Mwenyekiti
wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994
(UWKS) Dkt. Nelson Boniface akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa kwanza
wa Umoja huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini
Dar es Salaam.
Katibu
Msaidizi na Msemaji wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma
mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Bibi. Elizabeth Bisendo akifafanua jambo
wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika leo katika
ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria
na Mratibu wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 –
1994 (UWKS) Wakili Msomi Marko Anthony Nsimba akielezea namna
alivyoshughulikia suala la usajili wa Umoja huo wakati wa mkutano mkuu
wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip
Hotel jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
wanachama wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 –
1994 (UWKS) wakiwa katika mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo tokea
kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2011.
Baadhi ya
wanachama wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 –
1994 (UWKS) wakiwa katika mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo tokea
kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2011.
Mwanasheria
na Mratibu wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 –
1994 (UWKS) Wakili Msomi Marko Anthony Nsimba akikabidhi Cheti cha
usajili kwa Mwenyekiti wa Umoja huo Dkt. Nelson Boniface wakati wa
mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Anayeshuhudia ni Katibu Msaidizi Bibi. Elizabeth Bisendo na Katibu Mkuu
Godwin Ndaki.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994
(UWKS) Dkt. Nelson Boniface akionyesha Cheti cha Usajili wa Umoja wao
mara baada ya kukabidhiwa na Mwanasheria na Mratibu wa Umoja huo Wakili
Msomi Marko Anthony Nsimba (hayupo pichani) leo jijini Dar es
Salaam.Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa UWKS Janti Benjamini,
Katibu Mkuu Dkt. Godwin Ndeki na Kati Msaidizi Bibi. Elizabeth Bisendo.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994
(UWKS) Dkt. Nelson Boniface akipitia Katiba iliyosajiliwa ya Umoja wao
mara baada ya kukabidhiwa na Mwanasheria na Mratibu wa Umoja huo
UWKS 1991-94 yazinduliwa
Na: Mwandioshi Wetu.
Umoja
wa waliosoma shule ya sekondari Kigoma mwaka 1991-1994 umezinduliwa leo
rasmi baada ya mwanasheria wao Wakili Marko Anthony Nsimba kukabidhi
cheti cha kusajiliwa na katiba ya umoja huo kwa wanaumoja huo hii leo.
Akizungumza
baada ya kupokea cheti hicho, Mwenyekiti wa Umoja huo kwa niaba ya
wanachama Dk Nelson Boniface amesema, lengo kuu la UWKS kuwakutanisha
pamoja wanafunzi waliosoma Shule hiyo kuanzia 1991-94. Boniface
ameongeza kuwa pamoja na kukutana, lakini pia nikusaidiana katika shida
na raha kushiriki katika mambo mbalimbali ya maendeleo katika taifa letu
sambamba na kutoa ushauri, michango ya misaada ya hali na mali kwa
jamii yenye uhitaji.
Aidha
umoja utashirikiana na taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za
Kiserikali katika maendeleo ya jamii ya watanzania. Wakati huohuo
amezitaja baadhi ya changamoto ambazo umoja huo umekutana nazo ikiwa ni
pamoja na baadhi wahitimu wenzao kutoamini kuwa wanaweza kuwa na umoja
na wengine wakithubutu kusema ni kupoteza muda.
“pamoja
na kupotezana kwa Zaidi ya miaka 20 iliyopita, lakini sasa tumeweza
kukutana tena ingawaje siyo wote laakini kwa kuwa lengo letu ni moja
tuna amini na wengine watakuja taratibu” amesema . Mmoja wa wajumbe wa
UWKS Mbunge wa Kigoma Mjini Zito Kabwe(ATC) amesema tuliopo ni wajumbe
18, imefanyika kazi kubwa kutafutana lakini naamini kila mmoja wetu
atabeba jukumu la kuwavuta wengine hadi darasa litatimia.
Kabwe
ambaye ni ameweka wazi kuwa Umoja huo utapeleka msaada katika shule hiyo
kwa kuwa imechakaa na kurekebisha baadhi ya miundombinu iliyochakaa kwa
kuwa wakati wao wakisoma walikuta maabara zikifanya kazi lakini kwa
sasa zimechakaa, hiyo ni kama kurudisha shukrani kwa jamii.
Umoja
wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma kuanzia 1991 -1994 (UWKS)
umetokana na kikao cha wanajumuiya cha tarehe 06 Machi 2011ambapo ndipo
lilipopatikana wazo la kuwa na Umoja huu ndipo wajumbe walipo azmia
kuanza mchakato wa kusajili Umoja huo ambao leo umezinduliwa rasmi.
Wajumbe waliojiorodhesha idadi yao inafikia 40 mapaka sasa.
No comments:
Post a Comment