TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 17, 2016

WAZIRI SIMBACHAWENE AMPA SIKU TATU RC KUUNDA KAMATI YA KUCHUNGUZA VIONGOZI NA WAKUU WA SEKONDARI WANAOLALAMIKIWA KUTUMIA VIBAYA UONGOZI WAO


Na Woinde Shizza, Karatu Vijiji

WAZIRI waNchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh,George Simba Chawene amempa siku tatu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda kuhakikisha anaunda kamati maalumu ambayoitafanya uchunguzi kubaini viongozi wa vijiji na wakuu wa sekondari wa wilayaya karatu wanaotumia vibaya uongozi wao hali iliyopelekea kuwepo kwamalalamiko.

Waziri Simbachawene aliyasema hayo wakati alipokuwa kwenye uzinduzi wa majengo ya ofisi na maendelo ya parokia na Karakana ya Chuo cha Ufundi Audrey Veldamaniliyopo kijiji cha Kitete Wilayani Karatu Mkoani Arusha ambavyo vinamilikiwa naKanisa katoliki Parokia ya Kitete.

Alisema kuwa kutokana na malalamiko aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja nawananchi katika Wilaya ya Karatu kuhusiana na kuwepo kwa baadhi ya viongozi wavijiji na wakuu wa shule za Sekondari kutumia vibaya uongozi wao ahakikisheanaunda kamati hiyo ili watakapobaini ukweli waweze kutumbuliwa majipu harakasana.

‘’Mkuu waMkoa nakupa siku tatu fatilia jambo hili kuna ubadilifu mwingi upo wizi wafedha wakuu wa shule wamekuwa wakiiba hela za wazazi,ufaulu kwa wanafunziumeshuka sana katika shule zote za Karatu ,viongozi wa kijiji, kata hawako makini na kazi sasa unda kamati ili tupate ushahidi wa kudumuili tuwatimue’’alisema Simbachawene.

Pia alimpasiku saba Mkuu huyo wa Mkoa kuhakikisha anashushughulika suala la kuboreshamiundo mbinu hususani barabara ambayo imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa vijijivi navyozunguka Wilaya ya Karatu akidai kwamba anapaswa kukutana na wakurugenziwa monduli na karatu kukutana na kupanga namna ya kufungua barabara  kuanziaManyara,inayopita sabasaba ,kitete ,Lostete mpaka serera katika kipindi hikicha mwaka huu wa fedha huku akimsihi kuanza kufikiria Barabara ya Namangakupitia Monduli ,ziwaNatron ili iwe ya Mkoa.

Alidai kuwa kuwepo kwa barabara hizo kutasaidia wananchiwa kufanya biashara zao kwa urahisi huku watalii wakimiminika kwa wingi jamboambalo litafanya wafanyabiashara kutumia Raslimali za hapa nchini.,Nae Mkuu waMkoa wa Arusha Felix Ntibenda alisema kuwa anawasihi viongozi wa Wilaya yaKaratu kuwafanyia kazi wale watendaji na wenyeviti wanaokwamisha kazi zamaendeleo ya Nchi kuwafukuza kazi maramoja kabla ya kufika kwake.

‘’Nawambiawakurugenzi na wakuu wa wilaya wafukuzen kazi hao wanaokwenda kinyume na kazitutapata wengine hata kama walichaguliwa na wananchi tambua masuala ya uchaguziyameisha kwisha hakuna chadema wala CCM nisingependa nisikie malumbano bali nikufanya kazi kwa kuheshimu madaraka yaliyoko madarakani’’alisema FelixNtibenda.

Awali akitoahotuba yake mbele ya waziri Paroko waParokia hiyo Padri Costantine Changwe alisema kuwa katika kijiji cha kitete wananchikwa ujumla wanakabiliwa na changamoto kubwa ya barabara huku akidai kwambawakati wamasika huwa wanadondoka makorongoni na wengine kupoteza maisha jamaboambalo limekuwa kero kubwa kwa jamii hiyo.

Alisema kuwakumekuwepo na viongozi wa vijiji na vitongozi wa Mbulumbulu ambao wamekuwa nauongozi mbaya kwa madai kwamba wanalumbana kisiasa hawataki maendeleo hukuwakipingana na kauli ya hapa kazi . Alisema kuwawamekuwa wakitanguliza siasa bila uzalendo kwa maslahi yao binafsi huku akisemawanapaswa kunyoshewa vidole hata kutumbuliwa majipu jambo
ambalo litasaidiakuleta maendelea ya wanyonge

No comments:

Post a Comment