Akipokea gari hilo kwa niaba ya
wananchi wa jimbo na Wilaya ya Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada huo na
kuahidi kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kusema kuwa, utendaji
kazi wa Rais Magufuli umekuwa ukiungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali na
kuwaomba watanzania kuzidi kumuombea kwa Mungu.
Kwa upande wake Dakta Nasoro Ally
Matuzya, amesema gari hilo limekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa umezingatia utekelezaji
wa malengo ya Milenia hususan lengo namba nne linalosisitiza kupunguza
vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya
Wilaya ya Chalinze Ndugu Saidi Omar Zikatimu amesema gari hilo la kubebea wagonjwa
litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo la Chalinze hususan katika
kusaidia kutoa wagonjwa ambao wako katika maeneo ya vijijini wilayani humo na
kuwafikisha katika hospitali ya Chalinze na hivyo kunusuru maisha yao kwa
kupata huduma za afya kwa haraka.
Mbali na Wilaya ya Chalinze kupata
msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa, tayari magari mengine mawili ya
kubebea wagonjwa yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu
mkoani Morogoro.
Hospitali mpya ya Wilaya ya Chalinze
imepanda hadhi kutoka kituo cha Msoga ambayo ilikuwa haina gari la kubebea
wagonjwa na hivyo kufanya usafirishaji wa wagonjwa kutoka hospitali hiyo hadi
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi au kutoka maeneo ya vijijini kuwa
mgumu.
No comments:
Post a Comment