Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya,Emmanuel Humba akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani).
Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii
akiongea na waandishi wa habari kuhusu kikao cha wanachama wastaafu wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya.
Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewataka wanachama wastaafu
wanaohudumiwa na mfuko huo kutoa maoni na ushauri wa namna ya kuboresha
huduma zitolewazo kwa ajili yao.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya
Jamii Bw.Eugin Mikongoti alipokua akiongea na wanachama wastaafu katika
mkutano ulioandaliwa na NHIF.
“Hatukuwahi
kuwa na mkutano maalumu wa wanachama wastaafu,ndiyo maana mkutano huu
kwetu ni wa kihistoria na tunaamini ni muhimu kukutana na wastaafu peke
yao ili kutoka kwao tusikie, siyo tu huduma nzuri wanazozipata bali pia
changamoto wanazozikabili ili kwa pamoja tuweke mkakati wa
kuzitatua”alisema Mikongoti.
Bw.
Mikongoti ameongeza kuwa, wakati wote wamekua wakipokea na kuzingatia
ushauri na maoni ya wadau wake wote, kwahiyo wanatarajia mkutano huu na
wanachama wastaafu utakua ni uwanja mzuri wa kubadilishana mawazo na
kupata ushauri wa namna ya kuboresha zaidi huduma zao.
Aidha,Mwenyekiti
wa kikao cha wastaafu,George Yambesi amewasihi wastaafu wenzie
wafuatilie kwa makini na waulize maswali kwa kadiri watakavyoweza ili
wawe na uelewa mpana kuhusu huduma za mfuko wa NHIF kwakua hii ndio
fursa yao maana hawapo kwenye ajira na hivyo sio rahisi kupata taarifa
za mara kwa mara.
Pia
Bw. Yambesi kwa niaba ya wenzake ameipongeza Serikali kwa kuufanya
Mfuko huu kutoa huduma za matibabu kwa wastaafu pia amewashukuru
viongozi waasisi wa Mfuko kwa kuweka misingi bora ya kuwashughulikia
wastaafu bila kukata tamaa.
Naye
mmoja wa wastaafu kutoka Shirika la Utangazaji la Taifa Ngalinecha
Ngahyoma anaishukuru NHIF kwa kuwasaidia wastaafu kupata matibabu maana
gharama za matibabu ni kubwa bila kuwa na bima za afya wastaafu
wasingeweza kulipia huduma hizo.
No comments:
Post a Comment