Viongozi
wa kampuni ya saruji ya Lafarge wakiwa pamoja na watendaji wa
Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakati wa kukabidhi mifuko 1,000 ya saruji
kwa ajili ya mabweni yaliyoteketea ya shule ya Sekondari Iyunga.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro(kushoto)
akipokea mifuko 1000 ya saruji kutoka kwa Meneja Uajiri watu wa kampuni
ya saruji ya Lafarge Bryson Tarimo kwa ajili ujenzi wa mabweni ya shule
ya Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi karibuni.
Meneja
Rasilimali Watu wa kampuni ya saruji ya Lafarge ya jijini Mbeya Bryson
Tarimo akizungumza mara baada ya kukabidhi mifuko 1,000 ya saruji kwa
ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga ambayo hivi
karibuni yaliteketea kwa moto,Kampuni ya Lafarge imetoa mifuko ya saruji
yenye thamani ya shilingi milioni 14.
Mkuu
wa shule ya sekondari ya Iyunga Edward Mwantimo akitoa neno la shukrani
mara baada ya kukabidhiwa mifuko 1,000 ya saruji kutoka kampuni ya
Lafarge ya jijini Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya
Sekondari Iyunga ambayo hivi karibuni yaliteketea kwa moto ambapo pia
alielezea madhara yaliyotokana na moto uliosababisha kuungua kwa mabweni
ya wanafunzi wa shule hiyo.
Kampuni
ya Saruji ya Lafarge Tanzania (Mbeya Cement Company) imetoa msaada wa
zaidi ya mifuko 1,000 ya saruji na vifaa vingine vya ujenzi kwa shule ya
Sekondari ya Iyunga mkoani Mbeya kufuatia mabweni ya shule hiyo kuungua
moto hivi karibuni.
Mashine
ya kampuni hiyo pia itatumika kufyatua zaidi ya matofali 40, 000
yanayohitajika kukamilisha ujenzi huo na kufanya jumla ya msaada huo
kuwa na thamani ya shilingi 14 milioni. Akizungumza kwenye makabidhiano
ya msaada huo, Meneja Rasilimali Watu wa Lafarge Tanzania, Bryson Tarimo
alisema “tulipata habari za kushtusha kuhusiana na tukio la moto ambao
uliteketeza miundombinu ya shule pamoja na mali za wanafunzi.
Tunatambua
kwamba huu umekuwa ni wakati mgumu kwa uongozi wa shule pamoja na
wanafunzi.” Aliongeza kusema kwamba Lafarge inaamini kwamba elimu ni
muhimu kwa maendeleo ya mustakabali wa Tanzania na pia kwamba elimu
itasaidia kufungua mianya ya fursa mbalimbali kwa Watanzania. Tarimo
alieleza kwamba Lafarge ina jukumu la kujenga mabweni hayo ili
kuwarudishia wanafunzi wa Sekondari ya Iyunga mazingira mazuri ya
kujisomea. “Hii ni sehemu ya jukumu letu kuifikia jamii na kuisaidia
jamii pamoja na taasisi mbalimbali zilizopo mahali tunapofanyia kazi.”
Aliongeza:
“Uhusiano wetu na shule hii ni mkubwa sana kwa sababu tunaelewa
imewafundisha baadhi ya watu ambao hivi sasa wanaendesha kiwanda chetu
na kutufanya tuendelee kuwa na mafanikio. Tunataka kuona wanafunzi
wakirejea madarasani na walimu wakiendelea kutimiza majukumu yao kama
kawaida kwani azma yetu ni kuona shule hii inapata mafanikio na kuwapa
wanafunzi fursa ya kutimiza ndoto zao na kuwa na mustakabali mzuri.
Mtazamo
wetu ni kuona Tanzania ikiwa nchi inayotoa fursa ya elimu kwa kila
mtoto ili watoto hawa wote kila mmoj aweze siku moja kuchangia maendeleo
ya nchi hii.” Tarimo alisema kwamba Lafarge inajali maendeleo ya jamii
na ina fahari kuweza kutoa msaada huu kwa shule ya Sekondari ya Iyunga
kufuatia moto ulioteketeza mabweni ya shule hiyo.
Tunaamini
msaada huu utarejesha hali ya kawaida katika shule hii na sisi kama
sehemu ya jamii hii tunapenda kuona wanafunzi hawa wakiishi katika
mazingira salama.” Tarimo aliyaomba makampuni mengine na taasisi
mbalimbali, watu binafsi na jamii kwa ujumla kuisaidia ujenzi wa shule
hiyo.
No comments:
Post a Comment