleo,
hutegemea kiwango cha elimu kwa jamii husika.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:13 PM PDT
Na Sophia Fundi, Ngorongoro
MAMLAKA
ya Hifadhi ya Ngorongoro, mkoani Arusha, imewakamata watu wanne
wanaodhaniwa kuwa majangili ambao huwinda wanyama kwa kuwapa sumu katika
msitu wa mamalaka hiyo ulioko eneo la Kambi ya Simba, wilayani Karatu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Meneja Huduma za Uhifadhi wa mamlaka hiyo,
Bw. Amiyo Amiyo, alisema watu hao walikamatwa juzi, saa ya nne asubuhi
katika Msitu wa Sahata.
Alisema watu hao walikuwa na maboga 10 ambayo ndani yake waliyaweka sumu ya kuulia wanyama mbalimbali hasa tembo.
Aliongeza
kuwa, hivi sasa majangili wamebadili mbinu ya kuwinda wanyama wakitumia
sumu aina ya “aldicarb” ambayo kwa jina jingine hujulikana kama “temk”,
kwa mujibu wa uchunguzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Bw. Amiyo
alisema sumu hiyo ipo kwenye kundi la “Carbametes”, ambayo huathiri
mfumo wa ufahamu wa mnyama kama wataila hivyo kusababisha kifo chake.
Katika
tukio hilo, majangili hao walikutwa wakilinda maboga waliyotega msituni
ili yasiliwe na wanyama wengine zaidi ya tembo ambapo kutokana na hali
hiyo, mamlaka imelazimika kuimarisha ulinzi katika misitu.
“Kutokana
na doria tunayoifanya kila siku, tumefanikiwa kukamata majangili hawa
na kukuta mizoga ya tembo wawili ambao tayari walikuwa wametolewa meno,”
alisema.
Alisema majangili hao wanafahamika kwa majina ya Bw.
John Lohay (62), Bw. John Amisi (27), Bw. Isaya Arusha (36), Bw. Roman
Amsi (23) wote wakazi wa Kambiya Samba, wilayani Karatu na wamekabidhiwa
kwa Jeshi la Polisi.
Aliongeza kuwa, Februali mwaka huu mamlaka
hiyo ilifanikiwa kukamata watu wawili katika Msitu wa Mangola Juu
wilayani Karatu wakiwa na matikiti maji 60 ndani ya msitu huo.
Alisema matikiti hayo yalikuwa na sumu ya iina hiyo na tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya mjini Karatu.
“Kimsingi
majangili wamebuni mbinu mpya ya kuwatega wanyama na kuwaua kwa kutumia
sumu, tutahakikisha ulinzi unaimarishwa dani ya misitu yetu ili
kupambana na hawa magangili,” alisema.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:12 PM PDT
Na Anneth Kagenda
MAMLAKA
ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) inashikilia daladala
zaidi ya 126 kwa kukutwa na makosa mbalimbali, yakiwemo ya kutoa lugha
ya matusi, kupandisha nauli holela na mengine kutokuwa na leseni. Taarifa
iliyotolewa kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam jana na kusainiwa na
Ofisa Uhusiano wa SUMATRA Bw. David Mziray, ilieleza kuwa katika
kipindi cha Mei na Juni, 2012 mamlaka ilikamata ya daladala zenye
makosa mbalimbali, huku wamiliki wa mabasi hayo wakitozwa faini kati ya
sh 100,000 na sh 250,000.
Alisema daladala nyingi zilikamatwa
kwenye mkosa ya kutokuwa na leseni, kughushi nyaraka za Serikali, kuiba
njia, kutokuwa na tiketi kutovaa sale, kupakia eneo ambalo si la kitu na
mengine.
Bw. Mziray alisema kutokana na hali hiyo mmiliki ambaye basi lake litabainika na makosa hayo atachukuliwa hatua za kisheria.
"Pamoja
na kulipa faini hiyo mmiliki atatakiwa kusitisha mkataba na
kumbadilisha dereva wa basi husika ndipo aruhusiwe kuendelea na utoaji
huduma ya usafiri," alisema.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:11 PM PDT
|
Posted: 12 Jun 2012 11:09 PM PDT
Na Victor Mkumbo
MNYANGE atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia mwaka huu anatarajiwa kupatikana Jumamosi.
Mwakilishi
huyo atapatikana katika mashindano yaliyopewa jina la Redd's Miss World
Tanzania yatakayofanyika katika Ukumbi wa 327 Club jijini.
Akizungumza
na Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ndio waandaaji
wa mashindano ya urembo nchini, Hashim Lundenga alisema mashindano hayo
yanatarajia kushirikisha jumla ya warembo 10.
Alisema warembo 10
ndio waliothibitisha kushiriki katika mashindano hayo ambaye mmoja wao
ndio ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World
yatakayofanyika Agosti, mwaka huu nchini China.
Lundenga alisema
kuwa wameamua kuchukua warembo waliowahi kushiriki katika mashindano ya
Miss Tanzania katika miaka iliyopita, kutokana na mabadiliko ya ratiba
ya mashindano kwani awali yalikuwa yanafanyika Desemba.
"Tumeamua
kuchukua warembo ambao walishawahi kushiriki katika mashindano ya Miss
Tanzania miaka iliyopita kwa kuwa mashindano yetu huwa yanaanza Mei na
kumalizika Septemba," alisema.
Lundenga alisema mshindi katika
mashindano hayo anatarajiwa kuzawadiwa sh. milioni 10 pamoja na
kufanyiwa maandalizi yote ya kwa ajili ya matayarisho ya safari.
Naye
Meneja wa kinywaji cha Redd's, Victoria Kimaro, alisema wamejiandaa
vizuri na mashindano hayo ambapo wanatarajia kuwa watapata mwakilishi
mzuri.
Alisema kuwa shindano hilo litakuwa kwa ajili ya watu maalum ambao wataalikwa na kutakuwa na burudani ya aina yake.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:08 PM PDT
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga (kushoto), akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana kuhusu shindano
la Redd's Miss World Tanzania litakalofanyika Jumamosi. Kulia ni Meneja
wa kinywaji cha Redd's, Victoria Kimaro (Picha na Victor Mkumbo)
|
Posted: 12 Jun 2012 11:04 PM PDT
Na Daud Magesa, MWANZA BENDI
mbili kongwe za Muziki wa Dansi zenye upinzani wa jadi, DDC Mlimani
Park (Sikinde) na Msondo Ngoma, zinatarajia kutoa burudani katika
maadhimisho ya sherehe za miaka mitano tangu kuanzishwa kwa klabu ya
starehe ya Villa Park Resort. Sherehe
hizo zitahusisha michezo ya soka, muziki wadansi, taarabu na disco
zitafanyika kuanzia Juni 14 hadi 16, mwaka huu jijni. Akizungumza
na gazeti hili jana kuhusu sherehe hizo, Meneja wa hoteli ya Villa Park
Resort, Shijani Mtunga, alisema sherehe hizo zimelenga kuwakumbuka
wadau wanaofanya nao biashara na kujumuika nao ili kurudisha fadhila
kwao. Alisema kutokana na wadau hao kuwaunga mkono, ili
kusherehekea vizuri wamewaandalia burudani mbalimbali za soka, muziki wa
dansi, taarabu na disco kwa kila mtu. Alisema wapenzi wa muziki
wa dansi, watapata burudani ya muziki huo kutoka kwa Msondo Ngoma na
Sikinde, zitakapopambana Ijumaa, zikisindikizwa na bendi mwenyeji ya
Super Kamanyola, ambapo Jumamosi itakuwa ni mapumziko na fainali
itafanyika Jumapili. Alisema ufunguzi wa bonanza hilo utafanyika
Alhamisi kwa msanii, Jokha Kassim maarufu kama Kanga Moko, atachengua
kwa kutoa burudani ya muziki wa taarabu na Ijumaa kutakuwa na disko. “Bonanza
hili la miaka mitano ya Villa Park, si kucheza tu bali pia kufanya
mazoezi ili kujenga afya.Kauli mbiu yake ni kula ni lazima, michezo ni
afya," alisema Mtunga.
|
Posted: 12 Jun 2012 11:03 PM PDT
Na Zahoro Mlanzi
WAREMBO
12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni, mwaka huu
'Miss Kigamboni City 2012', leo wanatarajiwa kufanyiwa usaili kwa ajili
kumpata mshindi wa shindano hilo litakalofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa
Navy Beach, Dar es Salaam.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Mratibu wa shindano hilo, kutoka Kampuni ya K&L
Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema maandalizi ya zoezi hilo
yamekamilika na wanachosubiri ni siku ya shindano ifike.
Alisema
kitongoji hicho kina warembo wenye sifa na wanaojiamini ambao wamepania
kurudisha taji la Miss Tanzania kwenye Kanda ya Temeke.
Aliongeza
ili kuboresha shindano hilo Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia
'Wazee wa Ngwasuma' na msanii na mchekeshaji mahiri hapa nchini, Mpoki
watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Tunawaomba wadau wa
sanaa ya urembo kufika kushuhudia mrembo wa Kigamboni atakavyopatikana,
ni Kitongoji kilichoko sehemu pekee hapa nchini, hivyo ni vizuru
kushuhudia shindano hilo," alisema Somoe.
Aliwataja warembo
watakaochuana ni Susanne Jeremiah, Agness Goodluck, Elizabeth Boniface,
Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen
Kweka, Khadija Kombo, Linnah David, Rosemary Peter na Winnie Karaya.
Aliwashukuru
wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao ni Redd's,
Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global Publishers,
Nobro Collections, Times FM na Clouds FM.
Aliongeza kuwa warembo
watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika shindano hilo wataungana
na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe ili kuwania taji
la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment