MBUNGE
wa Ilemela, Angelina Mabula ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na
maeneo ya karibu kujitokeza kwa wingi kwa sababu ya unyeti wa Tamasha
la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Akizungumza
jana, Mabula alisema Tamasha la Pasaka ni la Watanzania wote, lakini
mwaka huu wamepata bahati ya kufikiwa na ujumbe wa neno la Mungu ambao
utakemea maovu kama mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi 'albino'.
"Binaadam
anatakiwa kubaki na heshima yake, kwani hakuna maisha bora ambayo
yanatokana na kuwaua na kuwakata viungo wenzao, si ubinaadam kabisa
tunatakiwa tumrudie Mungu kwani ndio kimbilio," alisema Mabula.Mabula
alisema Tamasha la Pasaka limebeba ujumbe wa neno la Mungu hivyo ni
nafasi kwa wakazi wa Ilemela na maeneo ya jirani na hata mikoa mingine
kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.
Aidha
Mabula alisema thamani ya Tamasha la Pasaka ni kubwa hivyo Watanzania ni
nafasi yetu Watanzania kumfikishia Mungu sala zetu.Naye Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema
maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea vizuri, hivyo wakazi wa
mikoa ya Kanda ya Ziwa wakae mkao wa kula.
No comments:
Post a Comment